Rais JK ungesema neno moja tu nasi tungepona | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais JK ungesema neno moja tu nasi tungepona

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Profesa, Jun 30, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, pamoja na mikakati yako yote unayoitumia kutawala nchi hii, sijajua wanaokuzuia kuongea na wananchi mambo yanapokuwa moto ni hao wasaidizi wako au ni wewe mwenyewe na hulka zako tu? Ninashawishika kuamini kuwa kama ungenena jambo moja tu, basi mengi ya yanayoendelea yasingetufika hapa tulipo. Ninarejea mifano mingi tu ya mengi ambayo ulikuwa na busara za hali ya juu katika kuyatuliza, basi na haya ya sasa nena neno moja tu. Na pia sidhani kama ni busara sisi tukupe wewe dhamana halafu kama kiongozi wa nchi umekaa ububu mpaka yazidi weee ndiyo utokee kusema, hayakukeri wewe? au mwenzetu kwakuwa hukatikiwi umeme, hupangi foleni, hununui chakula, hugombei daladala, na huendi hospitali kama sisi wengine? na hii tabia ya kutumia Wazee wa CCM kuongea mambo nyeti ya kitaifa, inaharibu mambo haijengi na inakupotezea umaarufu. Kwani hawa wengine walioko nje Mh raisi sio wa kwako? Hebu weka mambo ya chama pembeni na ya serikali, na uwe makini sana pamoja ya kuwa chama ndicho kilichokuweka madarakani, lakini hawa ambao ni wa vyama vingine ni wako kama raisi, ila si wako kama mwenyekiti wa CCM.

  Na kingine ninachotaka kujua, nani anaekuburuza humo ndani, nani ambaye anakujaza maneno ya hofu tele? Nani ambaye badal;a ya kukuipa moyo na kukushaiuri mikakati ya kiuhamasishaji anakueleza umbeya wa mtu mmojammoja na kukwambia huyo mmoja ndiyo chanzo wakati wewe kama raisi hupaswi kabisa kuangalia changamoto au matatizo katika sura ya mtu mmojammoja au kundi fulani, kwani hiyo ni kasoro kubwa na ni upotoshaji, unapaswa kuangalia mfumo ambao mtu mmoja mmoja huyo hawezi kufurukuta. Hao waliokuja na wazo la kukushauri umshughulikie mmojammoja wamekuponza, wanakujengea maadui wa ndani wengi tu, pamoja na sifa zote ulizonazo nje. Na mtu mmojammoja hugharimu muda mwingi sana na mambo huendeshwa kibinafsi na si kiutaratibu wa kimfumo ambapo serikali ndiyo inapaswa ksushughulika nao na kuleta chuki.

  Sasa basi, Mheshimiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, muda unao, anza kuangalia nchi hii kwa taswira mpya. Nina hakika watu watageuka miyoyo na utaiokoa nchi hii na majanga yaliyopo. Mfano:

  1. Anza kushughulikia kila jambo zito linaloibuka kwa kulizungumzia hadharani na kwa positive na kwa wakati, usisubiri lichache, wnakudanganya, umaarufu wako utapanda iwapo utaanza kufanya hivyo. Bila kumshutumu mtu, ukielezea hali halisi, na ukielezea mipango na madhumuni, na mara zote kufunga hotuba zako na neno la kutia moyo na motisha utakaowafanya watu kuchukua nafasi zao kushiriki katika kulishughilikia tatizo husika. Mfano, kama fedha zimepungua katika serikali ni kwanini? Iwapo unatuambia uchumi unapaa, makusanyo yamevuka malengo? Inamaanisha nini kunapokuwa hakuna fdha serikalini je ni kuweka akiba kugharamia Sensa (Mh Mkapa aliwahi kuahirisha sensa ili kukusanya fedha za kutosha)? Epuka kabisa kumshutumu mtu binafsi, elezea udhaifu wa mfumo na jinsi mnavyokabiliana nao. Unadhani watu hawajui serikali haina fedha za kutosha? Ila tabia za viongozi wa serikali kudharau wananchi na kudharau malalamiko na matatizo ndiyo inayotufikisha hapa tulipo. na mbaya zaidi wanaokuja kukueleza badala ya kukushauri kuhusu njia bora za kulishughulikia wanakueleza adui au mtu anaesababaisha haya, no that is wrong. Kama mfumo una kasoro, basi mgomo utatokea bila ya serikali kujua, ila serikali inaweza kuwa na taarifa za mipango hatarishi na kutumia mbinu muafaka bila kumuathiri mtu yeyote kuyashughulikia hata ikiwezekana kuzuia maandamano bila nguvu wala vurugu. Tumia muda mchache tu na uwe unasema maneno machache, pa kukaripia karipia, pa kutoa mungozo toa muongozo, pa kusihi sihi, pa kuomba rashi omba radhi, nchi hii itapona.

  2. Badilisha mtu anaekuandikia hotuba, hazina msisimko wa kutosha pamoja na kuwa na pointi nyinigi. Usisahau, ukiongea wewe huongei na wana CCM tu, epuka kutumia maneno kama wenzetu wa vyama vingine... NO! big No! waaache akina Katibuwa CCM na akina Katibu Mwenezi wafanye kazi hiyo, pale wewe hotuba zako zimguse kila mtu.Usisahau pia unaongea na watu weney upeo na Elimu ya aina mbalimbali, huwezi kutumia maneno ya kingereza bila ulazima, na pia lugha nzito ya kitaalamu kupita kiasi bila ulazima. Weka vionjo pale inapobidi kunogesha hotuba, cheka panapopaswa kucheka, kasirka na foka kabisa panapopaswa kufoka na huzunika ikibidi. Tumia propaganda vizuri najua wewe ni msomi wa hili na watu wanataka kuvutiwa na kusisimkwa na hotuba.
   
