Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameziagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Wizara ya Fedha kutoza Kodi ya nyumba 10,000/= kwa nyumba ya kawaida, 20,000/= kwa Gorofa zilizopo Wilayani na vijijini na 50,000/= Kwa nyumba kubwa. Rais amesema viwango hivyo vizingatie Hati ya nyumba na siyo idadi ya nyumba katika kiwanja.