Rais JK na Kilimo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais JK na Kilimo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by idumu, Jun 5, 2009.

 1. idumu

  idumu Member

  #1
  Jun 5, 2009
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  JK baada tu ya kutoka US anahimiza wawekezaji wawekeze kwenye KILIMO?? Kuna siri gani hapo?? Je kuna watu amesharobb US. Je kuna wazungu watakuja soon?/ Wapi watawekeza?? Bonde la Kyela?? Bonde la Mbalali?? Ni kweli tumezamilia kilimo. Soko lipo??
  Tujiulize.

  Ni maoni yangu sina baya kwa RAIS WETU. NAMTAKIA MAFANIKIO KWA HILO.
   
 2. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #2
  Jun 5, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  VERYSIMPLE

  Taifa ambalo haliwezi kujilisha ni aifa ambalo haliwezi kupiga hatua kwenye mengineyo kama technology and so on

  lakini tukianza kuongelea kilimo leo basi jiandae kusikia semo nyingi jinsi ganiserikali yetu ilivyoumiza kilimo kama vile NYERERE kwa sababu anazozijua mwenyewe KUNGOA RELI toka DAR KWENDA LINDI

  hii imefutwa kwenye historia ya nchi yetu kwa sababu ambazo wanazijua wenyewe lakini watu wa pwani wanaamini kuwa ukweli wa kungolewa kwa ile relini ilichangiwa zaidi na chuki yake dhidi ya WASWAHILI wa PWANI

  mbaya zaidi CCM inajichanganya kwenye ilani ya Uchaguzi ya 2005 kwa kutaka kuendeleza viwanda halafu kilimo ndio kifuate

  soma Ibara ya 25 (i) utaelewa nazungumzia nini


  So far nadhani hii inaweza ikawa legacy nzuri ya PINDA kama ilivyokuwa ya LOWASSA na shule za KATA...sasa waache biashara ya kutembelea mashamba na wafanye mpango wa kufungua assembly ya ma TREKTA
   
 3. idumu

  idumu Member

  #3
  Jun 5, 2009
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hoja njema kaka??
  NOTED

  MWANANCHI
   
 4. F

  Felister JF-Expert Member

  #4
  Jun 5, 2009
  Joined: Aug 5, 2008
  Messages: 377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hili swala la Kilimo limesemwa nalisikia mara zaidi ya tatu sasa naomba tujiulize hivi mnadhani kwanini mataifa ya nje (yaliyoendelea) yameanza kuongelea kilimo nakujidai kutushauri jinsi ya kufanya? Watanzania tunapaswa kuelewa siasa ya dunia kwa sasa hasa ukizingatia suala la biashara na kilimo (WTO in general) .... tunatakiwa kuwa makini sana lolote tutakalo amua sasa hivi lina implication kwenye maisha yetu ya baadae. Niukweli ulio wazi kwamba kama tutajipanga vizuri umaskini tulionao utakuwa ni ndoto baada ya muda mfupi sana. Kama tukiongozwa na ubinafsi tujue kuwa tumepoteza nafasi muhimu sana katika maisha ya taifa letu kwa kudhani kuwa mimi nikifaidika wengine shauri lao the result will be all of us loosing forever. Kwa wenzetu wote sisi tuko sawa; tumewekwa kundi moja ila ndani yetu kuna matarishi na manamba (hii ni perception yangu)... wao kwanza sisi baadae.......

  USHAURI tutulie tujipange vizuri tuangalie policies zetu kwa macho ya kitaalam zaidi na kufanya positive analyses na siyo normative analyses kuona nafasi yetu ni ipi katika biashara in terms of absolute and comparative advanteges. Therefore ili kuenda kwenye high utility what should be the strategy in regards to SWORT. Mambo ya kualika tu watu na kudhani wanayosema ndo ukweli wenyewe huku wao wamejipanga na sisi tunasema hewala mgeni aje mwenyeji apona hii itatuponza na tutaishia kusema basi tena....... tumesha sign mkataba na mahakama inayo amua tayari imeshaandaliwa na WTO huko hakuna longo longo hukujua basi sorry subiri mkataba ukiisha utajipanga vizuri. Nasema haya kwa mapenzi mema kwa nchi yangu mkinisikiliza nitafurahi mkinipuuza nitawasikiliza na sintakuwa na chakujilaumu maana nimesema ninachoamini na hivyo dhamiri yangu itabaki kua safi.
   
 5. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #5
  Jun 5, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  soko liko kwao sio kwetu alafu mzungu huyu anaekuja kulima kwenye ardhi yetu bado baadae atuletee msaada wa chakula eti tuna njaa hii ndio akili ya mtu mweusi
   
 6. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #6
  Jun 5, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145

  Hii message sio tu inamzalilisha Rais, bali pia Waziri Mkuu Pinda, ambaye tangu aingie alishasema kitu kikubwa atakachofanya ni kumsaidia Rais kwenye issue ya Kilimo.

  Pia unawadhalilisha waandaji na wizara ya kilimo kwa pamoja kwa maana kwamba wote hawa hawakujua kwa nini waliitisha ule mkutano.

  Na kuna mengi alishafanya kama wewe ni mfuatiliaji mkubwa. alafu kumbuka mkutano kama hule kwa watu wa serikali utakuwa umeeandaliwa kama miezi sita iliyopita hivi.

  Sasa kweli kwa maelezo hayo unathubutu kusema agenda ya kilimo imetoka marekani.

  Shindwa na ulegee.

  Nadhani tufike mahali tuheshimu ndugu wengine.
   
 7. F

  Felister JF-Expert Member

  #7
  Jun 5, 2009
  Joined: Aug 5, 2008
  Messages: 377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Sidhani kama kweli nia ya mwandishi ni kama ulivyo mhukumu. Jaribu kuwa muungana na mwelewa yeye katoa maoni yake na wewe toa yako bila kumuwekea maneno mdomoni mwake. Nadhani nivizuri kuwa positive kwa critics za watu maneno yako yana vunja moyo na inakandamiza democracy tena mimi naona niyakinafiki ili wewe uonekane mzuri mwenzako aonekane mbaya. Tabia hii si nzuri na inarudisha maendeleo nyuma na kusababisha confrotations badala ya cooperation katika maswala ya kitaifa.Samahani kama nitakuwa nimeku perceive vibaya.
   
 8. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #8
  Jun 5, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kuna mambo ambayo nadhani ni muhimu Taifa likaweka mbele katika agenda zake za maendeleo, kuanzia sasa. Kati ya mambo hayo kilimo ndio jambo kuu.

  Baada ya mtikisiko wa uchumi duaniani (GFC), nchi nyingi za ulaya na marekani zimetambua kuwa Afrika inaweza kuwa mshiriki mkubwa katika kuweka maslahi yao salama zaidi. Imedhihirika hivyo kwa kuwa, waliokuwa wamewekeza Afrika, pesa zao na vitega uchumi vingine vimekuwa salama zaidi kuliko walikuwa wamewekeza ulaya, Asia na Marekani. Hii inatokana na Afrika kutokuwa na misukosuko mingi au harakati nyingi za kiuchumi kulinganisha na nchi zilizoendelea.

  Katika wakati huu, nchi itakayowekeza kwenye kilimo ndio itakayonufaika zaidi. Maana dunia nzima inahitaji chakula kutokana na hali mbaya ya hewa na uchumi wa dunia kutikisika. Tanzania ina nafasi muhimu sana katika hili kwa kuwa ina ardhi nzuri na imezungukwa na maji mengi (maziwa, mito na hata bahari) kila upande. Maji Tanzania yako mengi hata chini ya ardhi.

  Wawekezaji wengi watajitokeza na kuitaka serikali iwape nafasi ya kuwekeza kwenye kilimo hapa ila kwa masharti ya kumilikishwa ardhi na si kukodisha kutoka serikalini. Hii inaweza ikabadili sheria za ardhi na kuwa mwenye ardhi anaimiliki moja kwa moja (100%). Wawekezaji hutumia upungufu huu kukwepa kuwekeza nchini, na serikali haitaweza kuacha hali hiyo iendelee kwa muda mrefu. Pressure ni kubwa sana.

