Rais arudi afanye utafiti kabla ya kufanya uamzi wake kuhusu vijana

mpk

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
3,115
3,863
Juzi rais wetu alitoa kauli ambayo inaibua mjadala, alisema vijana hawapendwi lakini amegundua hawapendi rushwa na ni wachapa kazi. Kwa maoni yangu anaweza kuwa amewapima wawili watatu na hajafanya utafiti wa kutosha.

Hivi amesahau yule waziri anayemsubua mpaka akaamua kuanza kuwarekodi mawaziri wake siyo kijana? Lakini pia ukishasema vijana hawapendwi ila ni wachapa kazi hajui anafanya kazi ya kiasiasa ambayo inahitaji moral support? Utawapelekea watu waongozwe au kusimamiwa na mtu hawamtaki? Amejiuliza kwa nini hawapendwi?

Ukiteua wakuu wa wilaya 20 mfano na wakawa hawapendwi kwenye wilaya zao lakini wanachapa kazi, anajua kwamba inayokuwa haipendwi kwenye hizo wilaya ni serikali? Au hajali serikali yake kutopendwa? Au ndiyo maana alisema NICHUKIENI TU......!
 
Sasa mbona umeleta viroja tutajadilije hoja? Utamtoleaje mfano waziri mmoja kijana then ukasema kuwa vijana wote hawafai kupewa madaraka makubwa? Rais wetu kaona mbali hasa kwa mifano ya akina Makonda
 
Wapi nimesema vijana wote hawafai?
 
Ungeckiliza hotuba nzma ungeelew Kwa nn kasem ivo.... Afu c kila kjn atapew wadhfa maana wengne hawana vgezo, kumbuka alisema WAZEE NDO WAMELIFKISHA HAPA TAIFA HILI
 
Anautafta uzee

NDO maana nakwambia ungeckiliza vzr, uendane na kauli zake maana wengne wameckia kwe magazet bas ndo anakuj umu kubish
 
Huwezi kuwapendeza watu hata Mara moja, mfano VIJANA WA KITANZANIA TUNAWAZA KWA NJIA YOYOTE, MTUMBWI, BOTI, MELI AU VINGINEVYO KUZAMIA ULAYA IWE MAREKANI AU UINGEREZA LAKINI KATIKA NCHI HIZO TUNAZO ZAMIA KUNA WATU KATIKA NCHI HIZO HAWAIPENDI SERIKALI YA NCHI HIYO, PIA HATA TANZANIA TUNAICHUKIA SERIKALI WAKATI HUO HUO WAHINDI, WAARABU NA WAZUNGU WANAZAMIA KUCHUMA HUKU NABII WA KWELI ASIFIKIMKWAO
MAGUFULI ANATAFAKARI NZURI SANA TENA ANATUMBUA MAJIPU KWA KUTUMIA AKILI NYINGI SANA, MAANA MFANO ANGETUMBUA WIZARA NZIMA MMOJA SERIKALI ANGESHINDWA KUIENDESHA ANACHOFANYA KILA WIZARA ANAFUKUZA MAJITU MAWILI NGULI YA RUSHWA AU MAWILI WANAOBAKI WANAPOTEANA NA KUSHIKA ADABU
 
Ungeckiliza hotuba nzma ungeelew Kwa nn kasem ivo.... Afu c kila kjn atapew wadhfa maana wengne hawana vgezo, kumbuka alisema WAZEE NDO WAMELIFKISHA HAPA TAIFA HILI

Hivi hapa kama kuna Mtu ambaye hajui Kiswahili ,tuseme anajifunza hii Lugha Akisoma hapa ataelewa kweli? Au atajifunza hii lugha kwa ufasaha? Watu tunajifunza Lugha kupitia njia nyingi ikiwa pamoja na hizi Social Media.
 
Juzi rais wetu alitoa kauli ambayo inaibua mjadala, alisema vijana hawapendwi lakini amegundua hawapendi rushwa na ni wachapa kazi. Kwa maoni yangu anaweza kuwa amewapima wawili watatu na hajafanya utafiti wa kutosha.

Hivi amesahau yule waziri anayemsubua mpaka akaamua kuanza kuwarekodi mawaziri wake siyo kijana? Lakini pia ukishasema vijana hawapendwi ila ni wachapa kazi hajui anafanya kazi ya kiasiasa ambayo inahitaji moral support? Utawapelekea watu waongozwe au kusimamiwa na mtu hawamtaki? Amejiuliza kwa nini hawapendwi?

Ukiteua wakuu wa wilaya 20 mfano na wakawa hawapendwi kwenye wilaya zao lakini wanachapa kazi, anajua kwamba inayokuwa haipendwi kwenye hizo wilaya ni serikali? Au hajali serikali yake kutopendwa? Au ndiyo maana alisema NICHUKIENI TU......!

Mimi nimefikiria mbali zaidi, Raisi ameamua kuweka vijana wapya ili isimpe tabu kuwatumbua watatakapo haribu. Wazee inaamuwia ngumu sana kuwatumbua kwani wako kwenye mfumo siku nyingi na wana network kubwa, jipu moja lina vigogo zaidi ya kumi nyuma yake.
 
Mheshimiwa Rais anazo habari na anajua alikuwa anasema nini. Ni ukweli usiopingika kwamba Vijana ndiyo wenye uchungu na Taifa. Wazee wengi walishalitafuna Taifa wakalipeleka mahututi na hawana tena cha kupoteza maana umri nao umesogea. Japo ni mpango wa Mungu ila, katika hali ya kawaida ya utaratibu wa Mungu, Kila kitu kina mwanzo na mwisho. Mwisho wa wazee kuishi kuko karibu zaidi ya vijana, kama kila kitu kitakwenda sawasawa

Vijana bado wana safari ndefu ya kwenda, wasipokuwa makini safari yao ndefu itaharibika bila kujua. Mfano mzuri ni kwamba hata wazee wasomi wa ngazi ya uprofesa wana harufu ileile ya ufisadi. Taifa likicheka na baadhi ya wazee litavuna mabua.
 
Vijana hawawez kushiriki au kuingia kwenye rushwa na mikataba mibovu. Hivyo naungana na Rais!
Wazee wa nch hii ndio walio tufikisha hapa tulipo
 
Wewe kuna mizee ina miaka 42 haitaki hata kuachia vijana ni kujivutavuta tu ofisini wapishe na wao walipotufikisha imetosha
 
Juzi rais wetu alitoa kauli ambayo inaibua mjadala, alisema vijana hawapendwi lakini amegundua hawapendi rushwa na ni wachapa kazi. Kwa maoni yangu anaweza kuwa amewapima wawili watatu na hajafanya utafiti wa kutosha.

Hivi amesahau yule waziri anayemsubua mpaka akaamua kuanza kuwarekodi mawaziri wake siyo kijana? Lakini pia ukishasema vijana hawapendwi ila ni wachapa kazi hajui anafanya kazi ya kiasiasa ambayo inahitaji moral support? Utawapelekea watu waongozwe au kusimamiwa na mtu hawamtaki? Amejiuliza kwa nini hawapendwi?

Ukiteua wakuu wa wilaya 20 mfano na wakawa hawapendwi kwenye wilaya zao lakini wanachapa kazi, anajua kwamba inayokuwa haipendwi kwenye hizo wilaya ni serikali? Au hajali serikali yake kutopendwa? Au ndiyo maana alisema NICHUKIENI TU......!
Rais anabainisha uchapa kazi na si upenzi na ushabiki, kama hao wananchi watakuwa hawampendi huyo kiongozi ila huyo kiongozi anachapa kazi, tatizo lipo wapi?
 
Naamini alicho sema raisi ni kweli nimetembelea ofisi nyingi wazee wengi wanachokifanya nikukusanya chochote tafikiri mfanya biashara jioni yaani kila pesa lete. Wengne wamechezea ujana sasa wanaona kama ngekewa imekuja mwishoni wanawaza watarudi na nn nyumbani wanaona hawana mpya. Yaani rushwa sana bora Kijana utamweleza akusikie Hawa wazee wengi wao ni noma kwa rushwa na sifa.
 
Uneulizwa yeye ni mzee aua kijana ?
Yeye anataka achukiwe yeye serikali yake ?
Umemtaja makonda kama mfano Wa vijana wasiopendwa ?

Makonda yupi ? huyuu au mwingine..
 
Vijana hawawez kushiriki au kuingia kwenye rushwa na mikataba mibovu. Hivyo naungana na Rais!
Wazee wa nch hii ndio walio tufikisha hapa tulipo

Joka la makengeza wakati akiwa mwanasheria mkubwa hakuwa kijana? Ukosefu wa maadili ni hulka na haina uhusiano na umri
 
Wewe kuna mizee ina miaka 42 haitaki hata kuachia vijana ni kujivutavuta tu ofisini wapishe na wao walipotufikisha imetosha

Kama sio ubanafsi wa vijana ni nini? Kuna mizee ya miaka 42? Duu kwahiyo vijana anaotaka Magu ni wenye umri gani? Dhambi ya ubaguzi mbaya sana
 
Rais yupo sahíhi kabisa' wazee wanafanya kazi kwa mazoea, nenda misungwi utajionea maafisa watendaji wengi wapya wakichapa kazi lkn wanapigwa majungu na maafisa watendaji wazee pamoja na kuwashawishi wananchi wakatae kuhudumiwa nao. Pia wamekubuhu kwa rushwaa.
 
Back
Top Bottom