Elections 2010 Rais inapovunja katiba

Ngambo Ngali

JF-Expert Member
Apr 17, 2009
3,517
1,359
Ibara ya 51 ( 2 ) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema:

(2) Mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile ndani ya siku kumi na nne, baada ya kushika madaraka yake, Rais atamteua Mbunge wa kuchaguliwa kutoka katika jimbo la uchaguzi anayetokana na chama cha siasa chenye Wabunge wengi zaidi Bungeni au, kama hakuna chama cha siasa chenye Wabunge wengi zaidi, anayeelekea kuungwa mkono na Wabunge walio wengi kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, naye hatashika madaraka hayo mpaka kwanza uteuzi wake uwe umethibitishwa na Bunge kwa azimio litakaloungwa mkono na kura za Wabunge walio wengi.

Je Waziri mkuu ni mbunge wa kuchaguliwa???????
 
Pinda si mbunge wa kuchaguliwa. Ni kwamba alijaza fomu ya kugombea ubunge akakubaliwa kwa tiketi ya CCM lakini hakupiga kampeni, hakuchaguliwa na mtu yeyote isipokuwa NEC.

Siku ya kupiga kura hamna mtanzania yeyote aliyepiga kura kumchagua Pinda.

Najiuliza ni wapi kumeandikwa kwamba mtu asipopata kura hata moja ya ndio wala ya hapana, anashindaje kuwa mbunge? Hapa ilibidi waandae upya ili kupata watu wa vyama vingine ili demokrasia itekelezwe Tanzania tofauti na hapa Pinda hajachaguliwa kidemokrasia pia si mbunge wa kuchagulia.

Kwa hili kama kuna mtu anashangaa basi anieleze Pinda kapata kura ngapi kati ya ngapi sawa na % ngapi kati ya % ngapi? Yani Tz ni nchi ya ajabu.
 
Unajua wanaKijani wengi wanajipa moyo kuwa hata kama angekuwa na mpinzani lazima Mizengwe angeshinda, lakini wakati huo huo wanasahau yaliyomkuta checkibob Masha kule Nyamagana!

Rais amevunja Katiba ya nchi period! na consequences zake tunaweza tusizione leo lakini tayari imeshaingia kwenye recods na ipo siku hili ZIMWI lazima litawarudia watake wasitake...
 
Mchakato wa kuwaondoa hawa watu walioingia bungeni bila kupingwa keshauanza Mheshimiwa Mtikila kwa kuonesha nia ya kwenda mahakamani, mimi namtakia kila la heri.
 
Hilo akina Lissu walitakiwa waliseme, kama wamekaa kimya ina maana kuwa sheria imetumika so hakuna cha kulalama hapo
 
Hili swala linatakiwa kujadiliwa na ndicho kilichotokeo hata sophia simba juzi kwenye uwakilishi wa saddc aliambiwa kapita bila kupingwa.

Mzee gomezi
 
Ccm tumesha wazoea ni watu wa kupeana madaraka kihole, hebu niambie wapi katiba inaruhusu mtu kuwa Rc na mp kwa mpigo hamuoni kuwa huku ni kubebana. Hawa jamaa dawa yao iko jikoni
 
Nani ka kwambia akimna lissu ni kila kitu?nijuavyo tunaruhusiwa kuona zaidi ya pale anapoishia(mfano akina lissu)na kuueleza umma(sauti ya watu)kuhusu kosa lolote,na hili lazima tuwatonye hawa mabwana walilipue uone habari yake!
amka katika usingizi huu ndugu.
 
66
.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengine ya ibara hii, kutakuwa na aina zifuatazo za Wabunge, yaani-

(a) Wabunge waliochaguliwa kuwakilisha majimbo ya uchaguzi;

77.-(1) Wabunge wanaowakilisha majimbo ya uchaguzi watachaguliwa na wananchi kwa kufuata masharti ya Katiba hii na vile vile masharti ya sheria iliyotungwa na Bunge kwa mujibu wa Katiba hii inayoweka masharti kuhusu uchaguzi wa Wabunge wanaowakilisha majimbo ya uchaguzi.

(2) Isipokuwa pale ambapo Tume ya Uchaguzi, kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii au Sheria iliyotungwa na Bunge kwa ajili hiyo, itaagiza vinginevyo, kutachaguliwa Mbunge mmoja tu katika jimbo la uchaguzi.

Tafadhali tafuta sheria ya Uchaguzi no 4. Article 25 nadhani kuna kitu kinasema jambo... mfano kama wanasema Mbunge wa Kuchaguliwa ni yule anayetokana na jimbo la uchaguzi.... then hapo ndio mambo yalipoishia.

Tujaribu kuwa reasonable jamani,sheria inataka awe mbunge wa kuchaguliwa na wananchi hilo ni sawa.Je?inatamka idadi ya kura?manake alikuwa mgombea pekee hivyo hata angepata kura za hapana nyingi zaidi wangemkataa wamweke nani? ni wazi katika hali yoyote angekuwa mbunge.Kikubwa hapa kilichozingatiwa na kutopoteza fedha bure kwa kitu ambacho majibu yake yalishathibitika kuendana na mazingira yaliyopo.Tuwapinge ccm wanapokosea lakini si kwamba kila kitu tukatae huo utakuwa ujinga wa kupitiliza na haitatusaidia chochote katika taifa hili.
 
To Be reasonable ni KATIBA Ibadirishwe nadhani utakubaliana nami ili kuondoa Utata huu na ndio maana huwa twajadili ilikuwepo na Democrasia isiyo wayumbisha watu kwa hili na lile na linalotoke huko Bungeni ni wazi kuwa KATIBA yetu inatukanganya sana

Katiba ya Tanzania ni utata mtupu. Zamani watu walikuwa hawasome Katiba hivyo viongozi walikuwa wanafanya wanavyotaka kwa sababu hakuna aliyekuwa akihoji. Sasa watu wanasoma na kuhoji kasoro zake. Muda si mrefu itabadilisha tu watake wasitake.
 
Waziri mkuu si mbunge wa kuchaguliwa period. Yeye ni Mbunge wa kuteuliwa na Chama. Bisheni kwa kuwa mnafursa ya kufanya hivyo. Hapo katiba imevunjwa.jamani. Katiba haizungumzi defaults-kupita bila kupingwa. Hapa kuna shida kubwa sana ktk kutafsiri katiba hasa mtu akiwa na altitude za cha kimoja.
 
Tujaribu kuwa reasonable jamani,sheria inataka awe mbunge wa kuchaguliwa na wananchi hilo ni sawa.Je?inatamka idadi ya kura?manake alikuwa mgombea pekee hivyo hata angepata kura za hapana nyingi zaidi wangemkataa wamweke nani? ni wazi katika hali yoyote angekuwa mbunge.Kikubwa hapa kilichozingatiwa na kutopoteza fedha bure kwa kitu ambacho majibu yake yalishathibitika kuendana na mazingira yaliyopo.Tuwapinge ccm wanapokosea lakini si kwamba kila kitu tukatae huo utakuwa ujinga wa kupitiliza na haitatusaidia chochote katika taifa hili.

Naomba niwe kinyume na wewe.

Pinda alipitishwa na chama chake kugombea nafasi ya ubunge, na since hakuwa na mpinzani, I think NEC wao wangetimiza sheria ya kumweka kwenye karatasi ya ubunge jina lake peke yake na wananchi siku ya kupiga kura wapige kura za kumthibitisha.

Uzuri ni kwamba once you are alone unauhakika wa kupita, kwani mpiga kura ana'choice moja tu ya kuweka tick kwa mgombea, kama hayupo anaemtaka ataacha, means atakuwa ameshinda at any idadi ya kura atakazopata, (maana kwa hapo kutakuwa na kura safi walioweka tick, atakayeweka kosa au otherwise itakuwa kura iliyoharibika) lakini sheria ingekuwa imetimizwa na sio kutuwekea wabunge waliochaguliwa na chama (NEC)
 
Back
Top Bottom