GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,542
- 108,856
Nilikuwa nasikia na nikawa napuuzia ila kwa takribani mwezi mmoja sasa nimekuwa nikiifuatilia na kuisikiliza kiumakini sana Idhaa ya Kiswahili ya BBC ( Radio ) hadi hatimaye nikaja kupata majibu yangu ambayo hayapishani sana na ya Wale wenzangu waliyoyaona mapema kabla yangu.
Sasa siyo Siri tena kwamba hii idhaa ya Kiswahili ya BBC ( Radio ) ina chuki narudia tena kusema ina chuki ya waziwazi na Rais Dkt. Magufuli na Serikali yake. Hili linathibitika sana na maudhui ( Content ) yake hasa katika mambo yanayoihusu nchi ya Tanzania.
BBC Swahili siku zote wakija hewani lazima waje na something negative juu ya ama Rais Dkt. Magufuli au Serikali yake na ni nadra sana kuwasikia BBC Swahili ( Radio ) wakisema mabaya ya nchi ya Kenya labda kwakuwa wengi wa Watangazaji wao wa sasa hasa Bosi wao Mkuu anatokea nchini Kenya.
Hii idhaa ya BBC ( Radio ) ipo au inasikika takriban katika nchi zote tano ( 5 ) za Maziwa Makuu ( Great Lakes ) zikiwemo Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi huku kwa mbali sana kule kwa majirani zetu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo lakini cha kushangaza hawa BBC Idhaa ya Kiswahili wao interest yao ni mabaya tu yanayotokea nchini Tanzania na hasa hasa yakiwa yamefanywa na Rais Dkt. Magufuli au mmoja wa Watendaji wake wa katika Serikali yake.
Mfano hai tu mara baada ya Kauli ya Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli juzi dhidi ya Mabinti wa Shule na upataji Mimba / Ujauzito Idhaa ya Kiswahili ya BBC ( Radio ) walichokifanya wao ni kutafuta tu maoni ya upande mmoja tena ule ambao unaiponda Serikali na maamuzi ya Mheshimiwa Rais na kama haitoshi hawa hawa BBC Swahili badala ya kutafuta maoni ya Watu kutoka hapa hapa Tanzania wao wamekuwa wakitafuta Watu kutoka nchini Kenya na kuyasemea mambo yanayoendelea Tanzania kitu ambacho sidhani kama kina afya sana Kiueledi.
Napatwa na hisia kuwa yawezekana sasa hii idhaa ya Kiswahili ya BBC imekuwa ni moja ya Silaha Kali lakini iliyojificha ya kuweza kuangamiza juhudi zote za Rais Dkt. Magufuli pamoja na Serikali yake yote au yawezekana pia BBC Swahili ( Radio ) wanatumika na Maadui wakubwa wa Mheshimiwa Rais au nchi yetu nzuri ya Tanzania.
Tafadhali Rais Dkt. Magufuli, Waziri Dkt. Mwakyembe na Mamlaka zingine zote husika hebu haraka sana imulikeni kwa jicho la Kiumakini mno hii idhaa ya Kiswahili ya BBC ( Radio ) vinginevyo mkiendelea kuwalea hawa Watu kuna siku yaliyofanywa na hii Redio ya RTLM mwaka 1994 huko nchini Rwanda yanaweza pia yakatokea hapa nchini Tanzania.
Nawasilisha.