Rais Bora Tanzania - Chaguo la JF

Superman

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
5,695
1,692
Tumeona jinsi wana JF walivyo na upeo wa juu wa kuweza kuchambua mambo mabilimabli na hata viongozi.

Sasa kuna changamoto napenda kutoa kwa JF, na ningependa kwa hili tusikurupuke tu bali tutumie hekima na busara za hali ya juu kuchagua Mtanzania ambaye wewe mwana JF ungependa awe Rais wa Tanzania. Ni vema utaje jina na kisha kutoa sababu za chaguo lako.

Pili fikiria kuwa Prime Minister lazima awe member wa JamboForums.

Je Ni nani ungemchagua Rais? Kwa nini? Na ni nani PM kutoka JF na kwa nini?

Kazi kwenu.
 
Risi bora ni August Joseph ....ijapokuwa kijana bado anasoma ila kwakweli ni mtanzania mwenye nia ya maendeleo kwa watanzania wengi....huyu ndo mkombozi wa watanzania ndiye yule tuliye ahidiwa na mungu kwa taifa la watanzania
Waziri Mkuu ni Mh magufuli
 
Tumeona jinsi wana JF walivyo na upeo wa juu wa kuweza kuchambua mambo mabilimabli na hata viongozi.

Hapa swali limeanza kama lile aliloanza nyoka kumuuliza Eva kwenye bustani ya Edeni

Sasa kuna changamoto napenda kutoa kwa JF, na ningependa kwa hili tusikurupuke tu bali tutumie hekima na busara za hali ya juu kuchagua Mtanzania ambaye wewe mwana JF ungependa awe Rais wa Tanzania.

Hapa najibu kwa niaba ya kaka Ben Mkapa, nashauri Rais atoke kwenye ile kampuni yetu ya Net Group Solutions, na sababu ni kuwa watanzania wote ni wavivu wa kufikiri.
 
Rais - Salim Ahmed Salim

Waziri Mkuu toka JF: Mwanakijiji
 
Mtu wa pwani natamani sana swali lingekuwa sifa zinazostahili kwa kiongozi kuwa Mkuu wa Nchi na Kuwa Waziri Mkuu.

Nami ningechangia kwamba kiongozi yeyote kwenye hizo ngazi lazima awe amewahi kuwa kiongozi shuleni...
 
Rais awe Kada Mpinzani

Makamu wa Rais:Gembe

Waziri Mkuu:Augustine Mosha

Waziri wa habari na msemaji wa Nchi Mzee Mwanakijiji

Waziri wa burudani:Brazemeni a.ka. stinger belle
 
waswahili wanasema,mpe mtoto wako mchawi amlee, waswahili wameenda mbali sana, hata ulinzi wa mali mpe mwizi ulinzi wa mali hiyo. hapo sasa ndipo utakapoona kumbe viongozi wanaostahili ni hawa.

Rais ni E L

MAKAMU WA RAIS KARAMAGI

WAZIRI MKUU BWM

WAZIRI WA HELA FT SUMAYE,
NAIBU WAKE ALEX MASAWE
NAIBU WA PILI BABU SAMBEKI

WAZIRI WA USALAMA WA RAIA ZOMBE,
NAIBU WAKE MAHITA.
WATOTO NA USTAWI WA JAMII KINGUNGE,

HAPO BWANA HAKIPOTEI. NA HAO WAKIANZISHA CHAMA CHAO,CCM BYEBYE,KUTOKANA NA UMAKINI WA UTUMISHI WAO KATIKA NAFASI ZAO.

NISAIDIENI KAMA NIMEKOSEA.

SEFF.
 
Kama kule Kenya.Nguvu ya umma itawaondoa.Rostam waziri wa miundo mbinu.Umefunga kazi.
 
2010 . . . Vipi Dr. W. Slaa?

Hana nafasi ya kuwa kiongozi bora. Yeye ni wakutuibulia UFISADI na kutufichulia Mafisadi.
Tusimpe uongozi tutakosa mtu jasiri wa kufanya kazi za kutokomeza mafisadi.

Tukikosea kwa kumpa uongozi tutafanya kosa kama tulivyompoteza Daktari bingwa wa Mifupa na upasuaji tulipompa Prof. Sarungi uongozi wa kisiasa.

Kila mtu amepewa kipaji katika nafasi yake, tusijaribu kuuwa vipaji.
 
Superman, Heri ya Mwaka Mpya!
Umeleta mada nzuri sana, hasa tukielekea uchaguzi mkuu wa 2010 hapo mwakani. Ila nadhani ume-dilute uzito wa mada yako kwa kusema Waziri Mkuu atoke JF. Simaanishi kuwa hawezi kutoka Rais au Waziri Mkuu JF, ila nadhani limitation hizo zinatufanya tutazame humu humu tu ambako watu wengi haiyumkini hatujuani uhalisia wetu! Mfano, wewe au yule waweza kuwa kiongozi mzuri kwasababu labda una/mna mawazo mazuri kisisasa, ila si katika nyanja zingine zinazohusu kiongozi bora kama inavyokubalika katika jamii.

Mnapoendelea kuchambua mada hii na kwa kuzingatia katiba yetu ilivyo, lazima kuangalia mambo yafuatayo:
1. Kiongozi lazima awe na sifa zote kisiasa, kitamaduni na kijamii mfano elimu, integrity,nk;
2. Awe na rekodi ya utendaji bora;
3. Ni LAZIMA tutazame chama chake cha kisiasa, mfano, sera zake. Chama cha siasa kina determine mambo mengi,mfano intergrity yake ikoje, kina uwezo wa kuunda serikali, nk nk.

Nashauri tujimwage bila kujali wanaotajwa wanatoka JF au la. I consider this a very serious discussion.
 
Historia ya mtu inaweza kusaidia sana nakumbuka kusoma habari ya Barack Obama kwenye Ebony ya November 2004 as a rising star. Angalia hapa Ebony | Find Ebony articles | HighBeam Research - FREE trial Barack Obama: new political star attracts national attention.(The 50 Most Intriguing Blacks Of 2004)(Biography).
Wengi wetu wamamsikia Barack juzi tu lakini waandishi wa habari walisha mtabiria toka wakati huo, amekuwa akiweka rekodi hapa na pale. Sina maana kuwa lazima awe Raisi bora lakini angalau historia yake inaweza kupa mwelekeo angalau ni mtu wa namna gani

Nov 01, 2004; Kinnon, Joy Bennett
 
Mmmh!

Salim A. Salim . . . . Ok

Prof. Mark Mwandosya sina uhakika . . . Nyeti zililizonifikia December last year ni kuwa by June 2009 Mwanazuoni huyu naye atatembelea pale Kisutu . . . Kulikoni? Tuendelee kutega masikio.
 
...Lazima awe mchochezi wa maendeleo, mbunifu, anayekwenda na wakati, awe kiongozi kwa vitendo, ...

Kuna kipindi Tanzania kulikuwa na viongozi wa namna hiyo;

Marehemu Edward Moringe Sokoine, na kina Seif Sharif Hamad, Augustino Mrema walipokuwa CCM ...bila kumsahau mzee Ali Hassan Mwinyi.

Badala ya kutangulia kuorodhesha majina ya watu ni vema kujadili sifa za mtu afaaye kuwa rais (kiongozi) kwanza na baada ya hapo ndipo tuangalie ni mtu yupi ana sifa hizo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom