Rais Jakaya Kikwete amteua Bwana Hussein A. Kattanga kuwa Mtendaji Mkuu wa Idara ya Mahakama

kupelwa

JF-Expert Member
Aug 24, 2011
1,087
450
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Hussein A. Kattanga kuwa Mtendaji Mkuu wa Idara ya Mahakama kuanzia tarehe 1 Julai, 2012.

Uteuzi wa Bwana Kattanga ni sehemu ya utekelezaji wa Muundo Mpya wa Mahakama, na utekelezaji wa Sheria ya Uendeshaji wa Mahakama Namba 4 ya Mwaka 2011.

Sheria hii inaanzisha Kada Mpya ya Waendeshaji wa Mahakama, yaani Court of Administrators.

Hadi anateuliwa kushika wadhfa wake wa sasa, Bwana Kattanga alikuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
5 Julai, 2012
 
anayefafamu uadlifu na na C.V ya hussein katanga atupe
 
Naam, naona ile Sheria iliyozua malumbano makali Bungeni lakini badala ya nguvu ya hoja, ikapitishwa kwa "wingi" wa wabunge wa CCM imeanza kutumika rasmi. Miongoni mwa mapungufu makubwa ya sheria hii ni uhusika wa Wakuu wa Wilaya (makada wa CCM) katika utekelezaji wake. Mh. Tundu Lissu alipinga sana kwa hoja lakini ndio hivyo tena magamba hawaangalii umbali wa zaidi ya pua zao. Kazi ipo.
 
Nami nimeshangaa sana kusikia Rajab Kiravu ni msabato!ule usanii wote ule na wizi ,udanganyifu kweli ukiwa sirikalini lolote lawezekana!
 
Waziri TAMISEMI kawajibishwa, CAG ripoti katibu??? Hawajibisha anakwepeshwa na rungu la CAG!!!!
 
Nimesikitishwa sana na tabia ya baadhi yaetu. Eti unamuhoji mtanzania mwenzako ni wa dini ipi. Haya ndio mambo yanayo rudisha nyuma maendeleo. Tukianza kutafutana, wengi wataumia sabau wengi katika hao wanatoka kwenye dini hiyo nyengine lakini utaifa na utendaji ndio muhimu. Tukianza udini, tutakorogana kweli kweli.
 
Ni kweli masuala ya udini hayana nafasi siye tunachoitaji ni utendaji wa mtu na si dini yake ebu nikuulize wewe mheshimiwa unaye endekeza mambo ya ubaguzi wa kidini hivi unafaidika na mimi?
 
mh kwani si hiyo post walitangaza watu waombe?!au me ndo cjui maana walitangaza nafasi ya chief court administrator si ndio kiswahili chke hicho jamani?au mi ndo cjui kingereza?tena wakasema awe na llb orllm?mmm ngoja tuone kama ataziweza hizo protocol za,bulb imeungua yumbani kwangu chief;dio mh jaji naenda kuweka
 
Jaji mkuu jaji kiongozi msajili wa mahakama ya rufaa msajili wa mahakama kuu jaji mfawidhi kesho kadhi mkuu. Duh... masikini nchi yangu...
 
Tumekuwa minority within 5 years tuu???mhh ni mda muafaka sasa wa kuwa na majina ya dini mbili!
 
Jaji mkuu jaji kiongozi msajili wa mahakama ya rufaa msajili wa mahakama kuu jaji mfawidhi kesho kadhi mkuu. Duh... masikini nchi yangu...
Teh teh inauma eh? sasa ndio na wewe ujisikie yale machungu ambayo wenzako tumekuwa tukiyasikia tokea enzi za Nyerere!
Big up Jey Key!
 
kwa mtazamo wangu;
cha kuhuzunikia hapa si alieteuliwa ni dini gani, kwan kila siku tumekua tukisema kua uteuzi usiangalie dini bali sifa za mtu. wakristo wengi tulikua na elimu kwasababu za kihistoria, tukajaa kwenye srikali na nafas mbali mbali za uongozi kwe mashirika ya uma, sasa kama hatutaki waislam wahoji wingi wetu kuliko wao kwa kigezo kua wao hawakusoma, tusilalamike pale muislam aliesoma anapoteuliwa mana utakua unaonyesha kua wewe ndio mwenye ubaguzi wa kidini.
cha kutuhudhunisha hapa kinatakiwa kiwe ni; idara ya mahakama haiko huru kwani kila nafasi muhimu ktk uongozi wa mahakama, pamoja na majudge ni presidential appointmemnts. sasa hapa ile kanuni ya mgawanyo wa madaraka haishiki hatamu kwa kiasi kinachotakiwa na usitegemee maamuz huru dhidi ya serikali. hili athar zake haziangalii dini yako.
unaeza usielewe kama ambavyo baadhi hatuelewi mgomo wa madaktar upo au haupo mpaka yakukute
 
Back
Top Bottom