Rais atatueleza nini Uhuru bila majibu kuhusu wizi?

fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,448
2,000
Kwa vile nchi sio mali ya mtu, na kwa vile cheo ni dhamana tu, na kwa vile CCM na serikali yake ni wasikivu, na kwa vile bunge limekwishajadili na kutoa maazimio yake, na kwa vile ni haki ya waTZ kujua nini kinaendelea sakata la ESCROW.

Uhuru na maadhimisho ya siku ya UHURU wa Tanganyika ni siku mwafaka kwa Rais na amri jeshi mkuu kutoa minongono ktk maisha ya watz kwa kuongea kwa kina suala hilo na pengine kuchukua hatua kwa wahusika.

Najiuliza tu rais bila kusema escrow na kutekeleza maazimio ya bunge ni nini atawambia watz wamshangilie? au atanunua watu wenye njaa ya akili kumshangilia na kuhadaa umma kuwa anashangiliwa? au wataleta story za ajabu kama kiuengua wagombea wa UKAWA zaidi ya mia tano wakizani amani inapatikana kwa kunyonga haki, tena mchana kweupe?

Rais atasema nini iwapo kesho itafika bado watuhumiwa wa escrow wakitumia magari na mali za umma?? Maswi, Tibaijuka, Werema, Muhongo, Masele, Saada, Mwigulu, Kigoda, Mawe matatu??

Uwezo na uelewa wa JK sasa kwenye mizani tena pana sana. Wananchi wako nyuma ya bunge, kweli inafahamika bunge linawakilisha wananchi wala sio mahakama. Wananchi wanataka kuona kwa vitendo kuwa rais sio mtu wa kupuuza mambo makubwa ya taifa, rais sio shwaiba wa waharifu wa aina yoyote.

Je rais ameona nini na raha gani kukaa na suala hili zaidi ya wiki mbili sasa???

UHURU bila majibu japo kwa maazimio ya bunge ni fedheha nyingine wa umma.

Nawasilisha
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
12,494
2,000
In fact ndio mara yake ya mwisho kuhudhuria sherehe za uhuru wa Tanganyika kama Amiri Jeshi Mkuu.
 

JohnShaaban

JF-Expert Member
Aug 23, 2007
464
195
Mkuu usipoteze muda wako, wala hatatokea...

Anasubiri wachakachue matokeo ya Serikali za Mitaa ndio aongee na wazee wa DSM. Hapo itakuwa full mipasho kujustify kuwa Wananchi wanaunga mkono serikali ya WIZI ya CCM.
 

Manumbu

JF-Expert Member
Oct 28, 2009
1,749
1,195
In fact ndio mara yake ya mwisho kuhudhuria sherehe za uhuru wa Tanganyika kama Amiri Jeshi Mkuu.
what a relief to start seeing this guy going! these lost 10 years in my life aer really lost! I wouldnt wish a single month to be added on!
 

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
12,918
2,000
Rais anaumwa yuko katika likizo ya ugonjwa kwa miezi 3 baada ya hapo atakaporipoti kazini ndio wamletee maazimio ya bunge ili aone kama anaweza kuwasamehe, warudishe, awawajibishe au awaminyie hadi wastaafu kama wale wa Richmond ambao hakuna aliyewajibishwa ila rais aliwaacha walistaafu kwa heshima
 

FbUser

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
328
250
Siku ya uhuru hakuna hotuba. Ni ukaguzi wa gwaride wimbo wa taifa baadae usiku ikulu kuku juice za baaresa na nyagi nyingii kushne babujiii
 

fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,448
2,000
Hakuna dawa hospitalini tunatumia bilions kushereheka bila mpango, huu uhuru si tungesherekea after 20years kupunguza matumizi kwa nchi maskini
 

fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,448
2,000
Kwanza kuwa na sherehe hizo ni kutukuza ukoloni, tunataka mambo mabaya yafutike hata machoni mwetu, sio kila mwaka sherehe kutukuza ukoloni na mambo yao. NCHI MASKINI ingeweka vibaumbele vingine kama madawati, maabara na dawa kwenye hizo bilioni 8 kila mwaka. PINDA tuambie akili yako inasemaje kuhusu hili
 

MTK

JF-Expert Member
Apr 19, 2012
8,264
2,000
Kesho hata kama JK (bado anauguza jeraha la upasuaji) atahudhuria maadhimisho ya uhuru hawajibiki kutoa hotuba; anaweza kukagua gwaride na kuangalia burudani zitakazofuata na kuondoka tu basi.
Tumpe muda; ukizingatia kwamba Escrow imegusa watu wengi na bado wengi wengine wanazidi kuingia kwenye tuhuma; itamchukua muda kiasi kupata watu ambao "angalau" wanaweza kudumu hadi bunge la bajeti lijalo! CCM iko ICU; kupata watu 5 safi ni kama ngamia kupita kwenye tundu la sindano! hata wale "wanaovumilika wachache"; bado wahafidhina wa CCM na mafisadi hawawezi kuwapa nafasi kwa kuogopa kuumbuliwa ndio maana walifinyanga mchakato wa katiba ili wasibanwe.