  Kwa mtazamo wangu, mwekezaji yeyote mwenye nia ya kuwekeza kwenye kilimo hapa nchini ni vyema akapewa nafasi ya kufanya hivyo bila kujali ametoka wapi na soko lake liko wapi. Ili mradi tu analipa kodi zinazotakiwa na uzalishaji wake unaipa nchi tija bila kuvunja uhuru wa mTanzania (bila kutufanya watumwa).

  Inabidi waTanzania waanze kuamka sasa na kuona umuhimu wa ardhi. Nakumbuka alipokuwa anawasilisha bajeti ya wizara yake ya mwisho mwaka 2005, Keenja alisisitiza sana hili hasa akijua kuwa wawekezaji wanatamani kuja nchini kuwekeza kwenye kilimo na serikali imeanza kufikiria kuwakaribisha. Wakija wawekezaji hao, watachukua ardhi kubwa sana, hivyo kuna hatari kuwa baadhi ya watu wakakosa ardhi baada ya miaka kadhaa. Inabidi kuwa aggressive sana kujitwalia ardhi mapema.
   
 9. F

  Felister JF-Expert Member

  #9
  Jun 5, 2009
  Joined: Aug 5, 2008
  Messages: 377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Nakubalina na wewe kabisa kabisa na ambacho kinatoa msukumo wa hao wawekezaji. Kitu kimoja ni kuwa kazi ya kulinda haki ya raia ni ya serikali na si ya mtu binafsi haki hiyo ni pamoja na umiliki wa ardhi wa pamoja kama ilivyo sasa "A common property right" to all Tanzanians. Sheria yetu ya ardhi kwa upande wangu naona ni nzuri kabisa tatizo ni kuwa low social capital ndo inatatizo kwetu sisi. Kutokana na tatizo hili basi ndo maana kuna free riding characteristics kutokana na ignorance ya wengi na hivyo monitoring na evaluation haifanyiki vizuri. kama kungekuwa na balance kwenye information basi locals ni monitors wazuri sana. Kwa sababu hiyo hili tatizo ni short term tu kwani sasa hivi kutokana na technology information flow ni kubwa so whatever happens in one conner is heard by those in the other conner of the country. So backed with good policies in agriculture welfare ingekuwa distributed to the large group of people tofauti na kama private mode of ownership. Kwenye private mode wachache wananufaika na majority wanakuwa waajiriwa tu through renting a case of Latin America and India I think. Mfano wetu ni kama China sasa tukifuata model ya China vizuri na kufanyia modification to our own particularities welfare ya watu wetu itakuwa better off.
   
 10. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #10
  Jun 5, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  umezungumza ya kwamba wawekezaji wana-demand 100% unadhani ni kwa nini? ndio hue elewa wenzako si wajinga wana fikiria mbele na tayari wameshajifunza na makosi ya nyuma investment only people can change their mind anytime. why not let the Africans work on their farms and they could come as buyers of the final produce at the Market Price. no awawezi kukubali hilo kwa sababu nia ni kutudidimiza mwelewe mzungu afikirii leo, ana fikiria kesho ndio maana yupo alipo, always ahead of you anajua iko siku atakuwa mzee, atafariki yeye lakini watu still watahitaji kula kwao. sasa nasisi iko siku tutaelimika tutakuwa wengi naa tutahitaji chakula kingi zaidi kwa hivyo hayo mashamba tutayataka alafu itakuaje. we need to think like he thinks to play his game. si kweli kwamba wana akili za kutushinda wana system ya long term na kufikiria before they jump into things therefore always learning from their mistakes. sitaki kurudia ya Zimbabwe.

  yes at the moment a long term lease should be the solution. they should never get 100% control huo utakuwa ni upuuzi utakao watesa wanetu.

