Rais hukuahidi tetemeko, Laptop je?

Dumelang

JF-Expert Member
Aug 11, 2011
3,203
5,704
Hivi karibuni Rais mpendwa na mtukufu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania aliwambia Wananchi na wakazi wa Bukoba waliokumbwa na tetemeko la ardhi kuwa serikali haitawajengea nyumba kwakuwa haikuleta tetemeko

Akisisitiza msimamo wake huyo rais aliwauliza wananchi "Nilipokuja kuomba kura nilisema nitaleta tetemeko?" akaongeza "nilisema nitalileta?"

Pitia link hii kuanzia dakika ya 14:31


Bila shaka jibu ni hapana, kumbe Raisi anatekeleza alichoahidi tu, sasa mimi leo na mkumbusha Mh Rais hukusema utaleta tetemeko lakini Laptop za Walimu ulisema utaleta.

Kwa maneno mepesi kabisa tunaomba laptop za walimu maana hizi ulisema utaleta.

Pitia ahadi yake hapa
Magufuli na mradi wa laptop kwa kila mwalimu,hivi tatizo ni ukosefu wa laptops?

Pia August 12 gazeti la raia mwema liliandika
6e9630326d89c78cb852e814abf6b942.jpg
 
Kuna watu wengine ni watu wazima kabisa lakini wanatabia za kitoto! Kama mleta mada!
 
Aliahidi tufyatue watoto wengi kwa sababu elimu ni bure
Elimu bure wapi mkuu wameshindwa ndio maana sasa hivi hawaongelei hili, now wazazi wanapeleka maharage na mahindi shuleni maana watoto wanateseka na njaa, amebadili badala ya kupeleka fedha wanapeleka chakula inabidi ukinunue upeleke sasa hapo bure iko wapi? Jamaa amekuja na mambo ya kale kweli now ni mwendo wa biashara ya kubadilishana bidhaa kama enzi za kale.
 
Walimu Wangu nawapenda sana. Mkipata laptops naomba mnisitue nipo nchi za wenzetu.
 
kila mtu abebe msalaba wake mwenyewe!!! mniombee jamani urais ni mzigo kweri kweri!!!!
 
Kuna watu wengine ni watu wazima kabisa lakini wanatabia za kitoto! Kama mleta mada!

NDUGU KUMBUKA AHADI NI DENI. KULIPA NI MUHIMU. MLETA MADA AMEJARIBU KUMKUMBUSHA KUHUSU AHADI YAKE YA LAPTOP. HUENDA MLETA MADA NI MWALIMU HIVYO ANASUBIRI KWA ZAIDI YA MWAKA SASA HAJAONA HATA POWER CABLE YA LAPTOP.
 
Tofautisha kampeni na ku run nchi!

so its ok tu lie kwa sababu ni kampen? kama kampen unaweza ongea tu hata kama hutakuja tekeleza kuna haja gani ya kupoteza pesa za walipakodi kuendesha kampen tume ya uchaguz basi isingekua inatoa ela za kampen iwe inaaandaa uchaguz tu watu wajichagulie wanachotaka maana kampen si muhim unaonaje iyo?
 
so its ok tu lie kwa sababu ni kampen? kama kampen unaweza ongea tu hata kama hutakuja tekeleza kuna haja gani ya kupoteza pesa za walipakodi kuendesha kampen tume ya uchaguz basi isingekua inatoa ela za kampen iwe inaaandaa uchaguz tu watu wajichagulie wanachotaka maana kampen si muhim unaonaje iyo?

think beyond my sentence!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom