Lucchese DeCavalcante
JF-Expert Member
- Jan 10, 2009
- 5,471
- 734
Rais Jakaya Kikwete akijiandikisha kupiga kura kwenye kituo kipya cha kupigia kura kijijini kwake Msoga,wilayani Bagamoyo. Pembeni akiangalia ni msimamizi wa kituo cha kuandikisha wapiga kura cha Msoga Bi.Diana Fredrick. Kituo cha zamani cha Rais Kikwete kilikuwa Bwilingu, Kata ya Chalinze, wilayani Bagamoyo. Mama Salma Kikwete pia alijiandikisha kupiga kura kwenye daftari hilo la kudumu la wapiga kura kijijini hapo.
Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakikagua kwa makini vitambulisho vyao vipya vya kupiga kura walipojiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura na kupatiwa vitambulisho vipya huko kijijini Msoga wilayani Bagamoyo.Kushoto ni msimamizi wa kituo hicho cha wapiga kura Msoga Bi.Diana Fredrick.
Source: MichuziJr Blog.