Zanzibar 2020 Rais Hussein Mwinyi: Niko tayari kufanya maridhiano na vyama vingine

Mazrui kakutwa katika process ya kuhujumu ushindi 'matokeo' wa Hussein Mwinyi

Angefanikiwa labda Hussein Mwinyi asingekiwa Rais sasa mtu wa namna hiyo anasamehewaje!?!

Hakuna kuachiwa ova.
Hizo ni story ambazo unanakiwa uwaambie Darasa la saba
Hakuna uchaguzi hujuma zitoke wapi

Tume ya CCM Ndio yenye mamlaka ya kutangaza takwimu ambazo zilitayarishwa sasa utahujumu nini

Au wanakudaganya aliwarubuni tume CCM?

Anyway kuna watu bongo lala sana Dunia hii
 
Mazrui kakutwa katika process ya kuhujumu ushindi 'matokeo' wa Hussein Mwinyi

Angefanikiwa labda Hussein Mwinyi asingekiwa rais sasa mtu wa namna hiyo anasamehewaje!?!

Hakuna kuachiwa ova.
Kuhujumu kivipi?sasa imekuwa kuhujumu sio kesi ya kigaidi tena!?

Mbona wale waliokutikana na kura feki zilizokuwa zimeshapigwa na mihuri ya ZEC na NEC hamjawakata na kuwafungulia kesi?

Acheni kuonea raia kwa kuwabambikizia kesi za uongo

Free Mazrui and all Political prisoners
 
HABARI: Ninaheshimu maridhiano na matakwa ya Katiba ya kushirikiana na vyama vingine vya siasa katika kuendesha Serikali. Niko tayari kuyatekeleza maridhano kama Katiba ya Zanizbar inavyoeleza - Dk. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar #MwanaHALISIDigital.

View attachment 1624518
Maridhiano gani tena?
Wamesema uchaguzi ulikuwa huru na wa haki, na yeye kachaguliwa kwa kishindo kihalali.
Shida iko wapi?
 
Hussein, Allah hawafanyi madhalimu kuwa ni wenye kufaulu

Mmeiba uchaguzi, Mmetesa watu, Mmeua watu, Unataka maridhiano gani zaidi ya Haki? .

Hussein, Allah yupo na anaona mliyoyafanya na mtalipwa kwa dhulma mliyotenda.

Wewe tawala tu lakini ufalme huwa una kikomo, ipo siku hautokikalia hicho kiti na utaulizwa kwa damu isiyo na hatia mliyomwaga huko Zanzibar!
 
HABARI: Ninaheshimu maridhiano na matakwa ya Katiba ya kushirikiana na vyama vingine vya siasa katika kuendesha Serikali. Niko tayari kuyatekeleza maridhano kama Katiba ya Zanizbar inavyoeleza - Dk. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar #MwanaHALISIDigital.
=====================

KUMBUKUMBU.

Baada ya uchaguzi wa Zanzibar wa 2015 kufutwa Marekani kupitia shirika lake la misaada la Millennium Challenge Corporation (MCC) ilizuia pesa za mradi wa kupeleka umeme Zanzibar kiasi cha $472m karibu Tshs. Trn. 1. nafikiri hili somo kaliona Rais Mwinyi ndio maana anataka maridhiano.

Maridhiano anayataka kwa anavyoendeleza mauwaji namna hii

mauwaji  ya wapinzani zanzibar.jpeg
 
HABARI: Ninaheshimu maridhiano na matakwa ya Katiba ya kushirikiana na vyama vingine vya siasa katika kuendesha Serikali. Niko tayari kuyatekeleza maridhano kama Katiba ya Zanizbar inavyoeleza - Dk. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar #MwanaHALISIDigital.
=====================

KUMBUKUMBU.

Baada ya uchaguzi wa Zanzibar wa 2015 kufutwa Marekani kupitia shirika lake la misaada la Millennium Challenge Corporation (MCC) ilizuia pesa za mradi wa kupeleka umeme Zanzibar kiasi cha $472m karibu Tshs. Trn. 1. nafikiri hili somo kaliona Rais Mwinyi ndio maana anataka maridhiano.

Haya mambo ya maridhiano ni uhuni mtupu. Yaani unaiba kwanza halafu uanatafuta maridhiano.

Kama ni kweli yuko serious akubali kuunda tume huru ya uchaguzi halafu warudie uchaguzi.
 
Mazrui kakutwa katika process ya kuhujumu ushindi 'matokeo' wa Hussein Mwinyi

Angefanikiwa labda Hussein Mwinyi asingekiwa Rais sasa mtu wa namna hiyo anasamehewaje!?!

Hakuna kuachiwa ova.
Hakuna MARIDHIANO pia ova
 
Hakuna cha uchunguzi wala nini

Nani aliwaambia waandamane na kufanya vurugu

Ebo!, uvunje sherie mwenyewe, janga likupate, halafu lawama ziwaendee wengine

Wangelitii sheria na mamlaka yasingeliwakuta ova.
Kuandamana ni haki zao kikatiba, Polisi kupiga na kuuwa watu wasio kuwa na silaha ni uvunjifu wa haki za Binaadamu

Wewe na wenzako kama wewe lazima mfurahie haya yanayoyokea Tanzania

Watu kuuliwa,kuteswa,kupotea,kwenu ni sawa Tu,Mmelelewa Kwa vichapo na kupewa adhabu kila ukifanya Kosa

Mnaendeleza yale mliofanyiwa na wazazi wenu,mnaamini kuwa ujumbe haunifiki mlegwa mpaka aadhibiwe..

Unajifanya ova,ova Kwani unaongea na Walkie talkie ya Polisi!!?

Kwani nchi nyengine Watu hawapigi kura,hawaandamani mbona hatusikii vifo na mauaji

Wewe ni mfano mzuri wa Mwafrika chini ya Jangwa la Sahara,

Mzee wako kafikisha ujumbe kwako kwa malezi ya vichapo na mateso,na wewe unaona ujumbe ufikishwe Kwa vitisho na maauaji kwa raia wema wasio na hatia
 
Kwanza Akafanye maridhiano na ndugu wa marehemu waliouawa na majeshi waliyoyapeleka Zanzibar kuua raia
 
Wabunge wa ACT Walienguliwa enguliwa,wamewafanyia dhulma kabla ya Uchaguzi

Hata hayo maridhiano yakifanyika,Act watakuwa hawana waakilishi wala Wabunge kwenye Baraza la Waakilishi na Bunge la Tanzania..

Au wanataka Seif akae peke yake kwenye hayo mabaraza kama kinyago wamkejeli?
 
HABARI: Ninaheshimu maridhiano na matakwa ya Katiba ya kushirikiana na vyama vingine vya siasa katika kuendesha Serikali. Niko tayari kuyatekeleza maridhano kama Katiba ya Zanizbar inavyoeleza - Dk. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar #MwanaHALISIDigital.
=====================

KUMBUKUMBU.

Baada ya uchaguzi wa Zanzibar wa 2015 kufutwa Marekani kupitia shirika lake la misaada la Millennium Challenge Corporation (MCC) ilizuia pesa za mradi wa kupeleka umeme Zanzibar kiasi cha $472m karibu Tshs. Trn. 1. nafikiri hili somo kaliona Rais Mwinyi ndio maana anataka maridhiano.

Rais Mwinyi ajue mambo mawili muhimu, mosi CCM haiko chini yake na pili yeye hapo ni Rais wa Zanzibar yupo chini ya Rais wa Tanzania ambaye ni mwenyekiti wa CCM iliyompa ridhaa ya kugombea hivyo hana madaraka ya kufanya maridhiano bila ya kuruhusiwa na CCM ambayo ndiyo iliyopanga matokeo ya uchaguzi. Ninaamini hakuna atakayeungana naye kwa kuwa naye ni mtoto yuko chini ya baba, hivyo ni baba ndiye mwenye uamuzi huo wa kuomba ushirikiano.
 
HABARI: Ninaheshimu maridhiano na matakwa ya Katiba ya kushirikiana na vyama vingine vya siasa katika kuendesha Serikali. Niko tayari kuyatekeleza maridhano kama Katiba ya Zanizbar inavyoeleza - Dk. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar #MwanaHALISIDigital.
=====================

KUMBUKUMBU.

Baada ya uchaguzi wa Zanzibar wa 2015 kufutwa Marekani kupitia shirika lake la misaada la Millennium Challenge Corporation (MCC) ilizuia pesa za mradi wa kupeleka umeme Zanzibar kiasi cha $472m karibu Tshs. Trn. 1. nafikiri hili somo kaliona Rais Mwinyi ndio maana anataka maridhiano.

NO!!!! Hakuna maridhiano yeyote yale mara hii mpaka pale CCM watakapokubali kuwashitaki wale wote waliowaua ndugu zetu na waliotuma kufanya hivyo. Yaani mauaji hadi sasa yanaendelea visiwani, watu wanatekwa usiku usiku na kupewa kichapo cha mbwa, halafu mnataka maridhiano?

Pia Mwinyi amesahau kuwa huko nyuma alisema, hayuko tayari kuwa rais kwa kura ya kuiba? Sasa ni nini kilichomfanya abadilike?
 
Hakuna cha uchunguzi wala nini

Nani aliwaambia waandamane na kufanya vurugu

Ebo!, uvunje sherie mwenyewe, janga likupate, halafu lawama ziwaendee wengine

Wangelitii sheria na mamlaka yasingeliwakuta ova.
Ewe Mola tumekukosa nini hata ukatuletea watu wenye mentality kama ya huyu? Kwa Namna hii hivi kweli Tanzania tutakwamuka hapa?

Hivi wewe umeona wapi kuwa polisi ndie muendesha mashitaka na hakimu? Polisi kazi yake sio kupiga au kuua, kazi yake ni kukamata wanaofanya makosa na kuwafiksha mahakamani ili waadhibiwe. Leo hii polisi wanarusha risasi kama pipi halafu wewe unashangiria? Ngoja ije siku ndugu yako au jamaa yako auliwe kwa namna yeyote ile iwe na majambazi, askari au ajali ya gari halafu jirani zako washangirie ndio utaona raha ya kufiliwa.
 
HABARI: Ninaheshimu maridhiano na matakwa ya Katiba ya kushirikiana na vyama vingine vya siasa katika kuendesha Serikali. Niko tayari kuyatekeleza maridhano kama Katiba ya Zanizbar inavyoeleza - Dk. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar #MwanaHALISIDigital.
=====================

KUMBUKUMBU.

Baada ya uchaguzi wa Zanzibar wa 2015 kufutwa Marekani kupitia shirika lake la misaada la Millennium Challenge Corporation (MCC) ilizuia pesa za mradi wa kupeleka umeme Zanzibar kiasi cha $472m karibu Tshs. Trn. 1. nafikiri hili somo kaliona Rais Mwinyi ndio maana anataka maridhiano.

Si amependa urais uliopatikana kwa kumwaga damu , aendelee nao tu , sigida ya buree ndani maibilisi watupu .
 
Back
Top Bottom