Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,191
- 672
Rais Jakaya Kikwete apigwa picha upya kwa matumizi ya kiserikali Na Mwandishi Wetu
SERIKALI imebadilisha picha ya Rais Jakaya Kikwete iliyokuwa ikitumika katia shughuli za kiserikali (Official Portrait)
Akizungumza na waandishi wa habari jijini jana, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Kassim Mpenda alisema serikali imeamua kubadilisha picha hiyo baada ya kupata ushauri kutoka kwa wataalam mbalimbali wa masuala ya picha.
Mpenda alisema wataalam hao walishauri kuwa picha iliyopigwa baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa Rais mwaka 2005, haifai kwa matumizi kwa kuwa wakati huo, rais alikuwa anakabiliwa na uchovu na mawazo ya kuanza kazi hiyo mpya.
Alifafanua kuwa picha hiyo, ilikuwa haionyeshi sura halisi ya sura ya Rais kwa kuwa ilionyesha msongo wa mambo mbalimbali.
''Picha hiyo ilipiga mwaka 2005 mara tu baada ya Tume ya Uchaguzi kumtangaza kuwa ndiye mshindi wa urais; Hivyo kipindi hicho bado alikuwa na msongo na mavune (stress & strain) ya kampeni za uchaguzi wa mwaka huo,'' alifafanua Mpenda.
Mpenda alisema Rais Kikwete alilazimika kupiga picha katika kipindi hicho kwa kuwa ilikuwa inahitajika haraka kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya ofisi, ikiwemo mahakama ambayo haziwezi kufanya kazi bila kuwepo kwa picha ya rais.
''Ofisi mbalimbali za serikali na hasa mahakama zinapofanya kazi zake ni lazima iwepo picha ya rais na picha ya Baba wa Taifa mbele. Tunamshukru sana aliyeipiga picha hiyo, lakini sasa tumeamua kuibadilisha,'' alisema Mpenda.
Mpenda alisema picha ya sasa ambayo imepigwa na mpiga picha, Zahur Ramji ni bora kwa kuwa inaonyesha sura halisi ya Rais Kikwete.
Alisema picha hiyo itaanza kuuzwa na Idara ya Habari Maelezo kwa wizara, wakala na mashirika ya serikali kuanzia juma la kwanza la Julai, mwaka huu kwa Sh15,000 na kwamba watu binafsi wataanza kuuziwa baadaye kuwa sababu, kwa sasa wamechapisha nakala chache.
source: mwananchi