Rais hakukosea kuwateua wabunge na hapohapo kuwapa Uwaziri. Wameapa tena leo. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais hakukosea kuwateua wabunge na hapohapo kuwapa Uwaziri. Wameapa tena leo.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nikupateje, Jun 12, 2012.

 1. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #1
  Jun 12, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Ujue ukweli wa kiapo cha mbunge, waziri

  MWEZI uliopita ulizuka ubishi magazetini na kwenye vyombo mbalimbali vya mawasiliano ukihoji mantiki ya mbunge kuapa na kuanza uwaziri kabla hajaapa ubunge. Sina hakika kama ubishi ule sasa utahamia bungeni kujadili viapo vile.
  Naanza kufafanua ninavyoelewa kwa kueleza historia ya ubunge.

  Mfumo wa sasa wa Bunge uliundwa na kusimikwa na Simon De Montfort, tajiri aliyeitawala Uingereza kimabavu kwa muda.

  Kabla yake, wafalme wa nchi hiyo walizoea kuwaita kwa msimu matajiri wa kwenye jamii (Lords) ili kusikia taarifa na ushauri wao.

  De Montfort alipochukua madaraka, alibadili mtindo huo. Januari 20, 1265 aliwaita matajiri (Lords) lakini pia akaamua kila eneo lichague watakaokuja kuwawakilisha masikini (Commons).

  De Montfort alifanya hivyo ili apendwe kuepusha chuki dhidi ya kitendo chake cha kumuondoa madarakani mfalme halali yaani Henry III.

  Mfumo aliousimika De Montfort, japo ulirikebishwa kidogo, umedumu hadi leo. Ni mfumo wa Bunge kuwa na mikusanyiko miwili. Mkusanyiko wa kwanza umeendelea kujumuisha wanaoteuliwa na mfalme au malkia, ukijulikana kama "Upper House".

  Mkusanyiko wa pili ni wa watu waliochaguliwa na wananchi. Mkusanyiko huu huitwa "Lower House".
  "Lower House" inajulikana kwa majina kadhaa kama vile House of Commons (Uingereza), Bundestag (Ujerumani), House of Representatives (Marekani).

  Wakati "Upper House" ina majina yafuatayo: House of Lords (Uingereza), Bundesrat (Ujerumani) na Senate (Marekani).
  Mikusanyiko yote miwili kwa pamoja ndiyo huitwa Bunge (Parliament). Mtindo huu wa Bunge kuwa na mikusanyiko miwili huitwa "Bicameral". Wakati mataifa yenye Bunge lenye mkusanyiko mmoja huitwa "Unicameral".

  Je, sisi tuna mabunge mawili (Bicameral) au moja (Unicameral)? Ni rahisi kujibu kuwa tuna Bunge la mkusanyiko mmoja tu, yaani ule wa kina John Mnyika, Anne Makinda na wenzao (National Assembly).

  Lakini katiba haisemi hivyo. Katiba inasema kwamba yenyewe haikutungwa na Bunge kama hili, bali imetungwa bunge jingine tunaloliita "Bunge Maalumu," au (Constituency Assembly).
  Hivyo, katiba imetaja mabunge mawili, yaani "Bunge Maalum" (Constituency Assembly) na Bunge la Jamhuri (National Assembly).

  Wanaosita kutamka kwamba tuna mabunge mawili (Bicameral), inabidi wasaidie kufafanua sababu zao kwani binafsi sioni ibara ya Katiba inayoonyesha kuwa lile "Bunge Maalumu" limefutwa.
  Haitofautiani na kudhani kwamba Tanzania haina Mahakama Maalumu ya Katiba kwa sababu hatujawahi kuiona ikifanya kazi, wakati imetajwa kwenye ibara ya 125 hadi 128 ya Katiba.

  Ni vizuri kueleza matukio yaliyotokea England Machi 2, 1629 na Januari 5, 1642 wakati wa utawala wa Mfalme Charles I wa England.

  Machi 2, 1629, Charles I alinuia kuvunja bunge kwa sababu alishachoshwa na ubishi wabunge kubishia matakwa yake hasa matumizi ya pesa. Mtumishi wa mfalme ambaye hadi sasa anaitwa "Black Rod" akatumwa kuwafikishia wabunge taarifa hiyo.

  Wabunge wa kikundi cha John Eliot walijua mtumishi sasa anakuja kuwaita ili bunge livunjwe. Wakajua Spika kwa woga wake akitoka kitini basi maamuzi yao yatakuwa batili yaani hakuna Bunge.

  Hivyo, wabunge wakagawana majukumu. Wengine wakaenda kuubamiza mlango mbele ya yule mtumishi ili asiingie, na wengine wakakimbia hadi kwa Spika wakamshika kwa nguvu asiinuke kitini.

  Mlango ukiwa umefungwa na Spika akiwa amebanwa pale kitini wenzao wakatumia mwanya huo kupitisha maazimio matatu waliyoyataka, kisha wakamwachia Spika wakatawanyika.

  Januari 5, 1642 hali ikuwa ni tofauti, kwani Charles I hakutaka kuishia kumtuma mtumishi, bali pia aliamua sasa aingie kwa nguvu bungeni kuwakamata wabunge watano ambao ni vinara wa ubishi hasa John Pym.

  Mtumishi wake alipofika mlangoni wabunge wakaubamiza lakini askari wa mfalme wakagonga na kuingia kwa nguvu. Charles I hakufanikiwa kuwakamata John Pym na wenzake kwani walishatoroka.

  Kitendo cha Charles I kuvamia bungeni na kuvunja uhuru wa Bunge kilisababisha Waingereza wapigane vita vya wenyewe kwa wenyewe yaani askari wa Bunge na wa Mfalme.

  Lakini kiliifanya hiyo Januari 5, 1642 iwe ndiyo siku ya mwisho kwa mfalme au malkia wa Uingereza kukanyaga kwenye mkusanyiko wa House of Commons. Hotuba za uzinduzi wa Bunge za malkia au mfalme huzitoa akiwa House of Lords.

  Kitendo cha kuubamiza mlango hurudiwa hadi leo kila mara wabunge wanapoitwa kumsikiliza Mfalme au Malkia kule House of Lords. Waweza kukishuhudia kikifanywa mbele ya malkia Elizabeth II mwaka 2008 kwenye tovuti hii (www.youtube.com/watch?v=h1bJ8nY2pcc).

  Kwanini kitendo cha kuubamiza mlango mbele ya mtumishi wa mfalme kinaadhimishwa kwa miaka 383 sasa.
  Maana yake ni kwamba Bunge liko juu ya kila mtu hata kwa mkuu wa nchi yaani Mfalme au Malkia.

  Hivyo, ni kazi ya Mkuu wa nchi kuwabembeleza wabunge kufungua mlango tena mara tatu ndipo awaombe kwa heshima na taadhima kuja kujiunga na wenzao kumsikiliza.

  Hapa nchini, yapo mengi yanayohitajika ili mkusanyiko uwe ni kikao halali cha bunge. Ibara ya 146(2) ya Kanuni za Bunge inamtaka Spika avae joho lenye bendera ya Taifa akiwa kwenye shughuli za Bunge.

  "Siwa" ni lile rungu linalobebwa na askari anayeongoza msafara wa Spika kuingia Bungeni. Hii "Siwa" ni ishara ya mamlaka ya Bunge.

  "Siwa" isipokuwepo, basi mamlaka ya Bunge yanakosekana kwenye mkusanyiko uliokuwapo. Vikao vya kamati za Bunge hufanywa bila "Siwa". Hivyo Kamati hizo si shughuli ya Bunge.

  Nimerudia maneno "Shughuli za Bunge" hivyo nalazimika kuyafafanua. Ibara ya 89(2) ya Katiba inasema "Shughuli za Bunge" ni zile za ndani ya Bunge tu, na wala si za kamati, si za kamati ndogo wala si zile za Ofisi ya Bunge.

  Maneno haya "Shughuli za Bunge" yanajirudia tena kwenye Ibara ya 68 inayomtaka mbunge kuapa kabla ya kuanza kushiriki "Shughuli za Bunge".

  Kwa mamlaka ya ibara ya 46A ya Katiba, Bunge lina uwezo wa kumshitaki Rais aliyeko madarakani. Utaratibu wa kumshtaki Rais unamtaka Spika kuunda Kamati Maalumu ya Uchunguzi wa Mashtaka dhidi ya Rais (Ib. 46A(4)). Mwenyekiti wa Kamati hii ni Jaji Mkuu wa Tanzania, na mjumbe mmoja ni Jaji Mkuu wa Zanzibar.

  Kitendo cha Kamati ya Bunge kuongozwa na Jaji Mkuu, ni mfano mzuri kuonyesha kwamba Kamati si "Shughuli ya Bunge" na inaweza kuhudhuriwa na hata kuongozwa na asiye mbunge.

  Sasa tujadili aina mbili za viapo yaani Kiapo cha Uaminifu na Kiapo cha Ofisi. Viongozi wakuu wa mihimili ile mitatu Bunge, Serikali na Mahakama huapa viapo vyote viwili wanapokabidhiwa zao. Inaelekea kwamba kile kinachoitwa Kiapo cha ofisi katiba haikitamki kama Kiapo cha ofisi. Badala yake yapo maneno mengi yasemayo (Kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake).

  Wingi wa maneno haya umewachanganya hata wataalam hadi kusema labda hicho 'Kiapo kingine' ndicho kile mawaziri wanachotakiwa kuapa siku wanayoingia Bungeni. Kwa kudhani hivyo hisia zilionekana zikihoji kwamba inawezekana ilikuwa ni makosa kuwaapisha wabunge kuwa mawaziri kabla ya hicho kiapo kingine.

  Je, mtu anakuwa mbunge siku anapotangazwa au siku anapoapa? Mbunge akishatangazwa tayari ni mbunge, maana hakuna wa kutugeuza tusimpende.

  Lakini, sheria yaani katiba inamfanya kuapa kwake bungeni kumpatie uhalali wa kushiriki "Shughuli za Bunge".
  Je, kwani lazima mbunge aende bungeni Dodoma? Mbona anaweza kubaki jimboni akawa anachimba visima au akanunua magari ya zahanati au akajenga shule kwa wanajimbo wake?

  Tumeona kwamba shughuli inayofanyika bila lile rungu la Spika, si "Shughuli ya Bunge". Kitendo cha mbunge kununua gari la zahanati au kusomesha yatima ni uhisani kama uhisani wowote. Si "Shughuli ya Bunge" kikatiba wala kihistoria duniani.

  Mbunge akiendelea na huo uhisani wake, tena hata akadiriki kuigharimikia bajeti ya nchi nzima lakini asikanyage bungeni kwa mikutano mitatu mfululizo, basi atapoteza ubunge wake kwa uzembe yaani utoro kama walivyodai Zitto alipoanza kutosaini fomu za mahudurio bungeni.

  Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Jaji Mkuu, Spika, Mbunge wote hawa wanaapa kiapo cha uaminifu kwa sababu wanautumikia umma kwa nyadhifa walizokabidhiwa.

  Kwa nini mtu akiteuliwa kuwa Waziri anaapa tena kiapo cha uaminifu pale Ikulu wakati alishaapa bungeni?
  Bungeni, mbunge anautumikia umma kwenye mhimili mmoja (Legislature). Wizarani, waziri anautumikia umma kwenye mhimili mwingine (Executive). Kule Mahakamani Jaji Mkuu anautumikia umma kwenye mhimili wa tatu (Judiciary).

  Hivyo, mawaziri wale walioteuliwa hivi karibuni ubunge na uwaziri ndani ya saa 24 waliapa kiapo cha uaminifu, ili wautumikiea umma kwenye mhimili wa utendaji, yaani ule uwaziri wake.

  Hivyo, tuwatarajie kuanzia keshokutwa waape kiapo cha uaminifu, lakini sasa kwenye mhimili wa uwakilishi.
  Kwa nini mbunge haapi mara mbili pale bungeni kama Spika? Wala si kama Spika tu. Viongozi wakuu wengi wa ile mihimili mitatu huapa viapo hivi viwili.

  Kwa nini sasa mbunge haapi kiapo cha ofisi? Kwani hana ofisi? Katiba imetaja majukumu ya viongozi watano : Rais (Ibara. 33-37), Makamu wa Rais (Ibara. 47-48), Waziri Mkuu (Ibara. 52), Waziri (Ibara. 58), Jaji Mkuu (Ibara. 119)}.
  Katika ibara zote hizo 40, hakuna hata moja inayotaja majukumu au madaraka ya Mbunge. Badala yake, ibara ya 63 na 64 imetaja na kufafanua majukumu ya mkusanyiko mzima unaoitwa Bunge.

  Kumbe, kila kinachotamkwa au kuulizwa au kuamriwa mle bungeni, kikipita bila kipingamizi basi katiba inatufundisha tutamke kwamba ("...Bunge limesema hivi...") au ("...Bunge limeazimia hivi..."). Katiba inatufundisha hivyo hata kama mzungumzaji mkuu alikuwa ni mmoja tu kati ya wabunge wote zaidi ya 350.

  Kwa maelezo haya mle bungeni panatakiwa uangalifu wa hali ya juu, kwani yanayojadiliwa, yanayoulizwa, yanayoamriwa pale ni ya bunge zima. Kama ni mafanikio yanakuwa ya Bunge zima. Kama ni lawama litupiwe Bunge zima.

  Nawatakia heri wabunge wapya watakaoapa siku yoyote kuanzia keshokutwa. Pia nalitakia heri Bunge zima katika mjadala mzima wa bajeti.

  *********************

  Source: Tanzania Daima
  Date: June 10, 2010 (Sunday)
  Website: http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=36836
   
 2. Paw

  Paw Content Manager Staff Member

  #2
  Jun 12, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 2,032
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Nimesoma kwa kusaka elimu mpya hapo.
  Nachelea kukuamini maana unataka tuamini kwamba shughuli za Bunge ni zile ulizofafanua wewe na si zilizoainishwa kwenye mkusanyiko wa Ibara za Katiba.

  Ni kweli Ibara za 63 pamoja na ile ya 64 zimeainisha madaraka ya Bunge ambayo ndiyo kwa tafsiri sahihi yanatengeneza shughuli zote za Bunge.

  Inaposemwa Kuisimamia na kuishauri serikali Ibara 64 (2), (3) ni wazi kwamba Bunge limetumia Ibara ya 89 (1), (2) (ambayo umejitahidi kuipotosha) kutunga sheria (kanuni za kudumu) namna ya kutekeleza hayo madaraka. Labda Katiba niliyosoma mimi imechapwa kwa makosa ya kisarufi... Nanukuu Ibara ya 89
  , Hivyo katika kutekeleza madaraka yake Bunge limeweka kanuni za kudumu zinazoweka maelekezo jinsi ya ushiriki na mipaka ya Wabunge kutekeleza Ibara za 63 na 64.

  Hivyo ni wazi kwamba Uwaziri ni kazi inayohusu utekelezaji wa maazimio ya Bunge ambapo kikatiba Waziri ni LAZIMA atokane na WABUNGE. na mbunge yeyote anahuishwa kwa KIAPO kabla ya kushiriki shughuli za Bunge. hili tunaliona kwenye Ibara ya 68 ya Katiba kama ninavyonukuu hapa
  Hapo kwenyer bold ni exception (nafuu) yake. Hivyo shughuli pekee ya mbunge mteule anayoruhusiwa kuifanya ni kumchagua Spika pekee ambaye baadaye wabunge watakuja kuapa kwake. Naamini wadau wanafahamu nini maana na aina ya wabunge wa Bunge letu la jamhuri ambapo hakuna mahala popote kwenye katiba, Sheria hata kanuni panapoelekeza kwamba aina fulani ya wabunge wataanza mjukumu yao ya kibunge MARA MOJA! bila ya kuapa kwanza.

  Ni wazi kwenye suala la Mawaziri kuapishwa na kuanza kushiriki shughuli za Bunge ni ukiukwaji wa Katiba.


  Nimewajibika kuliweka sawa hili kwa mtazamo wangu na uelewa wangu kwa kuwa katika maongozi au utawala aina yeyote ni budi kuwa makini na uangalifu wa hali ya juu kutekeleza makubaliano ya pamoja (Katiba, Sheria na kanuni) kwa manufaa ya walio wengi....
   
 3. S

  SubiriJibu JF-Expert Member

  #3
  Jun 12, 2012
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 1,124
  Likes Received: 776
  Trophy Points: 280
  Kama wewe umesoma na wengine tumesoma. Ungekuwa mtetezi wa ukweli usingeficha facts kadhaa. Hukuongelea kabisa kuhusu Jaji Mkuu na Jaji wa Zanzibar kuongoza kamati ya Bunge kwa maana ya kwamba wao si wabunge na hivyo Kamati si kazi ya Bunge.

  Kazi ya Bunge ni ile ambayo mace ipo mbele ya kila mmoja. Mace ni fimbo ambayo mwandishi kaieleza kwamba inaitwa "Siwa".

  Soma vizuri katiba na changia kila hoja iliyoletwa usiache zingine ili ku-tune maana yako.
   
 4. K

  Kisanduku Member

  #4
  Jun 12, 2012
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huhitaji kuapa kufanya shughuli yoyote kama kwenda ofisini kwa Spika. Huhitaji kuapa ili kushiriki Kamati ya Bunge.

  Unahitaji kuapa kusimama mbele ya "mace" maana hiyo ndiyo shughuli pekee ya Bunge na inafanyikia Bungeni tu huku Spika akiwa na joho lake.

  Kama "mace" haipo basi hiyo si shughuli ya Bunge na haina mamlaka ya Kibunge. Ndiyo maana hata uchaguzi wa kumchagua Spika huitwa kamati ya uchaguzi wa SPika.

  Kamati ni kamati haiwi bunge ata siku moja. Tumeona Kamati zikifanyia kazi zake hata nje ya nchi. Tumeona kamati ya Lowasa ikienda hadi Japan. TUliona Kamati ya RICHMOND ikisafiri hadi Marekani.

  Kazi ya Kamati ni kurahisisha mjadala itakapoleta taarifa pale Bungeni wakati "mace" ikiwepo.

  NIlipoacha hoi ni kutambua kwamba kumbe kuna kamati za Bunge zinaweza kuongozwa na hata wasio wabunge. Jaji Mkuu kuongoza Kamati ya Bunge inatosha kumaliza ubishi huu.

  Kumbuka Jaji Mkuu ni mtu wa Mhimili mwingine kabisa yaani hayumo serikali wala hayumo Bungeni. Lakini anakuwa mwenyekiti wa Kamati. Sikuwa nafahama hilo na niliposoma nilishani tumedanganyw aikabidi nihakikishe ndani ya katiba.

  Hizi ndizo subject tunazotakiwa tujadili humu JF.
   
 5. K

  Kisanduku Member

  #5
  Jun 12, 2012
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katiba ibara ya 89 (1) inasema hivi:
  Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii Bunge laweza kutunga Kanuni za Kudumu kwa ajili ya kuweka utaratibu wa kutekeleza shughuli zake.
  ********

  Ni kweli bunge linaweza kuweka utaratbu wa kutimiza shughuli zake. Kumbuka kwamba utaratibu inaouweka si lazima uwe wa ndani ya vikao vya Bunge ambazo ndizo shughuli za Bunge.

  Utaratibu kuwekwa na Bunge si lazima uwe shughuli ya Bunge wakati wa kuukamilisha.

  Hata ikiwa vipi, mwiho wa siku huo unaouita utaratibu hauwezi kuishi huko nje. Ni lazima uletwe kama hoja Bungeni ujadiliwe na Bunge zima na huo mjadala ndiy shughuli ya Bunge kwa sababu yupo Spika kavaa joho, quoram ya wabunge imetimia na kikubwa kuliko yote "mace" ipo kuonyesh kwamba kinachofanyika ni shughuli ya Bunge na ina mamlaka ya Bunge.
   
 6. Paw

  Paw Content Manager Staff Member

  #6
  Jun 12, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 2,032
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  ...utetezi nje ya vifungu vya katiba.

  Ni wazi kwamba hapa kinachotetewa ni KOSA lililofanyika kwa makusudi mazima ambapo tafsiri yake ni DHARAU dhidi ya Katiba iliyopo.

  Elewa kwamba kuna Kamati za KUDUMU za Bunge ambazo ndizo haswaa tunazoziunganisha kikatiba katika sehemu za shughuli za Bunge.

  Ukweli usipindishwe kwa maneno ya kuokoteza.

  Labda mnifafanulie hapa kisheria kuhusu majukumu (kazi, shughuli na madaraka) ya Bunge kwa undani ili isije ikawa tunaongea vitu tofauti na mada
   
 7. K

  Kieleweke Member

  #7
  Jun 12, 2012
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Mkuu,

  Nakuomba uongee kidogo kuhusu Jaji Mkuu na Jaji wa Zanzibar kuongoza kamati ya Bunge.

  Maana yake ni kwamba Bunge linaweza kutengeneza kanuni inayoruhusu hata wewe uwe mwenyekiti wa Kamati ya Bunge.


  Kazi ya kutunga Kanuni hiyo ni ya Bunge na inafanywa “mace” ikiwepo. Lakini Kamati utakayoongoza haina nguvu au mamlaka ya kibunge.

  Umeuliza kuhusu mamlaka ya Bunge. Mamlaka ya Bunge ni kutunga sheria, kuiuliza serikali. Haya yameainishwa kwenye katiba ambayo najua unaijua.

  Unaweza kusema mbona Kamati zinamuuliza Waziri. Hakuna Kamati inayofanya kazi zake halafu uamuzi wake ukawa wa mwisho. Kamati zote hata kama zimefanya utafiti mzuri kiasi gani, bado inabidi ipeleke findings zake pale Bungeni ili wabunge watoe maamuzi ya mwisho kukiwa kuna “mace”.

  Maana ya “mace” imo kwenye ibara ya 3 ya Kanuni za Bunge kama ifuatavyo:
  “Siwa” ni rungu la dhahabu linalotumika kama kielelezo cha mamlaka ya Bunge ambalo hubebwa na Mpambe wa Bunge akimtangulia Spika wakati wa kuingia na kutoka kwenye Ukumbi wa Bunge kabla na baada ya kikao cha Bunge;

  Hivyo, kikao ambacho hakina “siwa/mace” mbele yake hicho si kikao cha Bunge. Unaweza kukiita Kamati au vyovyote. Na ndiyo maana hata uchaguzi wa SPika hufanywa kwenye kikao kama hiki ambacho hakina “mace”.

  Ukiju maana ya “mace” utamaliza ubishi wote. Vinginevyo tutabishana hadi asubuhi.

  Narudia, uku-comment, tueleze kidogo, unaelewaje kuhusu Kamati ya Bunge kuongozwa na Jaji Mkuu.
   
 8. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #8
  Jun 12, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mmh, mpita njia tu...
   
 9. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #9
  Jun 12, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Shule nzuri sana hii kwangu, i real liked it and encourange this kind of topics
   
 10. Ditto

  Ditto Member

  #10
  Jun 12, 2012
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ni wakati gani hasa mtu anatambulika kama mbunge? wakati ametangazwa na msimamizi wa uchaguzi au wakati ameapa mbele ya spika? Tukishajua hilo, hapo ndio tutaweza kukitegua kitendawili cha hao mawaziri maana wanatakiwa wachaguliwe kati ya wabunge(ambao wanatambulika kisheria).
   
 11. Kilasara

  Kilasara JF-Expert Member

  #11
  Jun 12, 2012
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 578
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wakati Msimamizi wa Uchaguzi anapotangaza mgombea Ubunge ameshinda, anatamka pia hapo hapo kuwa huyo ni Mbunge wa Jimbo hilo. Pia Rais anaweza kikatiba Kumteua mtu kuwa Mbunge, na anakuwa Mbunge kuanzia hapo. Rais hawezi kumteua mtu kuwa Waziri kabla mtu huyo hajawa Mbunge kwanza: wa kuchaguliwa au wa kuteuliwa.
   
 12. KOMBESANA

  KOMBESANA JF-Expert Member

  #12
  Jun 12, 2012
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 862
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  kweli hii ni shule!shukrani kwa kutufungua mawazo hata kama maswali bado ni mengi.katika ulimwengu wa firka mmetuelekeza kiasi kwamba anayetaka kutambua zaidi aendelee kusoma,kuuliza,kutafiti,kuchunguza na kuhoji ili akili zetu zikue
   
 13. B

  Bob G JF Bronze Member

  #13
  Jun 12, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Na hata kama angekosea ungemfanyanini Rais yupo juu ya sheria?
   
 14. Paw

  Paw Content Manager Staff Member

  #14
  Jun 12, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 2,032
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Mkuu labda nikueleweshe kwa mifano inayoishi..

  Katika mfumo wa Asasi nyingi kuna kipengele muhimu cha Mikutano ya ASASI ambapo mengi yameainishwa mule.

  Tuangalie kwenye hii mikutano, utakuta mfumo wa ASASI (Katiba) umeweka mkutano mkuu wa wadau wa asasi husika na utaratibu na washiriki wake ni obvious. Ila kuna kipengele cha mkutano wa dharura ambapo hutambulika kama kikao/ mkutano halali lakini huwa haupo kwenye ratiba za kalenda za asasi.

  Hivyo suala la Jaji Mkuu, au hata mimi kuingia na kuongoza kamati za Bunge ni suala la extraordinary na siyo kwa ratiba iliyowekwa rasmi.

  Tunashuhudia kwamba suala la uwajibikaji limeachwa kwa kada ya chini ambapo zimetungwa sheria na kanuni mbalimbali endapo kutakuwepo na ukiukwaji wa taratibu zilizopo. Ila WAKUBWA wanapoamua kupindisha ama kukiuka taratibu huwa kunatumika utaratibu wa kutetea makosa hayo na KUYAPOTEZEA...
   
 15. S

  SubiriJibu JF-Expert Member

  #15
  Jun 13, 2012
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 1,124
  Likes Received: 776
  Trophy Points: 280
  Bunge siyo assasi (institution). Bunge ni mkusanyiko (Assembly).

  Jaji kuwa m/kiti wa kamati si dharura. Ni deliberate plan imo ndani ya katiba
   
 16. Paw

  Paw Content Manager Staff Member

  #16
  Jun 13, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 2,032
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Hayo ni matakwa ya KATIBA. Je katiba hiyo hiyo inaruhusu waziri kuapishwa kabla ya kiapo cha ubunge?

  A plain truth hapa ni kwamba Serikali kwa ukuu wake imekiuka vipengele vya katiba hasa kwa kumshauri vibaya rais kuhusu kuwaapisha mawaziri ambao si wabunge.

  Kuapa kwao jana hakuondoi kosa lililofanyika awali. Ni mfano mbaya usiopaswa kuigwa
   
 17. k

  kijonjolow Member

  #17
  Jun 13, 2012
  Joined: Apr 14, 2012
  Messages: 56
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 15
  Haya ndio mawozo uzamifu katika hoja kwa na wengine ni shule tosha na iwapo mtu anabisha basi ajenge hoja kama ulivyoweza kuchambua kwa hili raisi hakukosea kabisa kabisa!!!!
   
 18. S

  SubiriJibu JF-Expert Member

  #18
  Jun 13, 2012
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 1,124
  Likes Received: 776
  Trophy Points: 280
  Moderators,
  Naomba mnipige life ban iwapo huyu Paw akinitajia kifungu cha katiba kinachomkataza Rais kuwaapisha kama alivyofanya.
   
 19. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #19
  Jun 13, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,069
  Likes Received: 6,533
  Trophy Points: 280
  Hapa panahitaji umakini kwenye kusoma hii.
   
 20. Paw

  Paw Content Manager Staff Member

  #20
  Jun 13, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 2,032
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Mkuu wala usijiapize kwa suala hili.
  Kwanza weka majibu ya swali langu hilo hapo chini kabla sijajibu la kwako
   
Loading...