Rais awapiga kijembe TANROADS awatuhumu kuwa WABAGUZI!

Naona turudia tena tabia yetu ya kukimbilia kutibu symptoms badala ya ugonjwa wenyewe. Kwa kukimbilia matuta ni kukiri kuwa tumeshindwa kusimamia na kurekebisha tabia ya watumiaji wa barabara zetu. Kwa nini tunasisitiza kusema kuwa ni VIGUMU kuhakikisha sheria za usalama barabarani zinafuatwa? Wenye jukumu la kuzisimamia si wapo! kwa nini wasiwajibishwe? kwa mfano, ikitokea ajali mbaya ya basi, mwenye basi anasimamishiwa biashara ( anawajibika kuhakikisha kuwa dereva wake ni qualified na gari lake ni salama) na kamanda wa traffic wa eneo husika nae anakuwa suspended wakati uchunguzi unafanyika. Ikionekana kuwa ajali ilisababishwa na mwendo mkali, mwenye basi anaonywa na kuwajibishwa kama ni mara ya kwanza na kama ni mara ya tatu anafungiwa biashara ya kuchukua abiria. Kamanda wa traffic anashushwa cheo na ikitokea katika uangalizi wake zaidi ya mara tatu, anastaafishwa. Naamini tukifanya hivi (au hatua zifananazo) tutapunguza ajali maana hakuna anayetaka kukosa ajira au kipato. Madereva wananyang'anywa leseni kwa muda mrefu ( k.m. miaka mitano) na akirudia permamently.

Haya ya matuta yanafanana na wazo la kujenga hospitali kubwa Tumbi ati kwa vile ajali nyingi zinatokea Kibaha!

...........enforcement.............enforcement................enforcement..........Fundi yaani hiyo malizia yako hapo chini........imenivunja mbavu kweli.......hahahahah

Morani,
.....mmmmhhh....well.....tuboreshe matuta!!.............imgine mtu ana-speed between 120kph and 140kph..........."YERO" hata kama tuta ni bora kiasi gani aisee.........
Tusiwaonee haya wenye responsibility ya kuhakikisha usalama barabarani to both wenye mali/madereva na law enforcers.............lets act now
 
..................... Ili haya matuta yawe effective inabidi yawe kila baada ya mita hamsini barabara nzima! ..........................

....haya sasa........hebu angalieni wenyewe hapo juu mtaalamu anvyotueleza..............ndio maana nikasema akina Fundi Mchundo/Morani/Invisible....field yenu imevamiwa............some trying to undermine it!!
 
Mkuu Ogah, I feel you on the issue ya kuwa spidi halafu hamadi tuta... Ndio maana nikasema kwa kweli kwa hapa nyumbani unajua tumefanya vyote (luku, tochi, vituo vya kukagua muda wa mabasi, kusafiri mchana nk nk nk) lakini hakuna kitu....

Mimi ninachosema ni kwamba:
1. Wenzetu kwenye miji iliyojengeka njia kubwa (highways) wameweka bypass... Sisi hapa Bongo jamani nguvu hiyo hatuna basi tujiwekee vijimatuta (VILIVYO NA STANDARDS ETIII - hapa nina maana kuwe na distance flani imewekwa na rumble strips kwa[pande zote mbili ili wale madereva wanaojisahau waweze kuhisi kuna kitu mbele yake)

2. Hawa ndugu zetu wa idara husika (TANROADS/MoW/PORALG nk) lazima watusaidie kuangalia hili..... Ajali nyingi za watu kugongwa zinatokea katika maeneo flani flani na sio kila mahali.... Sehemu hizi lazima ziwe identified kisha iamuliwe kama ni matuta au hata rumble strip alone lakini wao kama wataalamu lazima waamue accordingly..

3. Kingine ni standardization ya matuta yenyewe...Ukifika Mikumi ukajaribu kuyapita yale matuta kama ulivyofanya Mazinde hukawii kujikuta mdomoni mwa Simba. Pia ukifika Arusha mjini pale karibu ka kwa Dr Mohammed (Arusha-Namanga Rd) kuna tuta moja pale hata ukiwa na spidi 30 usipoangalia hukawii kupindua gari....

Hiivi wakuu kuna ambao wameona yale local matuta ambayo yamekuwa yanawekwa tu eti kuna wanaokataa vumbi, kuna wenye majumba mazuri hawataki kelele nk? Sasa haya yoote ndiyo yanayofanya matuta yaonekane kuwa ni uchafu, karaha nk wakati kuna kaupande kake ambapo kwa kweli matuta yamesaidia sana (angalia Chalinze - Segera na ile ya Segera - Arusha) kupunguza watu kugongwa. Hii inapelekea kuona kwamba tatizo sio matuta ni regulation ya matuta yenyewe. Nani anahusika hapa, ni wale watendaji!!!
 
Maswali ya kizushi (mnamkumbuka yule jamaa anaitwa Seki?):
1. Je, ni kweli kuwa tuna Traffic Engineer kwenye Idara zetu (TANROADS/MoW)?? I mean a Traffic Engineer sio Highways Engineer!!

2. Je, kuna Traffic Safety Audit yoyote imefanywa kwenye mabarabara yetu yote yanayojengwa na ambayo yameshajengwa?? Ni lini na inaonyesha nini?? Chanzo cha ajali nyingi ni nini??

3. Je, katika sehemu zilizowekwa matuta ajali zimepungua au zimeongezeka??

Ukishajijibu hayo maswali then tunaweza kuangalia way ahead lakini otherwise kubakia kuyakataa matuta ni sawa na kusema "Sizitaki mbichi hizi" wakati ukijua kuwa ndizo pekee zilizopo!!! Tukumbuke hii ni Bongo na kitu kinaitwa "Studies/Research etc" ni wmbo usiokuwa na mwenyewe.... Sijaongelea uwajibikaji!!!

Mungu Ibariki Tanzania na Watu wake!!!
 
Unapokwenda kwenye event halafu ukawa huna cha kuongea, sio lazima uongee! Silence is golden. Sikutegemea rais akaongelee masuala ya matuta ya barabarani hadharani.

Mbona kuna mambo mengi sana ya msingi ya kufanya jamani!!!!

Mkuu Masaki, umeshakwenda kwenye mikutano ya hadhara vijijini?? Najua ni ngumu kuamini lakini kwa kweli kuna sehemu watu wanachinjika haswa na magari yanayoenda mbio especially watoto wa shule na hivyo wazazi na wengine kwenye vijiji hivyo kero zao (among many) ni kuwekewa matuta ya kupunguza/kudhibiti mwendo wa kasi kwa madereva wakiwa kwenye maeneo ya vijiji!!! Kwa kweli yanaongelwa na nina uhakika JK did not just jump up and say it bali lazima kuna Mwananchi alimweleza/alilalamikia jambo hili!!!

Tembea uone na kusikia mengi ndipo utaweza kujua extent ya swala hili Mkuu!!!
 
Nakuelewa sana, Mhandisi Morani. Ni muhimu kuwa na hizi stop gap measures. Sawa kabisa. Lakini cha muhimu zaidi ni hilo ulilolizungumzia za takwimu (na ripoti) za ajali. Bila kuwa na utamaduni na taratibu za kufuatilia kiini cha matatizo na kuchukulia hatua za dhati kuyaepuka, hatutafika mbali. Lengo lisiwe kupunguza ajali bali kuzitokomeza kabisa. najua hii haiwezekani lakini liwe lengo ili tuwe na ajali chache inavyowezekana. Na hii haitawezekani kama hatutachukua hatua za dhati kuhakikisha kuwa kuna enforcement ya sheria zilizopo na uwajibikaji pale zinapokiukwa. Hilo la bye-passlinawezekana hasa ukiangalia kuwa barabara zetu nyingi ni za kusaidiwa. Kwa nini tusihakikishe zinakidhi mahitaji yetu na hata ikibidi kuchangia ili zifikie hiyo standard?
 
Nafikiri kuna watu wanadhani kuwa Tanzania hahihitaji vilivyo bora; au kwa maana nyingine Tanzania inastahili vilivyo hafifu tu. Hii ni kasumba ambayo hata viongozi wetu walio nayo huitumia kutuingiza kwenye mikataba hafifu. Wafanya biashara nao wanaitumia kwa kutuletea vitu ambavyo ni substandard. Inabidi tufanye kazi ya ziada kuiondoa ili tuanze kujenga imani ya kuwa "Tanzania inastahili vilivyo bora."

Nasema hivyo kulenga wale wanaodai kuwa Tanzania hahihitaji highways za lane mbilimbili (dual carriageway). Kwa nini tusizihitaji wakati sasa hivi idadi ya magari imeongezeka vile; na vile vile ukizingatia kuwa kama tuna uwezo wa kutupa nje nje vijisenti kwa mafisadi wachache, vijisenti ambavyo kwa pamoja vinaweza kujenga barabara za namna hiyo.

Ingawa hakuna data kamili za ajali za barabarani hapa Tanzania, ukifuatlia taarifa mbali mbali za ajali zinazoripotiwa magazetini zinaonyesha kuwa nyingi za ajali hizi hutokea ama kwenye kona au wakati magari yanapishana. Ajali za namna hiyo zitapunguka sana kama kuna barabara za lane mbilimbili. Pamoja na uzembe wa madereva na ubovu wa magari, sehemu kubwa ya ajali za barabarani husababishwa na uwezo mdogo wa barabara zenyewe. Kumbukeni tunaongelea katika kipindi cha takriban nusu karne ya uhuru.
 
Bro Morani nimekuwa nakukubali hata huko nyuma ktk posts mbalimbali zinazohusu Ujenzi...wengine hapa tutapinga kwenda Mbele hata kama ufafanuzi umetolewa...

Binafsi si mtaalam wa Ujenzi, ila bahati tumeona namna Highway zilivyo....may be ktk perspective tofauti...

Tukisema Matuta yasiwepo, basi Highway ziwe Njia 2 separated na UZIO...{manzese town umeweka uzio, watu wanaiba...}then wapita kwa Miguu wawekewe njia za chini au Juu ili waweze pita kila Mahala ambapo kuna population kubwa...either Kijiji etc...kwa utaratibu wa sasa wa barabara moja...Madereva walevi...sijui sie tunashauri nini....

Tanzania tuna mengi ya kujirekebisha.....Hatuna kawaida ya kutii TARATIBU zilizopo, RUSHWA, WIZI wa aina zote...bado ni maradhi sugu ktk Tanzania Huru.
 
Hatuna Traffics Engineers....ila wapo baadhi ya wabongo wameshaona hilo Gap...na sasa wameanza kukamua...sina hakika wangapi ila friend of mine yupo Amerika anakamua hii...Ukifuatilizia ktk matangaz ya kazi ktk nchi za Ughaibu...hawa wataalam wa Traffic Engineerng wapo in demand sana...

Morani bahati mbaya iliyopo ktk system zetu, waliopo ktk Mamlaka TANROAD hawapo tayari kusikiliza mawazo mapya hata nyie ma-engineer vijana...
 
Kichuguu, kwa kweli mimi binafsi ni wale wanaopendelea sana nchi yetu ipate the best there is in kila kitu. Lakini hii ni only a wishfull thinking considering our actual situation. Lakini kuendelea kuangalia yale yanayosaidikika na kuacha watu wetu waendelee kuteketea na ajali sidhani kama ni sawa.... Hivyo tunapojaribu kutetea sio kwamba tumekubali kushindwa bali ni kama Fundi Mchundo hapo nyuma aliposema kwamba all we need is to have a stop gap measure lakini sio kulala bali kuendelea na nguvu zetu zote kutafuta chanzo na kulimaliza tatizo husika!!

Mkuu Chuma, hilo la ajali zetu hata huko kwenye njia kubwa pamoja na ufinyu wa barabara tukumbuke kuna madereva wazembe kama ulivyosema, kuna madereva wanaondesha under the influence (mirungi, goto etc) nk... Aisee kama kuna vijana wameingia kwenye hili la "Traffic Engineering" watakuwa wamepiga bingo lakini tatizo wote tunaelewa kuwa since hao wataalamu wanahitajika sana duniani na ukiangalia kipato cha hapa Bongo unadhani watarudi?? Ukumbuke pia kuwa wakati huu watu wengi wanajisomesha wenyewe tofauti na enzi zetu amabpo serikali ilikuwa inatusomesha hivyo hao wanaweza kusoma ndio lakini kurudi na kufanya kazi hapa nyumbani kwa kamshahara ketu..... Sijui!!

Asante Mkuu, kweli mimi ni Kijana na wa zamani!!! Ha ha haaaa!!! (joking)
 
Tanzania tunapenda kila kitu kijifanye chenyewe.Mfano,unaweza ukawa unapita Salender bridge na kukuta taa za barabarani hazifanyi kazi,lakini utaona kuna traffic police wawili wako pembeni wanasimamisha magari kucheki kadi na insurance!
Nenda Kawawa road Kinondoni pale kwenye junction na Mwananyamala road,taa zinafanya kazi lakini madaladala hayazifuati kabisa,na ni tatizo la siku nyingi sana hilo,kama ni mgeni hapo unaweza kupata ajali.Traffic police wanajua lakini huwezi kuona yupo pale hata mmoja.
Matuta yameharibu barabara nyingi sana hapa dar.Shekilango ilikuwa haipitiki kwa sababu ya matuta yalivyoiharibu,wametengeneza barabara na matuta yamerudi tena!Mbezi hivyohivyo.
Sasa kama ni ku over speed,mbona tunashikwa Mlandizi au Kwa Mathias sijui na matraffic police,lakini mjini hapa husikii hata siku moja dereva kashikwa kwa kuoverspeed? Infact,kama traffic police anaongoza magari,utaona anakuita kama uko mbali uende haraka,kama pale Kinondoni road kuingia Ali Hassan.Nilishashuhudia mama mmoja hapo akifuata jinsi anavyoharakishwa na askari akajikuta akipamia zege upande wa bahari.
Hii nchi tatizo ni kwamba kila kitu ni dili.
 
Mkuu Chuma, hilo la ajali zetu hata huko kwenye njia kubwa pamoja na ufinyu wa barabara tukumbuke kuna madereva wazembe kama ulivyosema, kuna madereva wanaondesha under the influence (mirungi, goto etc) nk... Aisee kama kuna vijana wameingia kwenye hili la "Traffic Engineering" watakuwa wamepiga bingo lakini tatizo wote tunaelewa kuwa since hao wataalamu wanahitajika sana duniani na ukiangalia kipato cha hapa Bongo unadhani watarudi?? Ukumbuke pia kuwa wakati huu watu wengi wanajisomesha wenyewe tofauti na enzi zetu amabpo serikali ilikuwa inatusomesha hivyo hao wanaweza kusoma ndio lakini kurudi na kufanya kazi hapa nyumbani kwa kamshahara ketu..... Sijui!!

Asante Mkuu, kweli mimi ni Kijana na wa zamani!!! Ha ha haaaa!!! (joking)
Wachangiaji,
Samahani nilisafiri kidogo na kuacha mjadala ukiendelea. Moran umesema jambo ambalo pana wakati niliandika yaani umuhimu wa hawa TRAFFIC ENGINEERS. Hapa nilipo wakati nikiwa shule alikuwepo mzee mmoja mwenye Masters na chini yake kijana mwenye PhD. Ila hadi leo hii anamwita jamaa BOSS. Hii field inahitaji sana UZOEFU na si KUMALIZA SHULE. Hawa vijana hata wakimaliza itawachukua muda mrefu sana kuanza kuwa "Washenzi" wa hiki kitengo. Vinginevyo MACHINJIONI Tanzania yatakuwepo siku zote. Nikiwa na project naye, nilidesign taa za barabarani kwenye T-Junctions. Nikaamuru kwanza magari yaendeyo DIRECT na baadaye nayasimamisha ya upade mmoja na kuyaruhusu yanayokata kushoto(Right side drive). Nilipomuona akasema "Utafanya machinjioni". Hadi leo sielewi kwa nini alisema hivyo ila nafikiri ni uzoefu wake wa kujua tabia za watu. Hata mzee mwingine mkali wa HIGHWAY (PhD) alikubaliana na mimi kwa proposal ya kwanza ila niamueleza mzee wa Ms. kasema nibadili akasema "Kama yule bwana kasema hivyo basi ndivyo ilivyo". Yeye alisema kuwa "Kwanza unaruhusu yanayokata kushoto, na ndipo baadaye unaruhsu yote yanayokwenda direct.
Nafikiri Tanzania wakati tukisubiri hawa wamalize, ingelifaa kutafuta Watanzania hata waishio nje na wako tayari kuisaidia Tanzania na kufanya nao kazi kwa karibu so longer ni ma-Traffic Eng. wa muda mrefu. Naitamani sana hii field ila niliikimbia kwani ni ngumu sana. Pia twaweza tumia hata ule UTUNDU wa kuwapa hawa WANAFUNZI kazi zao ziwe zinatoka Tanzania wakati huo wao wanasoma nje. Tutawatumia Maprofesa wao na wakati huo huo tunaanza tayari kusolve matatizo yetu. Nafikiri kukimbilia kuweka MATUTA, kujenga hospital Tumbi nk nk ni kuiingilia kazi za watu yaani ambazo sisi wote hapa hatutakiwi kuzifanya. Ila heri nusu shari kuliko shari kamili, Morani andeleeni kusaidia hadi wataalamu watakapopatikana. Pia hawa TANROADS lazima wawe wanatunza DATAS zote za ajali na kuweka kila kitu kama sehemu, aina ya gari, chanzo, saa ngapi, maoni ya POLISI, nk. Hii ni muhimu kwa hao wahandisi kutafuta vyanzo na solutions hata kama wanasoma USA, China au Hungary. Pia picha za eneo hilo na hali ya hewa ya hapo wakati wa ajali ........
Mwisho ikiwezekana basi lianze kufundishwa vyuo vikuu vya ufundi hapo hapo Tanzania kwani kusema ukweli halihitaji vifaa vingi na vya kutisha. MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Back
Top Bottom