Rais awaonya wakuu wa mikoa na wilaya maeneo yao yatakayofanya vibaya kwenye zoezi la kuandikisha wapiga kura

Binafsi hata kwenda sijaenda manake sijajua wanajiandikishia wapi kwa mtaani kwangu
 
..kujiandikisha na kupiga kura ni suala la HIARI.

..kauli hii ni kana kwamba Mzee anataka wakuu wa wilaya watumie NGUVU / AMRI kuhakikisha wananchi wanajiandikisha kupiga kura.
 
Maeneo yanayoongozwa na chadema wananchi wagoma kujiandikisha kupiga kura
 
Hata sijafikiria ,Sina hata mpango
miaka ya nyum nilikuwa nikimhimiza mke wangu, jirani zangu na vijana wenzangu kujiandikisha na elimu ya kupiga kura, mwaka huu niko vize na kujitafutia mkate wa wanangu, sisikii hata mtaani mtu aneongelea zoezi la uchaguzi.
 
Aliwaonya wasitangaze ushindi kwa wapinzani, watu wamegoma kujiandikisha, amerudi kuwatishia tena acha wararuane wenyewe siku ya uchaguzi mie nitaomba mwanangu anioneshe katuni na wasifu wa wahusika, kuliko kwenda kupiga kura.
 
Ngoja tuone watakavyojiongeza. Maana muda hakuna tena wa kurekebisha hiyo blunder ili wasitumbuliwe “ule usaa”😀

Msishangazwe kuona kuna maeneo yenye wapiga kura wengi kuliko waliojiandikisha kupiga kura!
 
Naona chama cha kijani kina andaa ushindi wa mezani
Maana kinatengeneza mazingira ya vitisho ili matokeo yaje yafanane na uhalisia
 
Kama Rais anaona anakubalika sana vitisho vya nini? Yeye ndio amesimamia kunajisi hadhi ya uchaguz katika taifa hili sasa anamuonya nani wakati alitakiwa ajionye mwenyewe kwa kushindwa kusimamia katiba vizur.
Ni Rais huyu huyu aliyetamka hadharani kuwa atashangaa mtu aliyemteua yeye amtangaze mpinzani ...
Tatizo la Rais wetu ni unafiki na wananchi wanampa meseji kuwa hawana hata haja ya kuchagua kwani hata wakichagua haitasaidia chochote na mshindi atatangazwa aliyepanga na sio alieyechaguliwa.
 
Back
Top Bottom