Rais Dr. Magufuli amsimamisha kazi aliyekuwa Mkurugenzi wa Mji wa Babati Ndugu Omari Mkombole

Foundation

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
1,421
603
Wanabodi,

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli amemsimamisha kazi aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Babati Ndugu Omari Mkombole. Omari Mkombole alihamishwa kutoka Halmashauri ya Mji wa Babati na kupelekwa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma mwishoni mwa mwaka jana.

Rais ameyasema hayo leo mchana katika mji wa Babati karibu na Ofisi ya CCM mkoa wa Manyara alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Mji wa Babati aliposimamishwa kusikiliza kero zao wakati akitokea Dodoma kuelekea Arusha.

Rais aliyasema hayo alipoulizwa na mwananchi mmoja kero za ardhi zinazowakabili hasa zinazohusu Shamba la Makatanini. Rais alimjibu mwananchi kwamba taarifa zote za ardhi anazo na anazishughulikia. Rais akasema amemsimamisha aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati kwa tuhuma zinazohusu uuzaji wa ovyo wa shamba la Makatanini.

Kusimamishwa huku kumekuja baada ya Tume iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Kocha Joel Bendera na kugundua kero nyingi na ubadhirifu katika mradi wa kuuza viwanja katika shamba la Makatanini na sekta nyingine zinazosimamiwa na Halmashauri ya Mji wa Babati.

Chanzo: Mimi mwenyewe, nilikuwa eneo la tukio
 
Rais uwe muangalifu na wananchi wa manyara (magugu,babati) na arumeru,siku hizi wanajichukulia sheria mkononi ya kupora mashamba ya wamiliki halali na kujigawia.Yaani wao wanajifanya wanaijua thamani ya ardhi kuliko watu wengine.Hii inapelekea hata wawekezaji katika kilimo kuwa na woga wa kuvamiwa na wanavijiji
 
Bado kuna wale madiwani wa zamani walioshiriki kwenye ,chezo wa shamba la katani tuwachukulie hatua..Safi sana kwa kuchukua hatua, huu mgogoro ulipelekea Pauline Gekulu kuvuliwa nguo hadharani akipinga utaratibu wa kuuza viwanja.
 
Rais uwe muangalifu na wananchi wa manyara (magugu,babati) na arumeru,siku hizi wanajichukulia sheria mkononi ya kupora mashamba ya wamiliki halali na kujigawia.Yaani wao wanajifanya wanaijua thamani ya ardhi kuliko watu wengine.Hii inapelekea hata wawekezaji katika kilimo kuwa na woga wa kuvamiwa na wanavijiji

Arumeru haipo mkoa wa Manyara. Arumeru ni moja kati ya Wilaya zilizopo mkoa wa Arusha. Arumeru inajulikana kama Wilaya ya Meru, makao makuu yake yapo USA RIVER.
 
Rais uwe muangalifu na wananchi wa manyara (magugu,babati) na arumeru,siku hizi wanajichukulia sheria mkononi ya kupora mashamba ya wamiliki halali na kujigawia.Yaani wao wanajifanya wanaijua thamani ya ardhi kuliko watu wengine.Hii inapelekea hata wawekezaji katika kilimo kuwa na woga wa kuvamiwa na wanavijiji
sawa BONGOLALA
 
Wanabodi,

Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli amemsimamisha kazi aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Babati Ndugu Omari Mkombole. Omari Mkombole alihamishwa kutoka Halmashauri ya Mji wa Babati na kupelekwa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma mwishoni mwa mwaka jana.

Raisi aliyasema hayo leo mchana katika mji wa Babati karibu na Ofisi ya CCM mkoa wa Manyara alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Mji wa Babati aliposimamishwa kusikiliza kero zao wakati akitokea Dodoma kuelekea Arusha.

Raisi aliyasema hayo alipoulizwa na mwananchi mmoja kero za ardhi zinazowakabili hasa zinazohusu Shamba la Makatanini. Raisi alimjibu mwananchi kwamba taarifa zote za ardhi anazo na anazishighulikia. Raisi akasema amemsimamisha aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati kwa tuhuma zinazohuzu uuzajia wa ovyo wa shamba la makatanini.

Kusimamishwa huku kumekuja baada ya Tume iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Kocha Joel Bendera na kugundua kero nyingi na ubadhirifu katika mradi wa kuuza viwanja katika shamba la Makatanini na sekta nyingine zinazosimamiwa na Halmashauri ya Mji wa Babati.

Source: Mimi mwenyewe, nilikuwa eneo la tukio

Huyu so ndiye alitoa ushaidi juzi juu ya kesi ya Kafulira kule Kigoma , Kwa utetezi ule bora aende tu aiseeee
 
Hata chembe ya huruma hakuna? Apewe basi hata nafasi ya kujitetea
 
Wanabodi,

Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli amemsimamisha kazi aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Babati Ndugu Omari Mkombole. Omari Mkombole alihamishwa kutoka Halmashauri ya Mji wa Babati na kupelekwa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma mwishoni mwa mwaka jana.

Raisi aliyasema hayo leo mchana katika mji wa Babati karibu na Ofisi ya CCM mkoa wa Manyara alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Mji wa Babati aliposimamishwa kusikiliza kero zao wakati akitokea Dodoma kuelekea Arusha.

Raisi aliyasema hayo alipoulizwa na mwananchi mmoja kero za ardhi zinazowakabili hasa zinazohusu Shamba la Makatanini. Raisi alimjibu mwananchi kwamba taarifa zote za ardhi anazo na anazishighulikia. Raisi akasema amemsimamisha aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati kwa tuhuma zinazohuzu uuzajia wa ovyo wa shamba la makatanini.

Kusimamishwa huku kumekuja baada ya Tume iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Kocha Joel Bendera na kugundua kero nyingi na ubadhirifu katika mradi wa kuuza viwanja katika shamba la Makatanini na sekta nyingine zinazosimamiwa na Halmashauri ya Mji wa Babati.

Source: Mimi mwenyewe, nilikuwa eneo la tukio
Safi sana mheshimiwa. Lakini nikukumbushe tu kuwa hicho ni kijipu ambacho hata uliowateua wangeweza kukipasua. Majipu ni mengi yanayotumbulika lakini naona umeyageuzia macho. Mojawapo ni hili la UDA na DART. Je, unadhani haya bado hayajaiva?
 
Wasomali kibao wapo Nrb na Ars wanamiliki maeneo makatanini Babati!!
Watu wamejimilikisha maeneo kiholela, bila utaratibu!!
Kesi ya Mbunge Paulina kuvuliwa nguo na kupigwa na madiwani ifufuliwe sasa!!
 
Back
Top Bottom