Rais asiye dhaifu ni malaika. Upuuzi wa CCM umefanya Tanzania kuwa maskini wa kutupa hadi Leo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais asiye dhaifu ni malaika. Upuuzi wa CCM umefanya Tanzania kuwa maskini wa kutupa hadi Leo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by NtakuwaSikuchukui, Jun 21, 2012.

 1. NtakuwaSikuchukui

  NtakuwaSikuchukui Member

  #1
  Jun 21, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kutoka Usalama wa Taifa,
  Taifa hodari, la kishujaa na Lililoweka mbali Uoga.


  Bungeni juzi mchana muheshimiwa Mnyika alisema Rais jk ni dhaifu, kwa kitendo hicho akaonekana ametukana na kuchukuliwa hatua ya kutolewa Bungeni. Je ametukana? Je neno Dhaifu ni matusi? Jibu: Si kweli neno dhaifu sio tusi, wala lugha chafu bali ni neno nzuri lifahalo kutumiwa mahali popote. Usemapo mtu ni dhaifu, unamaanisha mtu huyo anamapungufu, yapo mambo kwake hayako sawa,haja kamilika katika utendaji wake, yapo mambo mabaya yanamwandama. Baada ya kusema hayo Rais JK ana ujasiri wa kuuambia umma wa watanzania yeye sio dhaifu?.Wote tunafahamu kiumbe asiye dhaifu ni malaika tu. Rais ni malaika? Kwa haraka haraka unaweza sema RAIS NI FISADI tena na ushahidi, lakini kwa sababu unaogopa kuuwawa,utakaa kimya tu, lakini moyoni unasema RAIS NI FISADI.

  VileVile bungeni Muheshimiwa Mnyika alisema ….CCM ni Upuuzi… au. …Upuuzi wa CCM…. Je neno Upuzi ni matusi? Jibu: Si kweli neno Upuzi sio tusi, wala lugha chafu, bali ni neno nzuri lifahalo kutumiwa mahali popote kwa makusudi mbalimbali. Neno Upuuzi linamaana kitu,mtu,jambo,wazo,maoni.n.k hakina/hayana maana,faida,maintiki,uhalali kuwepo,kutumiwa,kutendewa kazi n.k.

  Kwasababu hiyo CCM NI UPUUZI, kwa nini, miaka 50 sasa toka uhuru Tanzania bado maskini wa kutupa pamoja na wingi wa utajiri wa rasilimali kama madini, gesi, maji, misitu, mbuga na vivutio vingi sana vya uchumi. Leo hii Rais Jk na familia yake pamoja na marifiki zake na familia zao, wanaweza wakaona kwa vitendo kwa jinsi wanavyoishi kuwa Tanzania sio masikini. Vipindi Viwili hivi vya uongozi wa Rais JK umehalalisha na kutoa Hati miliki kwa mafisadi kuwa TANZANIA NI SHAMBA LA BIBI, waibe watakavyo kikubwa wawe karibu na Rais tu, vinginevyo utaishia jela.

  Wengi wetu kajamba nani,ugali konzi na mboga picha ya samaki, tunaona wazi wazi Tanzania ni maskini na Dunia inashuhudia hivyo hivyo kwa kutazama mambo yafuatayo;


  • Watu wanashindia mlo mmoja au kukosa kabisa. Bidhaa sokoni hazishikiki.
  • Maskini wengi wazidi kuwa maskini……na matajiri wachache wanazidi kuwa matajiri = kwa kasi kubwa
  • Deni la Taifa kwa kasi kubwa linazidi kuengezeka na kuongezeka huko ni kulipana mishahara minono, posho, kuendesha magari ya kifahali,kupewa nyumba bure, umeme bure,maji bure n.k.
  • Madini na Rasilimali nyingine zinaibwa kwa wingi na kubaki danganya toto kulipa kodi ndogo Serikalini.
  • Misamaha ya kodi mikubwa ya matrilioni ya fedha kuendelea kutolewa hadi leo.Nchi maskini eti ina misamaha ya kodi kiasi hichi? Wizi mkubwa huu!.
  • Mafisadi wakubwa kesi zao kuendelea kuogopwa na TAKUKURU, eti TAKUKURU haina fedha za kuwafatilia mafisadi wakubwa, badala yake TAKUKURU iachwe ifatilie kesi za kifisadi za kuanzia laki tano hadi milioni kumi.
  • Huduma duni za afya…….Wanawake wanajifungulia Maporini.

  • UPO HURU KUENDELEZA LIST HII………………….


  Mwisho wito wangu: VIONGOZI WALIO SERIKALINI kama wanandelea funga macho wajue WATANZANIA WAMEBAKIA NA MIEZI MICHACHE UKIMYA WAO UNAFIKA MWISHO, MABOMO YA MACHOZI, POLISI NA JESHI HAVITAWEZA SAIDIA LOLOTE KAMA TUNAVYOONA SYRIA,LIBYA N.K

  RAIS ASIDHANI KAMA ILIVYOKAWAIDA YAKE ATATUMIA PUNDA WAKE(NDEGE) KUKIMBIA NA FAMILIA YAKE.YEYE NA SISI,SISI NA YEYE,AKIMBII MTU,ATOKI MTU……..NGUMI JIWE ASUBUHI HADI USIKU.  MOYO WANGU UNAMAJERAHA MENGI NA MAKUBWA SANA, KUONGEA HUKU KUNAWEZA KUKANIONGEZEA SIKU ZANGU ZA KUISHI HAPA DUNIA, VINGINEVYO NITAKUFA.

  MTANZANIA MWENZANGU CHUKUA MAWAZO HAYA YAANDIKE NA YAPELEKE KILA MAHALI KWA GHARAMA YOYOTE…………..UTAKUWA MMOJA WAPO WALE WALIOTOA MCHANGO KUIKOMBOA TANZANIA YETU……WEWE NI MIONGONI MWA MASHUJAA HALISI WALIOWEKA UOGA MBALI.

  Kutoka Usalama wa Taifa,
  Taifa hodari, la kishujaa na Lililoweka mbali Uoga.
   
Loading...