Rais aunde tume mbili kuchunguza shutuma za watu kudhulumiwa mali zao awamu iliyopita pamoja na kifo cha Hayati Dkt. Magufuli

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
43,742
2,000
Nimemsikia Raia Samia anasema watahakikisha wanakusanya kodi halali na sio ya dhuluma na huko nyuma amekemea TRA kunyang'anya watu mitaji na hela zao kwa kisingizio cha kodi.

Hapa tuseme ukweli kuwa tuhuma kuwa miaka mitano iliyopita watu 'wamedhulumiwa' na kunyang'anywa hela zao' zimezagaa sana.

Sasa je, ukweli ni upi?

Waliofanya hivyo walipokea kweli maagizo kutoka juu au wengine walisingizia 'maagizo kutoka juu'kuendesha ujambazi?

Nafikiri hili ili tuweze kulijua ukweli wake ingeundwa tume ya kuchunguza na kuweka ukweli wote wazi ili ijulikane kiasi gani kilidhulumiwa, kilienda wapi?

Kina nani walihusika? Walipewa kweli maagizo au walifanya ujambazi tu wenyewe? Tume iwe ya wazi kabisa na media ziwepo wakati watu wanahojiwa.

Ingine ni Tume ya kuchunguza kifo cha JPM.

Je, ingewezekana kuepuka?Kulikuwa na uzembe? Mkono wa wa mtu? Kama mkono wa mtu walikuwa wanataka nini? Wapo wapi?
  • Kama ni uzembe, je tumeweka mazingira ya kutukutokea tena uzembe huo?
  • Zilikuwepo tetesi aliwahishwa Nairobi dakika za mwisho. Je, why Nairobi?
  • Why hizo facilities za Nairobi hazipo hapa nchini huko Mzena au Muhimbili?
  • Nani anahusika na uzembe huo?
  • Lolote la kujifunza? La kulifanyia kazi?
Binafsi naona hizi tume mbili ni muhimu mno kama kweli kama Taifa tumedhamiria kwenda mbele bila kurudi nyuma, vinginenevyo historia ina kawaida ya kujirudia.

Tujifunze. Turekebishe
 
Ryaro ryaro

JF-Expert Member
Feb 10, 2021
326
1,000
Hizi tume unazozisagest hazina manufaa kwa Taifa vyvyote na kwa matokeo yoyote yatakayotoka. Wastage of time and scarse resources we have. Tusonge mbele yaliyopita basi
 
Bengal

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
5,072
2,000
Wakati mwingine kutochimbua makaburi kuna manufaa kwa taifa.
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
42,559
2,000
Sioni huyu mama akiweza hayo matamanio yako, kuna ripoti ya BoT mpaka leo imeshindakana kuwekwa hadharani. Hilo la uchunguzi kuhusu sababu ya kifo cha Magufuli ndio haliwezekani kabisa, maana hatujafikia kuwa taifa la uwazi wa hivyo, Magufuli mwenyewe akiwa mmoja wa kutoamini uchunguzi wa uwazi, rejea shambulio la Lisu.
 
Ndahani

Platinum Member
Jun 3, 2008
17,591
2,000
TRA nafikiri ni sahihi ili turudishe confidence kwa wafanyabiashara na wawekezaji. Wengi walikuwa wanaburuzwa kwa ubabe tu.
Ila kifo ni kifo. Hakuna lolote linaweza kufanyika. Tuachane na hizi mada ambazo zinaweza kuligawa Taifa na kuleta chuki. Tugange yajayo
 
Bantugbro

JF-Expert Member
Feb 22, 2009
4,429
2,000
Naunga mkono juu ya hoja ya uwazi, lakini inaonekana haitawezekana leo, but mambo hayo sio lazima yafanyike ktk awamu ya 6, yanaweza kufanyika hata awamu ya 7 au ya nane. Tumeona nchi nyingine zikifanya hivyo na matokeo yake huwa ni matatizo zaidi.
 
Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
12,690
2,000
Ni kweli tume ni kupoteza muda tu.
Katiba mpya iliyo imara na bora ndio suluhisho la kudumu.
Hizi tume unazozisagest hazina manufaa kwa Taifa vyvyote na kwa matokeo yoyote yatakayotoka. Wastage of time and scarse resources we have. Tusonge mbele yaliyopita basi
 
dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
15,221
2,000
... moja ni muhimu sana; nyingine haina maana; ni kupoteza muda na resources tu.
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
121,226
2,000
Mama kanyuti kuhusu ripoti ya BoT labda wameshamtisha wahuni maana waliomo ndani ya Baraza lake la Mawaziri ni wahusika wakubwa wa hilo sakata la kujichotea mabilioni eti ya kumtibu mwendazake wakati alishajifia tangu March 11 lakini akaendelea kuwekwa kwenye life support baada ya kuambiwa hatafufuka ndiyo wakaamua kututangazia rasmi kwamba dhalimu is no more siku sita baadaye March 17, 2021.
Sioni huyu mama akiweza hayo matamanio yako, kuna ripoti ya BoT mpaka leo imeshindakana kuwekwa hadharani. Hilo la uchunguzi kuhusu sababu ya kifo cha Magufuli ndio haliwezekani kabisa, maana hatujafikia kuwa taifa la uwazi wa hivyo, Magufuli mwenyewe akiwa mmoja wa kutoamini uchunguzi wa uwazi, rejea shambulio la Lisu.
 
Uttarra

JF-Expert Member
Jan 5, 2019
468
1,000
Wakati mwingine kutochimbua makaburi kuna manufaa kwa taifa.

We learn from mistakes, sheria hutungwa kutokana na udhaifu au matukio.

Huoni kuchimbua haya makaburi kunaweza kuwa na faida in future, haujalishi matikeo yatasema nini, lkn lazima kutakua na kujifinza kama hizo tume zitakua huru na zitatenda haki kwa kufanya uchuncguzi wa kina.

Kutochimbua makaburi ni sawa na kukubaliana kuendelea kuwa katika status quo.
 
kizaizai

JF-Expert Member
Mar 31, 2010
4,150
2,000
Waliodhulumiwa nawaomba wasahau, wamwombe MUNGU awatie nguvu, maana kamati ya wadhulumu bado ipo kwenye uongozi. Navyoona Mama kanogewa na mapeema kaanzankutengeneza mazingira ya 2025.
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
121,226
2,000
Easier say than done especially when you take into consideration that they took billions of your hard earned money and left you with NOTHING.
Waliodhulumiwa nawaomba wasahau, wamwombe MUNGU awatie nguvu, maana kamati ya wadhulumu bado ipo kwenye uongozi. Navyoona Mama kanogewa na mapeema kaanzankutengeneza mazingira ya 2025.
 
kalonji

JF-Expert Member
Feb 17, 2021
6,165
2,000
Wapo wezi wanaonekana kwenye ccctv camera za bureau de change wakikwapua Pesa kwa kigezo cha uhakiki five years now imepita labda tuwaulize ni lini watamaliza uhakiki wa hizo pesa Ili wazirejeshe kwa wamiliki.
 
kalonji

JF-Expert Member
Feb 17, 2021
6,165
2,000
Hizo tuhuma za kifo ni uzushi tu man.Hivi kwa ulinzi wote ule ikiwemo helicopter angani kama tupo iraq hio nafasi wangepatia wapi.
Mwache Mungu asikie maombi ya wengi yaliyofanana.
 
kizaizai

JF-Expert Member
Mar 31, 2010
4,150
2,000
Easier say than done especially when you take into consideration that they took billions of your hard earned money and left you with NOTHING.
Nikweli kabisa, ukishaona teuzi kama ya Mwigulu unategemea nini? Ndio ujue wale walio inner circle bado wapo kazini. Pesa inatafutwa ni kukomaa tu, na kupambania uhai.
 
  • Love
Reactions: BAK

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
12,495
2,000
Hizi tume unazozisagest hazina manufaa kwa Taifa vyvyote na kwa matokeo yoyote yatakayotoka. Wastage of time and scarse resources we have. Tusonge mbele yaliyopita basi

Hata waliodhulumiwa nao wanasema yaliyopita basi?

Kweli mzigo wa mwenzio kwako ni kama kanda la Sufi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom