Rais atambue, trumped-up charges ni ugaidi na uhujumu uchumi wa kweli

Pulchra Animo

JF-Expert Member
Jun 16, 2016
3,398
2,990
Mbowe na wenzake watatu wamekaa gerezani kwa at least miezi minane na mahakama imesikiliza kesi dhidi yao kwa at least miezi mitano mfululizo. Out of the blue, leo Mbowe na wenzake wameachiwa huru na mahakama kwa entry ya nolle prosequi iliyofanywa na DPP.

Hizi harassments zinazofanywa na Serikali kwa watu wasiokuwa na hatia ni ugaidi usiokuwa na chembe yoyote ya mashaka. Vilevile, hasara zinazosababishwa na Serikali kwa kuwaweka gerezani watu wasiokuwa na hatia na kutumia muda na resources nyingine nyingi kuendesha kesi dhidi yao ni uhujumu uchumi usiokuwa na chembe yoyote ya mashaka.

Nguvukazi (productive workforce) iliyopoteza muda kwenye kesi ya Mbowe na wenzake ilikuwa kubwa sana. Ukiachilia mbali wanasheria na watumishi wa mahakama ambao jumla yao hawapungui ishirini, kuna watu wengine wengi walikuwa wakiacha kazi zao na kwenda mahakamani kufuatilia hiyo kesi.

Kwasababu kesi imehusisha watu wengi wenye specialized knowledge and experience, naamini kwa wastani, hasara kwa siku kwa mtu mmoja ilikuwa haipungui laki moja. Kama, kwa wastani, kulikuwa na watu hamsini kila siku ya kesi, maana yake, taifa lilikuwa linapoteza kiasi kisichopungua shillings million tano. Hasara hii imeendelea kwa siku zisizopungua mia moja. Kwahiyo, kadirio langu la chini la hasara iliyosababishwa na kesi hii ni shillings nusu billion. Hiki sio kiasi kidogo cha pesa. Kinatosha kujenga kituo cha afya cha kisasa.

Nimalize kwa kusema, magaidi na wahujumu uchumi kwenye hii kesi walikuwa Rais na Serikali yake. Ni dhahiri kwamba umma wa Watanzania unayo kazi ya kufanya kulimaliza hili janga katika nchi yetu!
 
Nauona mpambano wa Uchawa Utakaopamba Moto kwa Ccm kati ya Chadema na Act-W.
.
Kila mtu atajipendekeza kwake, kila mtu ataomba kukutana na Chief State House.
.
Kila Chama kitataka kiwe mtetezi wake.
.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tukiachana na hii Katiba ya ccm ya mwaka 1977, naamini haya madudu kama hayatapungua, basi yataisha kabisa. Na polisi wetu hawataitwa tena policcm.
Katiba mpya haikwepeki,tunahitaji Katiba Bora ya Wananchi ambayo itatokana na Rasimu Warioba iliyojadiliwa na kupendekezwa na wananchi.
 
Back
Top Bottom