Rais asiwe mwenyekiti wa chama-Ole Molloimet | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais asiwe mwenyekiti wa chama-Ole Molloimet

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by August, Oct 15, 2009.

 1. A

  August JF-Expert Member

  #1
  Oct 15, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,509
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Kauli inayo takiwa kufanyiwa kazi pia Katibu wa Chama asiwe Pendekezo la Mwenyekiti

  Rais asiwe mwenyekiti wa chama-Ole Molloimet
  [​IMG] [​IMG] [​IMG] Sunday, 11 October 2009 16:33 Edmund Mihale

  MBUNGE wa zamani wa Jimbo la Monduli, Bw. Lepilall Ole Molleimet amesema umefika wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania asiwe mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi kwa sababu wanachama wake wanashindwa kumkosoa, kumshauri na kumdhibiti pindi anapokosea.

  Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Monduli jana, Bw Molleimet alisema angefurahi iwapo katika kipindi kijacho chama hicho kitafanya marekebisho ili anayekalia kiti cha urais asiwe mwenyekiti wa chama kwani chama kwa sasa chama kinashindwa kumkemea au kumpa ushauri pale anapokosea.

  "Nitafurahi iwapo katika siku zijazo rais kama akatoka katika moja ya ngazi yeyote ya chini ndani ya chama ili kusudi chama kiweze kumkosoa na kumwajibisha pale anapofanya makosa kuliko ilivyo sasa kwani rais anapokuwa pia mwenyekiti wa chama inasababisha kushindwa kumkosoa kwa kuwa anakuwa anaogopwa hata katika vikao vya chama kwa kuwa ndiye anaongoza kikao," alisema Bw. Molleimet.

  Luteni Molloimet aliyewahi kuwa mkuu wa wilaya kadhaa, alisema hatua ya kujilimbikizia madaraka ndani ya chama kwa wakati huu ni sawa na kukiuwa na kukifanya kionekane kuwa kimeshikwa na wateule wachache, hali ambayo inasababisha makundi ndani ya chama hicho na kukipeleka pabaya.

  Alisema chama hicho kina mpasuko mkubwa ambao kwa sasa hauwezi kuzibika hadi hapo kitakapozaliwa upya kwani kwa sasa kimepoteza mmelekeo wake kutokana kukifanya kuwa cha kibiashara na kuwatelekeza walengwa ambao ni wakulima na wanfanyakazi wa hali ya chini, tofauti na ilivyokuwa wakati wa Marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

  Alisema hivi sasa chama hicho kimekuwa ni cha wafanyabishara wakubwa ambao wameingia katika ulingo wa siasa kwa kutafuta na kulinda maslahi binafsi na si kwa manufaa ya wananchi waliowachagua.

  Bw Molleimet ambaye amekuwa mbunge wa Monduli kwa miaka tisa kuanzia mwaka 1987 hadi 1995 alimshutumu Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusuf Makamba kuwa anakiharibu chama hicho kuwa kuwarubuni na kurudisha ndani ya CCM kisha kuwapa madaraka makubwa wanachama kutoka katika vyama vya upinzani hali ambayo ni hatari kwa uhai wa chama.

  Alisema hali hiyo inasababisha chuki ndani ya chama hicho katika ya wanachama waliokulia na kulelewa ndani ya chama hicho wakiwa hawana madaraka makubwa hali ambayo ni sawa na kuingiza mamaluki ndani ya chama na kuhatarisha usalama ndini ya chama hicho.

  Bw Molleimet alisema kutoka na kukithiri kwa wafanyabiashara ndani ya CCM, imefika hatua unapozungumua suala la rushwa ndani ya chama hicho unajenga uadui miongoni mwa wanachama ndani ya chama hicho.

  Alisema kuzuka kwa mambo ya ufisadi ndani ya chama hicho yametoka na kuifanya siasa ya Tanzania kuwa ni biashara na ili kukidhibiti suala hilo na kutojilimbikizia madaraka kama ilivyo sasa.
   
Loading...