  Mungu Ibariki Tanznania
   
  Last edited: Jun 6, 2009
 11. F

  Felister JF-Expert Member

  #11
  Jun 5, 2009
  Joined: Aug 5, 2008
  Messages: 377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kwakuongezea si kwamba wawekezaji wangekataa kuwa na partnership ambapo wao watakuja na technology sisi tuka contribute land and human resources tatizo ni katika ku bagain sisi hatuelezi haja zetu sawasawa na hii weakness ni advantage kwao. Wao wana propose then ni juu yetu kubagain on terms lakini tatizo is either wale wanaofahamu hilo wanachukua hiyo advantage at their own benefits na kusahau kuwa hiyo ni advantage kwa wenzetu na ni cost kwa society yetu or they realy dont know what to do. Mwisho wa siku kwakua welfare inagusa watu wengi na development ni integration in total kama shule zetu ni mbovu, barabara ni mbovu, drainage system mbovu, population increase kubwa mijini hizo kero hazitawapata wao (wawekezaji for they just come for a while) ila wale waliomua kufaidika hiyo income watakayoipata haiwezi kusolve general problems zilizopo so wote tuna kuwa worse off na zaidi tension ikizidi ndo mambo ya struggle for power na competition inapokuwa kubwa the strongest survive and the weakest r eliminated according to the law; although in reality the weak ndo wanaamua kujilipua kwasababu kufa na kupona zote ni sawa hana matumaini tena ya maisha. This is the long term effect ya kuexclude majority kwenye development.
   
 12. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #12
  Jun 5, 2009
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Binafsi nina mtazamo tofauti. Mapinduzi ya kilimo hayawezi kupangwa kutoka juu, yakajulikana kwa viongozi tu na kuzinduliwa kunduch Beach. Hii ni sawa na kumuomba Mungu mvua iendelee kunyesha mijini ili mavuno yawe mengi vijijini!
   
 13. K

  Koba JF-Expert Member

  #13
  Jun 5, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 494
  Trophy Points: 180
  Siasa za kina Pinda majukwaani kuhusu kilimo ni kupoteza muda tuu....kilimo ni kama biashara nyingine tuu ambazo zinahitaji capital & technology,good policy ili wanaoweka pesa zao watengeneze profit,bila hivyo vitu tutaendelea na njaa zetu na kuagiza nje,capitalist wote wapo after profit kama Tanzania ingekuwa inalipa leo wangekuwa wanagombania land lakini wakifikiria siasa zetu zisizoeleweka,rushwa,barabara mbovu,umeme wa uhakika hakuna...nani mwenye akili zake timamu ataweka pesa zake kupata hasara?
   
 14. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #14
  Jun 5, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Felister,
  Hakuna nchi yeyote katika dunia ya tatu au ya pili ambayo imeendelea kwa kutegemea wawekezaji peke yake. India ilipitia green revolution lakini walichofanya ni kuleta utaalamu wa teknolojia kutoka nje. Hicho tunaweza.
  Leo hii mwaka 2009 hatumhitaji Kaburu, Mmarekani, Mwingereza kuja kuchukua ardhi yetu kulima eti ni mwekezaji. Tunachohitaji ni utaalamu utakaomwezesha yule anayelima mpunga Kyela kuongeza zalisho lake kwa mwaka. Na kama ni soko la mpunga limejaa tele. Hatuhitaji kutafuta soko nje. Kuna Zimbabwe, Malawi, Kenya, hawa watanunua mazalisho yetu ya ziada. Siri ni kumwezesha mkulima wa Tanzania apanue uzalishaji wake na serikali ihakikishe mpunga wake hauozei shambani au kijijini. Shida ya viongozi wetu hivi leo ni kutafuta 10% ya rahisi lakini hawaoni kuwa wanauza nchi. Thailand wanazalisha mchele wao wenyewe kwa kutumia teknolojia ya kisasa sikusikia wanaita watu waje wawalimie. Hali yao inafanana sana na yetu Tanzania. Joto lile lile, mvua zile zile, n.k
   
 15. Kilasara

  Kilasara JF-Expert Member

  #15
  Jun 6, 2009
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 578
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Rais J.K. na Kilimo

  Mbona historia ya Tanzania hukuisoma vizuri Bw. Gama Theory? Hivi nyie watu wa Pwani mtaendelea kulaumu Nyerere mpaka lini? Nyerere hakung'oa Reli toka Dar kwenda Lindi, kwa vile hiyo Reli haijawahi kujengwa tangu Adamu na Hawa wakivinjari duniani.

  Kulikuwa na Reli toka Mtwara mpaka Nachingwea iliyojengwa baada ya World War II na wakoloni Waingereza wakitaka kuendeleza KILIMO CHA KARANGA (GROUNDNUT SCHEME). Hata Huko Kongwa, Mkoani Dodoma kulikuwa na Mradi huu. Bahati mbaya kutokana na pupa na kutozingatia utafiti yakinifu, yale materekta na matingatinga ya Waingereza hayakuweza kufanya kazi kwa ufanisi, na Groundnut Scheme ili-collapse.

  Reli toka Mtwara mpaka Nachingwea haikutumika baada ya mradi ya karanga kufa. Ama Wakoloni Waingereza au Serikali ya Nyerere baada ya kupata uhuru waling'oa ile Reli ambayo haikuwa inatumika. Labda ilikuwa ni makosa; lakini ingeachwa pale bila matumizi, wananchi wasiokuwa na kipato cha kutosheleza wangeweza kung'oa mataruma kama chuma chakavu!

  Sasa tukirudi kwenye suala la J.K. kusisitiza Kilimo, naona ni jambo la kupongezwa. Kitu ambacho nakitilia shaka ni kwamba anaonekana haamini kwamba la muhimu ni hii asilimia 80 ya WaTz wanaoishi vijijini wanaohitaji kuwezeshwa ili waingie ktk kilimo cha kisasa kujinasua kutoka umaskini wa kutupwa. J.K. anadhani ni wawekezaji toka California na Texas watakaoweza kufufua kilimo Tanzania!!!!!!!!!!

  Huku ni kupotoka. Kama sehemu kubwa ya nchi yetu inayofaa kwa kilimo itamegwa na kupewa wageni wawekezaji toka nje, naapa wengi wetu tutakosa pa kulima panapofaa na tutalazimika kwenda kuwa agricultural labourers ktk mashamba ya wageni. Vijana wengi watakimbilia mijini kuwa vibaka na wamachinga kuuza soksi, chupi na sidiria mitumba.

  Kinachotakiwa kufanywa na J.K. ni kuwezesha vijana waishio vijijini kupewa ardhi na mikopo yenye kulenga wakulima. Hiyo Benki ya Wakulima iliyopendekezwa na huo Mkutano J.K. aliyoongoza, iundwe mara moja. Iwe na wataalamu watakaosaidia vijana kulima kisasa, badala ya kuwalazimisha kuhamia mijini. Mazingira yatengenezwe kuhakikisha mazao ya mashamba yanauzwa soko la ndani na nje, tuondokane na huu umaskini wa kujitakia.

  J.K. na marais waliomtangulia wamekuwa na sera ya kutoa kipaumbele kwa wawekezaji wa kigeni katika madini na sehemu nyingine za uchumi wetu. Sasa anataka hata kilimo kinachowafanya 80% ya Watanzania wajaribu kubabaisha kimaisha, kichukuliwe na wageni. Ardhi eti itapewa wageni walime mazao ya kutumia humu humu nchini na ku-export. Hakuna guarantee kwamba wazawa wanatengewa ardhi na wanawezeshwa vipi. Tutakwishaaaaaaaaaaaa!
   
 16. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #16
  Jun 6, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  you have explained what is in my mind the trouble is most people dont see the plan ahead. your 100% on that most Tanznanians or Africans for that matter want everything now, then how do they achieve it they havent got a clue, this is why Europeans always take the advantage on us, as you've put it we dont how to negotiate i put it due to being naive and not having future plans.

  Mungu Ibariki Tanzania
   
 17. F

  Felister JF-Expert Member

  #17
  Jun 6, 2009
  Joined: Aug 5, 2008
  Messages: 377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Get my points right!! Sikusema wawekezaji ndo wataleta mapinduzi nononooo! Nachosema ni comperative advantages in trade kuzingatia siasa ya dunia kwa sasa. Wazungu wantechnology ya juu kwenye kilimo kuliko sisi. Kuwekeza sisi kwenye technology ambayo tayari ipo ni hasara kiuchumi lakini kama tutafanya trade na wale wenye technology na sisi kwakua wao ktk mazingira ya WTO conditions plus other internal constraints hawataweza kuendelea na kilimo kama walivyokuwa mwanzo then hii ni advantage kwetu sisi na kwao pia kama tuta amua kutrade on these basis utility ya kwetu na ya kwao itakuwa juu kuliko ilivyo sasa. Wao wana advantage ya technology sisi tuna land and human resources tuki cooperate badala ya ku compete na ku comfront each other production inakuwa kubwa zaidi. Tatizo lina baki kwenye who is benefiting and who is loosing in both sides and how can the benefiting comapasate the loosing. Pia equity in terms of welfare itakuaje na hiyo sasa ni kazi ya policy analysis as market can not do that kwani kuna externalities na perfect compettition is in reality non exisistent to make the market function well to reach socially optimal equilibrium.

  Sasa mwanzo wa thread nilielezea hii ndo maana nikasema naongezea. Kubali au kataa bado wenzetu wanatawala biashara na uchumi wa dunia sasa ili tuwa win diplomacy inahitajika na pia bagain tukiwa na facts ni muhimu kwani wao pia ukiwashinda kwa hoja si wagumu kukubali kama at all wao pia hawatakuwa worse off. Kinachotushinda sisi ni ubinafsi na kutopenda kuangalia mbeleni itakuaje na hii wanaijua ndiyo maana tunakuwa defeated either technically or sometimes by force or through devide and rule ili tusifikirie umoja kwa faida yetu.
   
 18. M

  Mkandara Verified User

  #18
  Jun 6, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Felister,
  Mkuu sikuelewi unaposema:-
  Nachosema ni comperative advantages in trade kuzingatia siasa ya dunia kwa sasa. Wazungu wantechnology ya juu kwenye kilimo kuliko sisi. Kuwekeza sisi kwenye technology ambayo tayari ipo ni hasara kiuchumi lakini kama tutafanya trade na wale wenye technology na sisi kwakua wao ktk mazingira ya WTO conditions plus other internal constraints hawataweza kuendelea na kilimo kama walivyokuwa mwanzo then hii ni advantage kwetu sisi na kwao pia kama tuta amua kutrade on these basis utility ya kwetu na ya kwao itakuwa juu kuliko ilivyo sasa.


  Nakuomba ufafanue, maanake kilimo cha technologia unayozungumzia hata sikielewi au unazungumzia Biashara na Uchimi kwa ujumla..
  Nachoelewa mimi, tatizo kubwa la Watanzania ni Mtaji sio technologia..na ndio maana hao WTO wanaingiza gear zao. Sisi ni wakulima kwa jadi na kilimo ni kipaji chetu toka tuumbwe.. Ndio maana tulichukuliwa Watumwa tukalime Pamba huko Marekani.Na kama sii wakulima wa mazao ni wavuvi au wafugaji wa jadi...yote haya yanaangukia ktk Kilimo kwa mapana yake.

  Kinachohitajika ni wataalam wa biashara.. Sii ktk uzalishaji wa kilimo kwani Tanzania tunao wengi sana, Kati ya graduate 100 wakati wa mwalimu 80 walikuwa upande wa kilimo.. hawa hatukuwatumia ipaswavyo na leo hii ni kizazi kinachoondoka (Baby boomers)..
  Inawezekana sana sisi kuyatumia mashirika ya usambazaji duniani kuingia nchini na kujenga viwanda vyao..Shirika kama la Tilda, hawawezi kuja jenga kiwanda cha Mchele wa Pishori ikiwa wakulima wetu hawalimi Pishori..Wakulima wetu hawawezi kupanda Pishori kwa sababu hawana mbegu, hawana uwezo wa kuagiza magunia elfu ya mbegu toka Pakistan au India wala hawafahamu kwamba mbegu hizo zinapatikana huko na mbolea gani gani inafaa...Ukitazama mazao yote utakuta wananchi wana uwezo, ujuzi na nguvu ya kuzalisha isipokuwa system ndiyo inawaangusha... Kilimo sii kipaumbele cha maendeleo ya Mtanzania.

  Nakumbuka wakati wa Mkoloni na miaka 10 ya mwanzo wa Uhuru Tanzania tulikuwa ktk ramani ya uzalishaji wa mazao mengi sana..Mashamba yote hayakuwa ya wazungu wala wawekezaji toka nje isipokuwa mipango bora ma msisitizo ktk kilimo ilifanyika toka shambani hadi kuingia sokoni.. sii leo kila mkulima anajitegemea hata kutafuta mbolea au maji shambani acha kutafuta soko na usafiri yota haya ni magumu kwa mkulima maskini...
  Nyie wasomi wenye nguvu serikalini ndio kazi mnayotakiwa kuifanya badala ya kutafuta mwekezaji toka marekani ambaye anaingia nchini na mtaji wa mkopo, kisha anawatumia wakulima wetu hawa hawa kama wafanyakazi.
  Kesho mtataka kudai ardhi yenu kama Zimbabwe na rais atakayefuata madai yenu ataonekana kuwa ni Mugabe.. Historia itasahau kabisa yaliyopita na mikataba iliyomwekwa sasa hivi..
   
 19. F

  Felister JF-Expert Member

  #19
  Jun 6, 2009
  Joined: Aug 5, 2008
  Messages: 377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mkandara asante kwa kuuliza,

  Naomba ni jaribu kufafanua nachomaanisha. Ninapoongelea technology sina maana kwa mashine na vitu kama hivyo nooo ila yenyewe pia inclusive. Katika kilimo ni pamoja na seed variety, irrigation technics, efficiency and effectiveness in production etc. Unapoongelea wataalam usiangalie vyeti tu ni pamoja na delivery capacity i.e transfering of the knowledge into realities. Sasa come to comparative and absolute advantage hii ni concept ya kiuchumi katika policy analysis. Nchi inaweza ikawa na absolute advantage kwa kuwa na uwezo wa kuproduce at low cost first kwa kuwa land is available and the labour is cheap pia weather ikawa favourable to the specific type of crop for example cotton. Nyingine ikawa na absolute advantage kwa production of cloth due to high technology and better quality cloth production. Lakini nchi hizo zote mbili zikawa na uwezo wa kuproduce both commodity and cloth although the first production kwenye comodity itakuwa kubwa na clothing ikawa kidogo due to its low technology. Ya pili due to weather na expensive labour productio yake ikawa siyo efficient kama ilivyo kwenye clothing. Now even if wote wana uwezo wakuproduce but if each country is to specialize in area where they have a comparative advantage the total production will be higher than if each is to produce independently. Because of these reasons thats why countries trade ili ku maximise utility for each will be better off by doing so.

  Kwa ufupi hicho ndicho nachomaanisha. Sasa WTO inataka kuliberalise trade maana kusiwe na barriers mambo ya kusema ooh kwanini waje au wasije then may be tujitoe WTO na tuendeshe nchi yetu kivyetu vyetu kama kweli its possible kuwa 100% sufficient. Kutokana na kuwa sisi ni signatory wa WTO then ndo tunatakiwa kujipanga kwa kuangalia SWORT na kuziangalia policies zetu za ndani jinsi tuta boresha maisha ya watu wetu na what are the safety nets maana its allowed in the rules governing trade bila kuinterfere market or if intervention ipo basi minimal na ziwe na sababu za maana. Ndo maana nikasema bagain ni muhimu sana maana bila hivyo sisi tutabakia watazamaji kilasiku nakuona wengine wakiendelea huku sisi tukifuata mkumbo.
   
Loading...