Rais j. Kikwete, Chukua Hatua kwa vikundi vya ghasia Tanzania, vifilisiwe

proisra

JF-Expert Member
Jun 14, 2012
214
158
Tanzania tokea uhuru haijawahi kushuhudia uvunjifu mkubwa wa amani na uchochezi wa mara kwa mara na makusudi kama awamu hii ya Rais JakayaKikwete. Tunakiri hili kwani kwa umri wa baadhi yetu, marais wote wa taifahili tumewashuhudia, kwa awamu zote (Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete). Ila hadisasa J.K kaweka historia ya kufumbia macho maovu yanayotendeka chini ya utawala wake.

Zanzibar, sehemu ya Jamhuri ya Muungano, kila siku ngoma za kuuvunja muungano zinapigwa na kuchezwa. Makanisa lukuki yamechomwa moto Zanzibar, chini ya utawala huu huu wa J.Kikwete… Hakuna hatua za maana zimechukuliwa.

Tanganyika (upande wa Bara), mauaji ya wananchi wasio na hatia kukabiliana na mikutano ya vyama vya upinzani yamefanyika na yanaendelea, Damu zao zinalia ardhini. Na hatutoshangaa hata ndani ya mwezi/mwaka huu tukashuhudia mauaji mengine ya raia...Hakuna hatua za maana zitachukuliwa vile vile.

Misikiti inayohubiri chuki imeongezeka, kila upande, tukiwa majumbani tunahubiriwa chuki kupitia spika za hii misikiti. Isitoshe, Radio Imann ya mjini Morogoro na magazeti ya Al-noor yanapandikiza chuki za udini kila wakati. Hakuna hatua za maana zimechukuliwa.

Mtu anashindwa kutofautisha mahubiri ya chuki yanayotolewa kwa watoto wa Kipalestina dhidi ya Israeli na mahubiri ya kiislamu ya chuki dhidi ya Wakristo hapa Tanzania…Mbagala (DSM) makanisa zaidi ya matatu yamechomwa moto juzi Ijumaa 12/10/2012. Je,isingekuwepo CHUKI, makanisa haya yangechomwa moto? Hapana. Waislamu wangekuwa wanahubiriwa UPENDO kwa jiraani zao, haya yote yangetokea? Hapana. Je, hatua za maana zimechukuliwa? Hapana.

Pale Manzese Bakhresa (Dar es Salaam), mahubiri ya kudhalilisha dini zingine (na hasa Ukristo) yanaendelea. Hakuna hatua za maana zimechukuliwa. Yamkini vipo vikundi vya wakristo vinafanya mambo haya haya ya Manzese Bakhresa (ingawa hatuna data) lakini pia hakuna hatua za maana zimechukuliwa.

Kuwa Rais na kuingia Ikulu siyo mwisho wakufikiri, kusikia wala kuona. Na wala siyo mwanzo wa kula bata tu na kusahau wajibu wako kikatiba kwa jamii iliyokupatia hiyo nafasi. Rais J. Kikwete usijisahau. kumbuka kuwa hata neno moja tu unalotamka kinywani mwako litaleta athari zipi kwa jamii tofauti yenye uelewa tofauti, itikadi tofauti, na imani tofauti (a complex society).

RaisJ. Kikwete, hatudhani kama umeshindwa hii kazi ya kutawala. Yamkini umesahau kidogo wajibu wako kikatiba. Biblia inasema hivi (If a sentence against an evil work is not executed speedily, therefore the heartof the sons of men is fully set in them to do evil…Endapo hukumu kwa watendamaovu haitolewi haraka, mioyo ya wanadamu hujaa mipango ya kutenda maovu…(Mhubiri 8:11).

Sisi siyo wasemaji wa Jumuiya za Wakristo wanaokandamizwa kwa sasa chini ya utawala wako. Tusingependa ushauri wetu kwako utafsiriwe na wapenda UDINI kama sehemu ya uchochezi. Ila tunakushauri, UCHUKUE HATUA ZA MAANA HARAKA, kabla mioyo ya hawa wanadamu haijapanga maovu. Kumbuka neno la Mhubiri 8:11 hapo juu ni la Mungu, na neno la Mungu kuna wakati litatimia. Hatua za kamata kamata ulizochukua siyo mwaraobaini. Utakamata wangapi, endapo kila kona ya Tanzania vikundi vya uchochezi vimezagaa. Je, makanisa yaliyochomwa moto yatajengwa lini na nani? Magari yaliyovunjwa je, ni nani atayakarabati?

Tunashauri iwepo sheria ambayo,wahusika wa ghasia Tanzania (wawe Waislamu, Wakristo, Polisi au Vyama vyaSiasa) wafilisiwe mali zao zote ili kufidia hasara ya uovu wanaosababisha. Tunajuahili litakuwa suluhisho la kudumu (Sustainable solution), kuliko kuweka watu ndani, huku vidonda vya uovu wao vikiwa havitibiwi haraka. Rais J.K,ukishauriwa, haijalishi ushauri mzuri kama huu umetolewa na nani, fanyia kaziushauri huo. Usivute muda ili kusubiri utoke madarakani 2015 ili atakayekurithi Ikulu ndiye apambane na mizigo hii iliyo chini yako leo. Kila mtu na kila rais atabeba mzigo wake mwenyewe. Kikwete, chukua hatua za haraka sasa.
====ChristiansUnited For Israel (C.U.F.I), Tanzania Chapter====
 
Back
Top Bottom