Rais Biden, kwa Afrika anza na Rais Magufuli na Mwinyi wa Zanzibar

Oct 1, 2019
91
150
Salaam JF,

Baada ya Rais Biden kuapa Jana Ikulu ya Marekani imetangaza kuwa mawasiliano ya kwanza ya simu yatakayofanywa na Rais Biden ni kati yake na Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau, bila Shaka kigezo na hoja kuu ni kwa jinsi utawala wa Canada unazingatia sheria, Demokrasia na uwajibikaji kwa Wananchi wake na taasisi zake.

Kwasababu kinachofanyika Canada na Tanzania ni sawa, Aidha misimamo ya Sasa ya JPM na uwajibikaji wake kiuchumi na kifursa kwa Wananchi wake.

Pia uwezo wa Rais mpya wa Zanzibar Dkt. Mwinyi anayeonesha alama ya uwajibikaki na Mapinduzi mapya katika ustawi wa amani uchumi, nashauri na kuomba iwe sababu muhimu ya Ubalozi wa Marekani Tanzania kuyatambulisha yote haya kwa Biden ili mazungumzo yanayofata yawe kati ya Rais Biden na viongozi wetu hawa Wazalendo.

Kwa Afrika Tanzania ni kituo kikuu cha Amani na uwajibikaji, tunayo Demokrasia na mihimili inayojitegemea ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika.

Aidha historia ipo wazi kati yetu na Marekani, Kwa Mantiki hiyo Tanzania ipewe kipaumbele zaidi katika mawasiliano ya awali na Rais Biden kwa manufaa ya nchi na Africa kwa ujumla kiuchumi, Kisiasa na kijamii nina imani ili litatimia hivi karibuni.
 

Fursakibao

JF-Expert Member
Dec 12, 2017
3,168
2,000
Alisema akiingia tu anafuta like zuio. Tunasubiri kea hamu. Ngoja same Bado ni usiku huko kwake.
 

residentura

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
4,035
2,000
Biden ni mtetezi mkubwa sana wa demokrasia ya ukweli.
Secretary of State Blinken ni mwanausalama aliye mfuasi mkubwa mno wa misimamo ya B. Obama kuhusu Afrika na demokrasia yake.

Biden ni mwiba mkali kwa wanaokandamiza demokrasia na haki za binadamu( anaunga mkono ndoa za jinsi moja na haki za LGBT.
 

Mangungu

JF-Expert Member
Apr 22, 2012
3,011
2,000
Unaota wewe! Former Secretary of State, Michael Pompeo, alimtungua Makonda na sasa hivi kawatungua, baadhi ya maofisa wa serikali walioharibu uchaguzi wa mwaka jana! Hivi kwa kipi hasa CCM walichofanya hadi washinde kwa kishindo like that? Amka acha kubwabwaja!
 

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
51,722
2,000
1611207093532.png
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom