Rais Felix Tshisekedi wa DR Congo kuwasili nchini Juni 13, 2019

Serikali siku hizi inasikiliza nilishauri May 22 hapo chini

Washauri wa serikali ni lazima tujue hatuwezi kujifungia tu ndani ya Tanzania wakati majirani zetu wana mali ambazo zinachukuliwa na China, US na nchi za EU.

Mimi nafikiri Magufuli anatakiwa kusafiri kwenye Congo ili kuweka urafiki na kusaidia kwenye sehemu hizi kwa manufaa ya taifa.

  • Reli tutafute strategic investment kwenye reli yetu ya umeme ili Congo waweze kuitumia
  • Soko la Madini. Tufungue soko la madini Kigoma ili madini yaweze kuja Tanzania. Ombea kazi geologist wetu pale vilevile
  • Soko ya vyakula liwe kigoma hasa samaki wa ziwa Tanganyika na soko la vyakula. Ingine mikataba ya kuuza vyakula Congo. Lakini washauri watanzania waanzishe viwanda vya mazao kama Azam pale kigoma waweze kuuza vitu Congo

  • Yaani hawa China na wengine ndiyo pekee wanachukua madini pale wakati sisi tumekaa hapa tu na jeshi leo linashughulikia korosho.

    Tungepeleka jeshi jeshi kama patner pale na kuhakikisha hakuna wizi na sisi tunaweka soko pamoja na Congo na tunakuwa partners.

    Sisi tumekuwa watu wa kuchukuwa wakimbizi tu hawa wengine wanawaletea silaha waendelee kupigana wakati wanachukua Gold na mengine mengi.

    Tanzania tusijivutevute uwezo tunao, urafiki tunao, nia tunayo sasa tunasubiri nini wakati Congo inaliwa mbele yetu hivi?. Ni kwanini hatupati hata mbao za bei rahisi kutoka kwenye ile misitu ya Congo?
 
Back
Top Bottom