Rais Dr Magufuli hajapotoshwa yuko sahihi kuhusu mapato ya Majiji...Jiji la Dodoma Bil 24.4 na Jiji la Dar Bil 16.8

tatum

JF-Expert Member
Jan 16, 2018
5,786
4,490
Rais Dr Magufuli hajapotoshw akuhusu mapato ya Halmashauri ya Majiji nchini kama alivyotoa taarifa hiyo alipokuwa anawaapisha viongozi aliowateuwa hivi karibuni Ikulu Dar es salaam.

Tusichanganye Halmashauri za Manispaa na Halmashauri za Majiji.....Rais alilinganisha Halmashauri ya Jiji la Dar na Halmashauri ya Jiji la Dodoma ambako makusanya kwa Dar ni Billion 16.8 na kwa Jiji la Dodoma ni Bilion 24.4

Nadhani Meya Boniface anatakiwa kuomba radhi kuhusu suala hilo baada ya kudai kuwa Rais kapotoshwa na akatoa takwimu kuhusu makusanya kwa kuchanganya Majiji na Manispaa wakati Rais alieleza vizuri kabisa kuhusu Majiji na Manispaa ambako Halmashauri ya Kinondoni ni yw amwisho kwa Munispaa huku kwa Majiji Mbeya ndiyo ya mwisho.
 
Sawa msemaji wa Ikulu tumekusikia.
Taarifa ziko sahihi kabisa alizoongea Rais lakini kuna watu kwa makusudi kabisa wanataka kuzipotosha halafu wakishughulikiwa kwa mujibu wa sheria wanalalamika.Sasa huyo Meya Boniface akihitajika kutoa maelezo yake kuhusu kauli ya Rais ataanza kusema ameonewa na ni msomi kabisa.Rais ameeleza wazi kabisa kuhusu Majiji na siyo mkusanyiko huo wa Manispaa kama Meya anavyotaka kuupotosha umma wa Tanzania na kuna wengine wameanza kuamini kuwa Rais amedanganywa kitu ambacho si kweli.

Na hata mwezi wa sita ..June Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma alitoa taarifa hizo kuhusu majiji 6 na makusanyo yake wakati huo Jiji la Dodoma lilikuwa linaongoza na kufuatiwa na Jiji la Dar na la mwisho lilikuwa Jiji la Mbeya
 
Fedha za mauzo ya viwanja haiwezi kushindana na mapato ya Dar es salaam kwa muda mrefu.
Mapato ya Jiji la Dar yameshuka kutokana kuwepo na maagizo, maelekezo yasiyo rafiki na usimamizi mbovu wa sera za awamu ya tano kwenye biashara ndogondogo na ujasiriamali
 
Kuna watu wanakazi ya kutetea kauli za jamaa... yaani siku tatu zote ulikuwa unawaza na kulinganisha kauli ya raisi na ya meya ili use na mawazo ya kumtetea hoja.... kwa sehem yangu sipingani na kauli ya mtu ila pia hainichukulii mda kuwaza namna ya kusafisha kauli ya mtu.. lakini hongera kwa juhudi zako
 
Halmashauri ya jiji la Dar iko wapi? Tumia akili.Halmashauri ya jiji la Dar inaundwa na manispaa za kinondoni,ubungo,Temeke na Kigamboni,Halmashauri zote hizo zinatengeneza kitu kinaitwa jiji la Dar es Salaam ambalo nabii jiwe anadai limezidiwa mapato na Dodoma......bichwa maji.
 
Swali la ufahamu: Bajeti ya Jiji la Dodoma 2017/2018 ilipangwa lini? Maana nachokifahamu kama sijakosea Dodoma Jiji lilitangazwa 26/4/2018 sasa unapotofautisha Mapato ya Dodoma Jiji na Dodoma Manispaa!!!!!!?????. Na kama Bajeti ilipangwa robo ya Mwisho ya Mwaka wa fedha wa Serikali kwaiyo kwa miezi miwili Mapato yamekusanywa na kuvuka malengo. Kama umeweza kutofautisha Manispaa na jiji Basi ata Mapato ya Dodoma Jiji na Manispaa yatofautishe.

Mtoa mada naomba ufafanuzi...
 
Hata kwa hyo idadi ya wakazi bado nina mashaka dodoma pale UDOM tukifunga chuo biashara zinadorora ka nn hayo mapato wanakusanyia wapi labda kule ng'ong'ona hata kwa mwanza huwez ilinganisha na DODOMA
IMG-20180802-WA0129.jpg
 
Kwa kuruhusu biashara holela n'a kutokuwa n'a utaratibu hata mapato y'a dar yangekuwa nusu y'a hayo y'a 16b nisingeshangaa ! Wenye kulipa kodi wamekabwa koo n'a wasiokuwa n'a shughuli maalumu
 
Hii kidogo haija niingia akilini Dodoma ndiyo.....? Kuzidi dar Na vyanzo vyote hivi au ndiyo promotion ya makao makuu anaye weza kufafanua kiufundi aje plz
usichanganye mapato ya kinondoni,temeke,ilala,kigamboni na ubungo hizo ni halmashauri za manispaa ambazo nazo zina mapato yake ya ndani.....hapa inaongelewa halmashauri ya jiji ambayo ina mapato yake ambayo ni billion 16.8......moja ya mapato ya halmashauri ya jiji la dar ni pamoja stand ya mabasi ya ubungo
 
Swali la ufahamu: Bajeti ya Jiji la Dodoma 2017/2018 ilipangwa lini? Maana nachokifahamu kama sijakosea Dodoma Jiji lilitangazwa 26/4/2018 sasa unapotofautisha Mapato ya Dodoma Jiji na Dodoma Manispaa!!!!!!?????. Na kama Bajeti ilipangwa robo ya Mwisho ya Mwaka wa fedha wa Serikali kwaiyo kwa miezi miwili Mapato yamekusanywa na kuvuka malengo. Kama umeweza kutofautisha Manispaa na jiji Basi ata Mapato ya Dodoma Jiji na Manispaa yatofautishe.

Mtoa mada naomba ufafanuzi...
kumbuka bajeti ilishapangwa ilipokuwa munispaa
 
Halmashauri ya jiji la Dar iko wapi? Tumia akili.Halmashauri ya jiji la Dar inaundwa na manispaa za kinondoni,ubungo,Temeke na Kigamboni,Halmashauri zote hizo zinatengeneza kitu kinaitwa jiji la Dar es Salaam ambalo nabii jiwe anadai limezidiwa mapato na Dodoma......bichwa maji.
hayo ni mawazo yako.....Halmashauri ya Jiji la Dar ina mipaka yake kiutendaji na siyo mkusanyiko wa hizo manispaa kama unavyofikiri na Halmashauri za manispaa zina mipaka yake kiutendaji
 
Rais Dr Magufuli hajapotoshw akuhusu mapato ya Halmashauri ya Majiji nchini kama alivyotoa taarifa hiyo alipokuwa anawaapisha viongozi aliowateuwa hivi karibuni Ikulu Dar es salaam.

Tusichanganye Halmashauri za Manispaa na Halmashauri za Majiji.....Rais alilinganisha Halmashauri ya Jiji la Dar na Halmashauri ya Jiji la Dodoma ambako makusanya kwa Dar ni Billion 16.8 na kwa Jiji la Dodoma ni Bilion 24.4

Nadhani Meya Boniface anatakiwa kuomba radhi kuhusu suala hilo baada ya kudai kuwa Rais kapotoshwa na akatoa takwimu kuhusu makusanya kwa kuchanganya Majiji na Manispaa wakati Rais alieleza vizuri kabisa kuhusu Majiji na Manispaa ambako Halmashauri ya Kinondoni ni yw amwisho kwa Munispaa huku kwa Majiji Mbeya ndiyo ya mwisho.
tupe takimwu sio kuropoka tu, meya aliongea kwa namba
 
Taarifa ziko sahihi kabisa alizoongea Rais lakini kuna watu kwa makusudi kabisa wanataka kuzipotosha halafu wakishughulikiwa kwa mujibu wa sheria wanalalamika.Sasa huyo Meya Boniface akihitajika kutoa maelezo yake kuhusu kauli ya Rais ataanza kusema ameonewa na ni msomi kabisa.Rais ameeleza wazi kabisa kuhusu Majiji na siyo mkusanyiko huo wa Manispaa kama Meya anavyotaka kuupotosha umma wa Tanzania na kuna wengine wameanza kuamini kuwa Rais amedanganywa kitu ambacho si kweli.

Na hata mwezi wa sita ..June Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma alitoa taarifa hizo kuhusu majiji 6 na makusanyo yake wakati huo Jiji la Dodoma lilikuwa linaongoza na kufuatiwa na Jiji la Dar na la mwisho lilikuwa Jiji la Mbeya
Pambana. Mkuu na ww utateuliwa
 
Back
Top Bottom