 2. Radhia Sweety

  Radhia Sweety JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 4,448
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 180
  Atasema nini wakati urais wenyewe kaupata kwa kupewa na wanaume wenzake. Na sasa hivi ameungana na zobakiloba lingine Mizengo Pinda basi ni LIWALO NA LIWE TU. Sasa hivi hata ukiyauliza kwa nini maisha ni magumu yatacheka kwanza hee hee hee hee hee hee hee hee hee........liwalo na liweeeeeee
   
 3. Ndechumia

  Ndechumia JF-Expert Member

  #3
  Jul 1, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 1,015
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  kwan huwa unapita humu?
   
 4. MKL

  MKL Senior Member

  #4
  Jul 1, 2012
  Joined: Mar 2, 2012
  Messages: 126
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  SUBIRINI KUONGOZWA NA WACHINA JK AMESAHAU KUWA YEYE NI RAIS KWA SASA YUKO KWAO MSOGA ANAOGOPA KURUDI ATAPOPOLEWA MAWE KAMA JANA TEGETA liwalo na liwe hahahahahah
   
 5. Jakubumba

  Jakubumba JF-Expert Member

  #5
  Jul 1, 2012
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 1,627
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Watu mna roho ngumu, bado tu mna imani na huyu mtu!!!!!!!!! Hivi Leo kulikuwa na hotuba?
   
 6. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #6
  Jul 1, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Kumshauri Kikwete kwa mda huu ni kupoteza, kwani hata Binti yangu wa miaka mi4 kishajua tuna Rais wa namna gani....

  Na nikimwambia una akili kama JK analia sana mpaka nimbembeleze..... lol...!

  Leo ilikuwa ni siku ya hotuba uh??

  Nimekuja kujua ukitaka kuipenda hii nchi japo kidogo ni usifuatilie hadithi za huyu jamaa.
   
 7. Gwangambo

  Gwangambo JF-Expert Member

  #7
  Jul 1, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 3,655
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Hotuba yake itauwa hivi "Ndg watanzania wenzangu, naona nchi yetu bado inakabiliwa na matatizo mbalimbali Waziri mkuu sikujua kama ni kilaza hivyo, wabunge na mawaziri wote ni legelege, madaktari jeuri, nimejaribu kutuliza mgomo wao kwa kumuondosha yule Ulimboka vijana wangu wamechemka, Ndg wananchi nimeona niagize madaktari, wabunge, mawaziri na waziri mkuu toka nje Hapo vipi?'
   
 8. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #8
  Jul 1, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Natumaini hatafanya kosa kwenda safari nje na kuacha nchi katika hali hii
   
 9. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #9
  Jul 1, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,328
  Likes Received: 22,172
  Trophy Points: 280
  Raisi anayeongoza kwa kutoa ahadi nyingi bila ya kutekeleza huyo ni sawa msaliti.
  Amewasaliti watu wake.
   
 10. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #10
  Jul 1, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,746
  Likes Received: 12,826
  Trophy Points: 280
  kweli kabisa
   
 11. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #11
  Jul 1, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,746
  Likes Received: 12,826
  Trophy Points: 280
  Huo ushauri ni mzuri kama ange ufuata lakini kwa jk ni kama una mpigia mbuzi gita.
   
 12. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #12
  Jul 1, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  karibuni ataongea na wazee wa ccm pale diamond, huu ni upepo tu utapita
   
 13. kelvito

  kelvito JF-Expert Member

  #13
  Jul 1, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 388
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu ushauri wako ni mzuri sana but sidhani kama jk ataufuata, tatizo lake hata humu huwa haudhulii, na wasaidizi wake hawampi haya. But leo ataongea namshauri asiongee mambo ya kulrta madr toka nje, amalize mgogoro hapa nchini!
   
 14. Money Stunna

  Money Stunna JF-Expert Member

  #14
  Jul 1, 2012
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 13,105
  Likes Received: 284
  Trophy Points: 160
  yuko Rwanda sasa hivi
   
 15. d

  daddi5 Member

  #15
  Jul 2, 2012
  Joined: Aug 24, 2008
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  hivi nyie mnataka rahisi kama mrema ambaye anakurupuka tu na kuongea bila kujua kina na kufuatilia sheria, mnafikiri ni mjinga? hawezi kuongelea jambo ambalo hana fact kamilifu, kamati zimekutana madocta wakasema tunaoenda kuongea na wenzutu turudi na jibu, instead wakagoma, nasikilizia response ya kamati ya madocta watajibu nini but most likely i think rahisi alisema ya ukweli, madocta wamekuwa frustrated wakaamua kuchukua sheria mkononi it doesnt make it right ndio maana sheria ziko. i differ na rahisi jinsi ya kuhandle hii crisis but i agree with his response serikali haitakuwa blackmailed, wakae chini waongee they wont get everything the need but it would have been a good start instead of derailing their achievments, waache kutumia their position in our society kuweka maskini watanzania rehani na kutaku kuforce serikali into submission!!!! na nyie mnaopenda kuropoka fanyeni research na facts zenu kabla ya kuanza kuropoka!!!
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...