Rais Jakaya Kikwete amteua Bwana Hussein A. Kattanga kuwa Mtendaji Mkuu wa Idara ya Mahakama

Great Thinkers tufikirie Utanzania wetu na siyo dini zetu. Pia tuwaze tunafanya
nini kwa taifa letu kwa nafasi tulizonazo. Tukianza kuchunguzana dini zetu naona ni kuanza
kukosa mambo ya msingi ya kufikiria na kutenda pia.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Hussein A. Kattanga kuwa Mtendaji Mkuu wa Idara ya Mahakama kuanzia tarehe 1 Julai, 2012.

Nadhani ingesound sana kwa kusema Katibu Mkuu Idara ya Mahakama!

TUMBIRI (PhD, University of HULL - UK),
tumbiri@jamiiforums.com
 
Nimesikitishwa sana na tabia ya baadhi yaetu. Eti unamuhoji mtanzania mwenzako ni wa dini ipi. Haya ndio mambo yanayo rudisha nyuma maendeleo. Tukianza kutafutana, wengi wataumia sabau wengi katika hao wanatoka kwenye dini hiyo nyengine lakini utaifa na utendaji ndio muhimu. Tukianza udini, tutakorogana kweli kweli.

Wewe unaishi nchi gani udini ulishaanza muda sasa. Ila ni kimyakimya zaidi. Hata CCM inautumia kwenye propaganda zake.Uchaguzi wa 2010 ulikuwa Tanzania? It is amazing how we pretend to have fast ever fading short memory
 
mbinga wanamfahamu zaidi
Mbinga mbona mbali alikua mkurugenzi wa halmashauriya kinondoni,alipambana sana na genge la kina londa na mdogo wake Regina lowassa,baada lowassa akapendekeza aondolewe pale,akapelekwa kuwa RAS sijui mkoa gani nimesahau
 
Mbinga mbona mbali alikua mkurugenzi wa halmashauriya kinondoni,alipambana sana na genge la kina londa na mdogo wake Regina lowassa,baada lowassa akapendekeza aondolewe pale,akapelekwa kuwa RAS sijui mkoa gani nimesahau

aliwahi kuwa RAS mkoa wa morogoro!. kutoka Mkurugenzi wa manispaa kwenda kuwa RAS ni PROMOTION!atakuwa ametoa mchango mkubwa sana kuhakikisha wakurugenzi watendaji wa wilaya waliovuliwa madaraka,walioshushwa vyeo na waliopewa maonyo mwaka huu kuchukuliwa hatua!jamaa ni jembe
 
JK anampenda sana kattanga..alianza kama mkurugenzi manispaa ya kinondoni ..amepanda kwa kasi sana kwenye system

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Ndo maana tunataka sensa iwe na kipengele cha dini ili tujue ukweli uko wapi sio unatokwa na mapovu hapa mnajijua mpo wa chache halafu unanyanyua domo piga kimya.
Jaji mkuu, jaji kiongozi, wasajili wa mahakama, mtendaji WAISLAM
 
aliwahi kuwa RAS mkoa wa morogoro!. kutoka Mkurugenzi wa manispaa kwenda kuwa RAS ni PROMOTION!atakuwa ametoa mchango mkubwa sana kuhakikisha wakurugenzi watendaji wa wilaya waliovuliwa madaraka,walioshushwa vyeo na waliopewa maonyo mwaka huu kuchukuliwa hatua!jamaa ni jembe
Huyu jamaa ni mchapakazi makini.
 
Wadini ni sisi na si JK kwani tunamacho ya kidini, na dini zenyewe zinaishia kwenye majina tu. Watanzania tumekuwa wasanii na wavivu wa kufikiri tunataka majibu rahisi rahisi. Kama hoja hapa ni kujadili sifa za Katanga basi iwekwe CV yake humu then tujadili. Kidogo ninachokifahamu ni kuwa alikuwa Mkurugenzi Mbinga ndoo aliondoa mbinga kwenye kupata hati chafu za mkaguzi mkuu, ndoo aliyehakikisha mbinga inanunua grader. Baadaye akahamishiwa kuwa mkurugenzi Kinonondoni alikuwa mkali sana kwenye wapenda viwanja vya umma na alipambana na wakubwa wa makao then akateuliwa kuwa RAS Singida akapiga kazi vizuri then akateuliwa kwenda TAMISEMI na sasa ameenda huko. Dokezo dogo ni kuwa uteuzi unafanywa na mtu zaidi ya mmoja na rais ndiyo mwenye maamuzi ya mwisho ila kwenye kuchunguzwa ndoo kwenye kazi na sio kutangaza.
 
katanga alipokua mkurugenzi kinondoni ndie aliyenunua suzuki zote za kinondoni infact hakukuwa na vitendea kazi vingi ktk halmashauri ile mfano magari, trekta za kuzoa taka, makatapila, magari ya taka na hata ofisi, ndie alijenga masjala ile ya ardhi kinondoni, jengo la utawala kinondoni etc. kwa kweli katanga ni mchapa kazi mzuri sana, ila kwa nini mchapa kazi huyu ahamishwe hamishwe kwa nini asikae sehemu moja kwa muda mrefu ili aweze kuboresha. mfano amekaa kinondoni miaka 3 pekee
 
anayefafamu uadlifu na na C.V ya hussein katanga atupe

Ukiuliza wanafanyakazi wa Ofisi ya DED Mbinga wanaweza kukupa undani zaidi wa huu bwana. Alikuwa DED wa Mbinga miaka mingi iliyopita. Ni mwenyeji wa Kigoma-Ujiji
 
Ndo maana tunataka sensa iwe na kipengele cha dini ili tujue ukweli uko wapi sio unatokwa na mapovu hapa mnajijua mpo wa chache halafu unanyanyua domo piga kimya.

Lakini kwenye kile kitabu cha "One" Dr Njozi? cha Marginalization of Muslims in Tz, kwenye list ya wasimamizi wa Uchaguzi, huyu bwana alitajwa kama ni Mkristu! Sijui kama Mtunzi wa Kitabu kile ameshamtaka radhi Bwana HUSSEIN Katanga?
 
Back
Top Bottom