Kwa mfano watu kama Serukamba; Kangi Lugora; Luhaga Mpina; Ester Bulaya; James Lembeli; Keissy, Deo Kunjombe; Chris Sendeka na wengine kama hao; sitegemei kama wataungwa mkono katika kazi zao hata kama JK anaweza kuwa jasiri akawateua kuwa mawaziri; sitegemei kabisaaaaaa!

MaCCM waliobaki ama ni mafisadi; au outright thieves na majangili au ni praise singers na wachumia tumbo tu ndio maana Mura wetu Werema alipomuita David Kafulila Tumbili walishangilia sana na kugonga meza as if alichokisema Muraa kilikuwa kitu cha maana; sasa wanatafuta mahali pa kuficha sura zao kwa aibu baada ya "Tumbili kukamata Mwizi!!"; madalali na makuadi wa wawekezaji matapeli kina Sethi kuumbuliwa!!!
 

commonmwananchi

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
3,116
2,000
haya ndio maoni yangu:

kikwete anaujua mchezo wote na hii sio siri,watanzania wote tunashawishika kuamini hilo, hii ni kutokana na taarifa ya cag na pac iliyosomwa bungeni.

serkali imecheza rafu kwenye mfumo mzima wa uchaguzi wa serikali za mitaa,kikwete na ccm wanalijua hilo na mkakati mzima.walichlkifanya ccm na kikwete wameamua kukaa kimya kwa kuhofia kuwaharibia wagombea wao wa chaguzi za serikali zamitaa kwenye kampeni hizi zilizominywa muda na kuwapa ccm nafasi kufanikisha mkakati wao wa mapingamizi haramu ya wagombea wa ukawa
salsa kesho atahutubia kwanza kwa kuwashukuru watanzania kwa kumuombea wakati wote wa ugonjwa na matibabu na kusema salsa ninapata ahueni na muda sio mrefu nitarejea katika hali yangu ya kawaida
baada ya hapo atawaahidi watanzania kuwa atalishughulika suala la escrow bila kumuonea
mtu
 

fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,448
2,000
Lini zilikuwepo dawa hospitalini?.
Tukitumia fedha na mali tulizonazo vizuri, wezi wa epa escrow sherehe za bilion 65 kama ile ya miaka 50 ya uhuru zikifutwa pesa hizo ni nyingi kila mwaka sherehe za uhuru, what is it bwana, tufanye kila miaka 20 kama kumbukumbu tu na sio kutukuza ukoloni kwa kila mwaka tushereheka na mambo yao
 

fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,448
2,000
Sio vema kuendesha nchi kama mali binafsi, tunataka kauli ya rais juu ya wizi hawa. Tunajua tunawalipa usalama kutoa ripoti kila siku kwa rais, iweje hakuna majibu ya ripoti zao hakuna utekelezaji wa maazimio ya bunge, je rais akikaidi maazimio ya bunge bado bunge linakuwa na uwezo wa kusimamia serikali??? au ni mbwa asiyekuwa na meno???
 

Daata

JF-Expert Member
Dec 24, 2012
4,516
2,000
Hivi mapendekezo ya bunge yakishapita yanachukua muda gani kutekelezwa na mamlaka husika?
 

Asante

JF-Expert Member
Dec 18, 2009
2,086
2,000
Mkuu usipoteze muda wako, wala hatatokea...

Anasubiri wachakachue matokeo ya Serikali za Mitaa ndio aongee na wazee wa DSM. Hapo itakuwa full mipasho kujustify kuwa Wananchi wanaunga mkono serikali ya WIZI ya CCM.
Samweli Sita atatunukiwa nishani ya heshima ya Mt. Kilimanjaro kwa ujasiri wake wa kufanikisha kupatikana kwa katiba mpya
 

fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,448
2,000
Uhuru wa nini kesho ile hali mali zinaibiwa kama hatuko huru, kama nchi haina serikali? kumbe serikali ya JK ni safari na sherehe tu
 

Tetty

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
26,386
2,000
fikirikwanza,unasubiri hotuba ya Tembo mkubwa,pole ngoja nikupe hint ya hotuba ya kesho:

1.Itahusu wapinzani kuwa wanapenda sana uongozi mpaka kiasi cha kusingizia wizi wa escrow.
2.Serikali ya CCM ipo makini sana na itafanya kila iwezalo kuifanyia kazi ripoti ya CAG na PAC.
3.Uchaguzi wa serikali za mitaa watanzania jitokezeni kwa wingi mkapige kura.
4.Itahusu ugonjwa wa Tembo mkubwa,amerudi salama na ameshauriwa apumzike miezi mitatu,maana operation ilikuwa kubwa sana na ilifanikiwa kwa kiwango kikubwa,na watanzania muwe mnaenda kupima afya zenu maana vipimo na matibabu vyote vinapatikana kwenye hospitali zetu.
4.Katiba ya MAFISADI ndiyo tumeiona iko bora sana maana viongozi wataweka pesa zao wapi wakati hapabongo hakuna bank za kuweka pesa za wizi kama escrow account.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom