Rais ashinikizwe na upinzani na wahisani kuwachukulia hatua waliorudisha hela ya EPA

nderingosha

JF-Expert Member
Mar 20, 2011
4,281
3,243
Kama kunakitu chenye kuuma katika nchi hii ni jinsi ambavyo suala la wizi wa fedha za umma linavyoshughulikiwa na uongozi wa nchi hii ya tz. Haingii akilini eti leo rais anasimama anasema wazi eti anashughulikia corruption wakati amewaachia wezi walioiba fedha ya umma bila ya kuwachukulia hatua. Kupambana na rushwa na wizi wa mali ya umma kunaisha pale watuhumiwa wanapofikishwa mahakamani na kuchukuliwa hatua. Mara zote suala la watuhumiwa wa wizi mkubwa nchi hii huwa linamalizika kwa wao kuachiwa kwa kigezo cha kukosekana kwa ushahidi mahakamani. Sasa kama hivi ndivyo, kuna ushahidi gani kwa mtuhumiwa kuzidi pale anaposhikwa na ushahidi? (kwa maana hawa jamaa walirudisha hela ya EPA kwenye mabenki). Inauma sana kwani wakati ule walipokuwa wanarudisha hela ya EPA nilitokea wakati mmoja kuwa karibu na benki moja ya crdb dar na kushuhudia gari ikishusha mzigo wa fedha pale. Nilipompigia jamaa yangu kumuuliza akaniambia hiyo ilikuwa hela ya EPA inarudishwa, nilishangaa ajabu, na nilipo dodosa zaidi nikapata kuambiwa na jamaa yangu wa benki kuwa zoezi zima la kurudisha ile fedha lilikuwa lina hakikiwa na jamaa wa usalama wa taifa. Hii iliniuma sana kwani sijawahi kusikia mambo kama haya kufanyika nchi nyingine yoyote.
Kwa taarifa zaidi ni kwamba, fedha iliyorudishwa ilikuwa nyingi kuliko wanayodaiwa kuiba wale jamaa walioshikwa (e.g Maranda et al).Pia kuna taarifa hela hawa jamaa waliorudisha hawakurudisha yote, sasa kama wanajulikana kwanini wasibanwe na kushikwa?. Habari kamili ni kwamba wale walioshikwa na kufunguliwa mashtaka (e.g Maranda et al) walifanyiwa hivyo kwa kuwa hawakuwa na fedha ya kurudisha au walirudisha kiasi kidogo(cash), pesa yao ilikuwa kwenye miradi na nyingine walishatafuna (mfano Maranda anadaiwa kujengea misikiti Kigoma).

My take: Sasa ndugu zangu tunaishi kwenye nchi gani hivi? tutamwamini vipi kiongozi anae ahidi hivi wakati yeye anafanya vingine? hata mawaziri wake wanaweza kuwa na ugumu wa kutimiza wajibu wao kwa wananchi huku wakijua udhaifu wa kiongozi wao (maana wanajua weakness zake, atawaambia nini?), hata hizi kelele za sijui watu waondoke madarakani wenyewe, hii ni porojo ndugu zangu, hamna kitu hapa, aondoke nani wakati wanajua weakness za boss wao? (kwanza ndio walioshiriki kumweka madarakani).
Watanzania tutapiga kelele oh pesa haitoshi bajeti, sijui miradi haina pesa, sijui wafadhili wamepunguza pesa n.k n.k n.k...........vilio chungu mzima, lakini, kama kweli tunataka mambo yaende nchi hii, basi tuanze na shinikizo la nguvu kwa viongozi wetu wa juu kuwachukulia hatua wale wote wanaotafuna na walioonekana wametafuna hela ya nchi. Kamata wao weka ndani, mbona Sokoine aliweza? kandamiza wao ipasavyo warudishe hela waliyotafuna alafu funga wao ipasavyo. Kufanya hili jambo kunahitaji courage na ugumu wa nguvu na support ya wananchi wote na walinzi, lakini kubwa zaidi kunahitaji nawe kiongozi wa nchi kuwa msafi, sasa kwa status quo tuliyo nayo hili linawezekana? Ni wakati sasa kwa hata nchi wahisani kushinikiza hili jambo maana ndio wanaoleta hela ya maendeleo ambayo inaishia mifukoni mwa wajanja..tafakari
 
Back
Top Bottom