JUAN MANUEL
JF-Expert Member
- Nov 26, 2010
- 6,823
- 14,173
Jiwe angekuwepo hii safari angeenda PM au Makamu wa raisi
Alisha sema tushirikiane nae anaonyesha mfano, anavunja taratibu yeyote, jiwe amewahi mtuma Pinda China amwakilishe, si shida! Wote raia wa tz.Kuna jamhuri ya muungano na serikali ya Zanzibar na kila moja ina mamlaka yake
Mbona unasema uongo? Hamna mahali kwenye Katiba panapo mkataza Rais kuchagua mtu yeyote kumwakilisha? Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano na raia wake ni watanzania kama tulivyo wengine watanganyika. Kwa sababu hiyo Rais ana haki ya kumchagua kutoka sehemu yeyote ya JMT kumwakilisha katika shughuli yoyote. Hata akitaka anaweza kumuomba Lissu amuwakilishe katika kikao kitakachofanyika The Hague na hamna atakayeweza kumzuia.Rais wa Zanzibar hatakiwi kumwakilisha rais kwa mambo ya muungano ndio maana kwenye katiba wameweka wazi rais akitoka upande mmoja makamu wake anatoka upande mwingine na hata rais tuliyenaye tumempata kwa utaratibu huo
Mkuu kujua kwanini fulani kamtuma fulani KWA KWELI SIJUI kama ambayo hakuna aneyejua kwa nini umlimuoa/kuolewa na unaendelea kuishi na huyo aliyemuoa/kuolewa nayeUsiwe mchoyo wa maarifa mkuu, kama unayo lakini.
Mbona haukuuliza alivyoingia kwenye kikao cha baraza la mawaziri? Je unajuaje ndio alichopangiwa kufanya kwenye kile kikao?
Mkuu, tumefikaje huku?
Ukijua kwenye baraza la mawaziri aliingia kama nani ndio utapata jibu lako kwanini katumwa na Mh SSH.
Ndiyo maana ya MUUNGANO Mkuu. Halafu hivi hawaoni jinsi Mwinyi alivyo na credibility? Yaani hakika hata Wazanzibari wanafurahia. Kifupi Mwinyi ataibadilisha sana Zanzibar kiuchumi, kisiasa na kijamii. Na dada yake huku tunaamini mambo mengi yataboreka sana.I
Limekaa vizuri tu, tena Lima afya na linaleta taswira nzuri mno kwenye JAMII ya kimataifa.
Kimsimgi, Rais Wa Jamhuri ya Tanzania amaweza kumtuma raia yeyote ndani ya mipaka ya Jamhuri ya muungano Wa Tanzania!! Hapo ni credit kwa mama!!
Rais wa Zanzibar ni sehemu ya Baraza la Mawaziri la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Rejea ibara ya 54(1) ya Katiba ya JMT.Ndugu zangu!
Ni huyu mtoto wangu mdogo kaniuliza hilo swali.
Kwamba kwenye mkutano wa SADC inasemekana Rais wetu atawakilishwa na Rais wa Zanzibar, Dr Hussein Mwinyi.
Hii ikoje kiitifaki?
Rais wa Mwinyi anawajibika kuripoti kwa Samia?
Huko SADC Zanzibar ni nchi mwanachama?
Maswali ni mengi, karibuni tujadili.