Rais awapiga kijembe TANROADS awatuhumu kuwa WABAGUZI!

Phillemon Mikael

Platinum Member
Nov 5, 2006
10,529
8,614
HIVI karibumi mheshimiwa rais alizindua barabara hapo GEITA......yenye kiwango cha lami akiwa ameambatana na waziri wa ujenzi DR SHUKURU KAWAMBWA,na KATIBU MKUU OMAR CHAMBO...

Katika uzinduzi huo muheshimiwa rais aliwalaumu TANROADS Kwa kushindwa kuweka bumps au MATUTA kwenye barabara za KATI na CHALINZE hadi dodoma na nyingine nchini kwa kisingizio cha HIGHWAY wakati barabara ya MOSHI arusha Ina MATUTA[BUMPS] kila baada ya muda mfupi....alisema watu wa TANROADS wana DOUBLE FACE [DOUBLE STANDARDS]..

Kwa kitendo cha kuweka barabara ya Moshi - Arusha matuta ambayo ni highway na kutoweka highway nyingine nchini matuta.."TANROADS GUYS ARE ABSOLUTELLY RIDICULOUS AND WITH DOUBLE FACE"..alisema...

Aliendelea kusema ukosefu wa matuta huchangia ajali za barabarani na kutaka barabara zote ziwekwe matuta hata kama wataalamu wa masuala ya ujenzi wanapinga...wataalamu wa masuala ya ujenzi wanasema matuta ni chanzo kikubwa cha kufumuka kwa barabara nyingi na kusababisha viraka..na hasa wanasema kuwa kitaalamu barabara yoyote ya highway haitakiwi iwe na matuta ..bali inatakiwa iwe na ROAD SIGNS za kutosha....ambazo nazo nyingi huibiwa na kuuzwa kama vyuma chakavu....

nashauri wawe wanaweka ROAD SIGNS ZA PLASTICS.. nimeziona wanazitumia nchi mbali mbali pia...

Barabara ya SEGERA TO MOSHI TO ARUSHA ilijengwa miaka ya 1990...kwa msaada wa nchi za SCANDINAVIAN ....wakimtumia mkandarasi wao SKANSKA..na ni kati ya barabara imara nchini......barabara ya DAR to chalinze pia ilijengwa kwa ushirikiano wa tanzania na scandinavian country kwa mkopo nafuuu kwa kutumia kandarasi wao waliojiunga SKANPHIL COLAS[ aka SKANSKA AND PHIL COLABORATION].....na ni moja ya barabara imara kabisa nchini!
 
JK siku zote amakuwa akipinga kutuhumiwa yeye leo ana tuhumuj na hata baada ya kuelezwa ukweli na wataalam ? Je kauliza sababu za matuta na ya kule anako lilia ?
 
Hivi Rais wa hiyo nchi ilipo Tanroad si akutane na ya Rais Jakaya Kikwete ili JK amuombe waweke alama na humps anazotaka??

Au waombe Umoja wa mataifa wawakutanishe kama JK ambaye ni mwenyekiti wa AU imeshindikana.

Mambo mengine bwana.................................. kweli hii nchi itaendelea kudumaa kama kweli yamesemwa hayo.
 
kirefu cha tanroad ni TANZANIA ROAD AGENCY......ndio wasimamizi wa barabara kuu zote nchini...kuna mgawanyiko wa BARABARA ZA MIKOA,BARABARA ZA MITAA...na barabara KUU....IE ZINAZOUNGANISHA MAKAO MAKUU YA MIKOA NA NCHI JIRANI....
 
Phil,

Soma katikati ya mistari. TanRoads ipo Tanzania, rais wa nchi hii ni JK na waziri anyeshugulika na Tanroads yupo chini yake. Yeye hapaswi kulalamika.

Prez akilalamika wananchi wafanyeje??? Umenipata hapo bro?

Karibu basi hapa Mbagala twende sehemu tukapate nyama choma.
 
Phil,

Soma katikati ya mistari. TanRoads ipo Tanzania, rais wa nchi hii ni JK na waziri anyeshulika na Tanroads yupo chini yake. yeye hapaswi kulalamika.

Prez akilalamika wananchi wafanyeje??? Umenipata hapo bro?

Karibu basi hapa Mbagala twende sehemu tukapate nyama choma.

FD 100% with you on this bro!

Kikwete amekuwa mtu wa kutupa lawama kwa wengine siku zote.Swali kubwa ni kwamba kama rais yeye amefanya nini?

My personal view is that matuta have no business in the highway anyway. And if TANROADS were wrong, they were wrong in the first instance.The gov should be able to implement and enforce speed limits, not a meltdown of speeding every few units of distance with matuta.
 
Heshima mbele..... Wakuu, hili swala ni kwamba kuna mambo ambayo kwa kweli tunelemea kuwasikiliza watu wanje... Hebu anagalia aya:

1. Kuna nchi ambazo watu wanafuata alama na mistari ya barabarani, hapa nyumbani kwa kweli wewe angalia hata taa za kuongoza magari ni shida kuzifuatilia..... Lakini mbaya zaidi hebu angalia ni nani anayefanya "Safety Audit" ya mabarabara yetu..... Offcourse ni makampuni ya nje yenye wataalamu ambao kwa namna moja au nyingine hawakubali kuwa madereva wetu hapa nchini (ndivyo ......, Nyani upo?)... Kwetu sisi hapa Bongo, ni mwendo wa matuta tuuuu...... alama zikipona kuibiwa, basi ujue hakuna atakayeziangalia hata zinasema nini!!

2. Hili swala la barabara kutofautiana linaleta matatizo sana.... Hii kwangu nadhani inategemea sana na yule mtoa pesa na ndicho ambacho Mheshimiwa Raisi hataki.... Akijenga Taliano matuta yanawekwa bila mizengwe, lakini wakijenga wengine wanasema sio safe, give me a break.....

3. Humohumo TANROADS (Regional Managers etc) wanapendekeza sana uwekwaji wa matuta barabarani sababu ya speed control, lakini kuna yanayopitishwa na yasiyopitishwa ikimaanisha issue ya "Double Standards" ni kweli ipo na itaendelea kuwepo mpaka pale tutakapofanya "Standardization ya Ujenzi wetu"......

Naomba kuwakilisha!!
 
FD 100% with you on this bro!

Kikwete amekuwa mtu wa kutupa lawama kwa wengine siku zote.Swali kubwa ni kwamba kama rais yeye amefanya nini?

My personal view is that matuta have no business in the highway anyway. And if TANROADS were wrong, they should are wrong in the first instance.The gov should be able to implement and enforce speed limits, not a meltdown of speeding every few units of distance with matuta.

Pundit, tupo pamoja lakini kwenye wala la matuta tukubali yafuatayo:
1. Standardization ya matuta yaani ujenzi wake na maeneo ya kuyaweka (mfano kwenye mashule, vivuko vya mifugo, vijijini nk)

2. Kwa kweli Raisi kwenda kufanya kazi ya kusimamia matuta?? Mkuu, hapana kuna watu wamepewa jukumu hili nao ndio walitakiwa kutoa mapendekezo (through Audits etc).... Mimi pekee nilifanya Safety Audit ya barabara flani hapa nyumbani na mapendekezo yalikuwa ni matuta kwenye vijiji, mashule nk. Tatizo ni kwamba implementation ilikuwa ngumu eti sababu ni highway!!! Tukumbuke kuna tofauti kubwa sana kati ya "HIGHWAYS" na "FREEWAYS".... Kwetu huku highways ndio lakini zinapita wapi?? Wenzetu wameweka vitu kama bypases (around towns/built up areas) na hivyo hawana wasiwasi na watoto etc.... hapa kwetu??

3. Kuhusu Govt ku enforce speed limit? Mkuu wewe nina uhakika kuwa unelewa kwamba sio kitu rahisi ukizingatia uwezo wetu (vifaa, askari nk)... Hata huko kwenye nchi zilizoendelea wana hikli tatizo sana tu (pamoja na kwamba wao wana Freeways) ila wao wameweka "Speed cops" wenye magari ya kufanya patrol..... So kwa hili Mkuu naomba niseme kwamba sio kitu rahisi kama kinavyosomeka!!!

Naomba kuwakilisha!!!
 
Ahsante Morani,

Valid point kuhusu bumps kwenye shule na vijiji.Ingawa ningependa kuona speed limit zinawekwa na kuwa enforced pengine siyo practical sana kwetu kutokana na gharama za ku enforce.

Still we do not need a crybaby president.Kuna mtu humu aliongelea tatizo la wanasiasa wetu kuingilia kazi za professionals.

Hivi karibuni kuna mtu alipiga kibomu uchwara Times Square NYC, meya wa NY akawa anahojiwa, katika moja ya maswali aliyoulizwa ni kwamba ka nini hajataka kujichanganya katika effort za kusafisha (photo op) au kutaka kumkamata huyu bazazi? Meya Bloomberg akajibu kwamba mimi siwezi kuingilia kwa sababu si mtaalamu wa mambo haya, naweza kwenda kusafisha halafu nikaharibu ushahidi.

Wanasiasa wetu inabidi waheshimu watendaji.Makaripio haya ya kama mtu anayekaripia watoto hayaonyeshi hilo.Na zaidi ya hilo yanamuonyesha rais aliye toothless, clueless na reluctant.
 
Tuko pamoja Pundit, kwa kweli tumejaribu sana swala la speed control ikiwemo kuweka "LUKU" kwenye mabasi lakini kama kawaida yetu rushwa na nini mambo yakawa palepale..... Unajua tumekuwa tunaangalia ajali zikiendelea kutokea siku hadi siku na kupoteza maisha ya nguvu kazi yetu muhimu sana kwa nchi yetu... Ukiangalia kwa haraka inaonekana swala zima la "Traffic Safety" limeachwa kwa Polisi.... Kwa mtazamo wangu ni kwamba Polisi sio watunga sheria za barabara bali ni wafuatiliaji wa utekelezaji (mahakama pia inaingia hapa).... Ukijiuliza, TANROADS/MoW wana jukumu/nafasi gani katika hili?? Sisi tunaishia kuangalia ujenzi wa mabarabara bila kuangalia effect ya barabara mpya, ongezeko la magari vinatoa mchango gani katika kuongezeka kwa ajali....

Hawa wakuu wa TANROADS walitakiwa kufanya a concise study ya nchi nzima kisha kuamua kufanya improvements zikiwemo matuta, rumble strips, katika mabarabara yote ya Bongo... Lakini cha kushangaza hili halijanyika, pia lazima wafanye standardization ya matuta hayo (angalia yale ya Mikumi na yale ya kule Mazinde, utafikiri jamaa wanatoa contract ya kujenga matuta na standards ni up to the contractor regardless of the difference)

Hili la wanasiasa kuheshimu watendaji ni sawa kabisa lakini ndugu yangu tukubaliane kuwa swala la ajali ijijini na uwekaji wa matuta wa kwanza kujua ni wanasiasa.....sababu ni kwamba mikutano ya hadhara wanavijiji wanalalamika kwa wanasiasa manake hao watendaji (wahandisi) hawaendi/hawafiki kujua vifo vinavyotokea kwa ajali!!! So kwa hili sidahni kama tunaweza kuwa control wanasiasa unless us, watendaji/wajenzi tuamua kutimiza wajibu wetu - kulinda maisha na mali za watu wetu!!
 
Ngoja nikale jamani. Mi huwa nachoka sana na issues za huyu kiongozi wetu.

FD,

Tatizo lako hujui system inavyofanya kazi... ile statement yake ilikuwa namna fulani ya kuwaeleza TANROAD kuwa makini...

Kuna namna mbalimbali za kuwakilisha ujumbe kwa taasisi zilizochini ya rais... ukitumia zaidi amri... it doesn't work.

Niko maeneo ya mbagala... nishitue basi tukapate hiyo nyama choma... nitakupenyezea simu yangu kwenye PM.
 
jk anasema bora matuta yatapindua magari ya madereva wakorofi wakafie mbali kuliko kuwagonga watoto wetu...

anyway as a president if what matters to him is not a political statement ni kweli haipendezi na yeye kulalamika ....kama ameshauriana na wataalamu akaona solution ni matuta...atoe maagizo tu!!!
 
Madereva na wasimamzi wa sheria na taratibu za matumizi ya barabara hawafanyi wanayopaswa kufanya....then matuta hayakwepeki. Ni madereva wachache sana wanaofuata speed limits za vibao. Lazima walazimishwe.

About Mkuu wa kaya kulalamikalalamika tu, tumezoea...tupo naye kwa miaka miwili na nusu sasa. Tusishangae siku akilalamika magodoro ya magogoni yamechakaa!
 
JK ni mbumbu sana, lini highway ikawekwa matuta, huyu jamaa si kila leo anasafili nchi mbalimbali au uwa anafikia hotel tu basi. Matuta ni kwa ajili ya residetial area, shule au business premises. Siyo kwenye highway, cha kushangaza huyo waziri ana PhD ya Construction engineering kwa nini hampi shule Mkuu wa kaya.
 
I regret to say wewe ndio mbumbu!!! Highway nyingi zina Matuta Tanzania... pamoja na Mandela Road... sidhani kuna high way Tanzania kama hiyo... lakini ndio hivyo tena vijana wetu wa chuo kikuu wamekuwa huenda wanagongwa!!!
 
I regret to say wewe ndio mbumbu!!! Highway nyingi zina Matuta Tanzania... pamoja na Mandela Road... sidhani kuna high way Tanzania kama hiyo... lakini ndio hivyo tena vijana wetu wa chuo kikuu wamekuwa wamegongwa!!!

barabara ya mandela road ina matuta, yesu na maria.
 
kama rais anatoa amri kwakua yeye ni rais bila kuzingatia ushauri wa wataalamu basi ana-abuse power.kuna maana gani ya kuwa na wataalamu kama rais anaamrisha anachotaka!!? haya matuta highway yameua sana, sehemu zenye matuta hakuna vibao, na kama ni mgeni wa barabara lazma ulivae, pia hayo matuta hayana reflecting color ambayo inasaidia kuliona hata ukiwa mbali.matuta yenyewe hayana proper dimensions, unakuta tuta kuuubwwa na haliko smooth kabisa na barabara.wangeyatoa tu kwenye highways.
 
Sawa mwananchi... nadhani hili tulipeleke ERB na CRB... sio kwa Rais... inaonyesha wananchi wa Tanzania hawajui JD ya Rais...
 
Back
Top Bottom