Cannabis
JF-Expert Member
- Jan 20, 2014
- 8,938
- 25,281
Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte anaonya kuwa Wafilipino ambao wanakataa kupata chanjo dhidi ya coronavirus hawataruhusiwa kuondoka nyumbani kwao kama kinga dhidi ya aina ya kirusi cha delta kinachoenea zaidi.
Duterte alisema kwa njia ya televisheni Jumatano usiku kwamba hakuna sheria inayoamuru kizuizi kama hicho lakini akaongeza yuko tayari kukabiliwa na mashtaka ili kuwaweka watu ambao "wanasambaza virusi kushoto na kulia" barabarani. Amesisitiza iwapo raia hao waliokataa kuchanjwa watatoka nje ya nyumba zao, atalazimika kuagiza polisi kuwarudisha majumbani mwao.
Rais huyo akizungumza kwa ukali aliongeza kuwa kwa watu ambao hawataki kupatiwa chanjo, wanaweza kufa muda wowote.
Hata hivyo, licha ya kusita kwa umma kupokea chanjo dhidi ya COVID-19, nchi hiyo yenye raia ya zaidi ya milioni 108 imekuwa ikikabiliwa na upungufu wa chanjo.
Karibu Wafilipino milioni 7 wamepewa chanjo kamili na wengine zaidi ya milioni 11 wamepokea dozi ya kwanza. Hiyo ni asilimia ndogo ya lengo la serikali la kichanja kati ya watu milioni 60 hadi 70.