Rais aonyesha mapenzi makubwa kwa wananchi wa Kahama. Awafundisha jinsi ya kukwepa kodi

Mimi bado sijaelewa,kuhusu hiyo barabara,ina maana ilikuwa bado haijazinduliwa tu,au walitoa ile lami wakajenga upya,
nakumbuka miaka 8 iliyopita nilikuwa huko na barabara ilikuwepo ya lami,au walifanya kuijenga upya tena?
Kwani alivyoenda kuzindua mwendokasi ilikuaje,si ulikua ushaanza fanya kazi karibia mwaka Ila kwa kupenda Kiki akaenda kuzindua tena.

Mambo mengine tuyaangaliege tu
 
Mbona alivyokuwa Tanga kama sijakosea ashawahi kusema hivyo hivyo wenye pick up safirisheni mazao na msisumbuliwe na akafuta tozo kwa tani moja ?

Chadema mna matatizo sana

Chadema Sio tatizo ndezi wewe, hii mbona ilipita bunge la mwaka jana huko Dodoma? Ila kinadharia haitekelezeki ilikuwa ni kuwatetea wakulima kinafiki.
 
Waziri wa ujenzi hivi yupo kweli? Maana kila uzinduzi unaohusu wizara yake huwa simuoni, majengo na barabara nasikia/naona mara nyingi zikizinduliwa na magufuli kulikoni wandugu...!
 
Leo Kahama kwenye uzinduzi wa barabara ya kiwango cha lami yenye urefu wa km 132 Isaka---Ushirombo.

Rais amesema mazao yenu mkisafirisha zaidi ya tani moja anatakiwa ulipe ushuru. Sasa ili kuwakomoa safirisheni tani moja moja mpaka mazao yako yanaisha hata kama tani miambili.
Hajawaokoa mkuu, kumbuka kodi ipo kwenye mafuta, unaponunua mafuta kila lita kodi shs 40, mwenye akili ndogo atasema wamekwepa kodi, la hasha wamekamuliwa haswaa
 
Leo Kahama kwenye uzinduzi wa barabara ya kiwango cha lami yenye urefu wa km 132 Isaka---Ushirombo.

Rais amesema mazao yenu mkisafirisha zaidi ya tani moja anatakiwa ulipe ushuru. Sasa ili kuwakomoa safirisheni tani moja moja mpaka mazao yako yanaisha hata kama tani miambili.
hahahahahahqhahaha.......
 
Wakulima nchi hii wameshanyanyasika vya kutosha, wacha awaokoe

Hiyo gharama ya kukodi usafiri tani moja moja na kurudia ni afadhali kulipa huo ushuru!!!
Kama kweli wakulima wanapaswa kusaidiwa basi aseme mkulima apatiwe kibali cha kusafirisha mazao yake bila ushuru. Hii inawezekana kwa kuorodhesha wakulima.
Wafanyabiashara wao watozwe ushuru
 
Leo Kahama kwenye uzinduzi wa barabara ya kiwango cha lami yenye urefu wa km 132 Isaka---Ushirombo.

Rais amesema mazao yenu mkisafirisha zaidi ya tani moja anatakiwa ulipe ushuru. Sasa ili kuwakomoa safirisheni tani moja moja mpaka mazao yako yanaisha hata kama tani miambili.
Unakodi gari la kubeba tani 7,wewe unabeba 1, afu gharama ya kubeba tani 1 sawa na tani 7,afu ukilipa ushuru na karushwa kidg kwa jamaa wa getini inakuwa poa kbs.
Siungi mkono rushwa ila najaribu kumsaidia mkulima tu kama serikali imeshindwa kumfutia kbs ushuru.
 
Bora umetumia akili kwa kweli maana sometimes ukisoma humu unabaki unashangaa tu watu wanaongea utadhani hata la saba hawajafika. Kipi ghali kusafirisha tani moja moja hadi zifike kumi au kulipa kodi unasafirisha mara moja? Hata economy of scale hatuijui? Watakaofaidika na agizo hili ni wale wakulima wadogo wadogo amba uwezo wao ni kuzalisha tani moja au pungufu ya tani moja and not the other way round. Na hatuwezi kuongelea maendeleo kwa mkulima anayezalisha tani moja. Hiyo ni susistance farming in fact we can not call them farmers but rather call them peasants
Manaa tunaongelea magunia 10, sasa magunia 10 si ya chakula cha kula nyumbani tu haya, hii sera mi niliiona ya ajabu sana manaake haikuwa na msaada wowote kwa mkulima...mimi huwa sielewi wasomi wetu serikalini wanafanya kazi gani kama wanakuja na jambo la kijinga kama hili nao ndo wanasema wamemsaidia mkulima..
 
Leo Kahama kwenye uzinduzi wa barabara ya kiwango cha lami yenye urefu wa km 132 Isaka---Ushirombo.

Rais amesema mazao yenu mkisafirisha zaidi ya tani moja anatakiwa ulipe ushuru. Sasa ili kuwakomoa safirisheni tani moja moja mpaka mazao yako yanaisha hata kama tani miambili.
It is called to be nice to your tribal members
 
Una tani 100 alafu usafirishe tani moja moja si wehu huo....

Huyu raisi ameona watanzania wote kama wanae..
 
Leo Kahama kwenye uzinduzi wa barabara ya kiwango cha lami yenye urefu wa km 132 Isaka - Ushirombo.

Rais amesema: “Mazao yenu mkisafirisha zaidi ya tani moja unatakiwa ulipe ushuru. Sasa ili kuwakomoa, safirisheni tani moja moja mpaka mazao yako yanaisha hata kama tani 200.”
Kusafirisha mazao mengi kidogo kidogo unakuwa unakwepa ushuru wa mazao unakutana na road licence kwenye mafuta.
 
Leo Kahama kwenye uzinduzi wa barabara ya kiwango cha lami yenye urefu wa km 132 Isaka - Ushirombo.

Rais amesema: “Mazao yenu mkisafirisha zaidi ya tani moja unatakiwa ulipe ushuru. Sasa ili kuwakomoa, safirisheni tani moja moja mpaka mazao yako yanaisha hata kama tani 200.”
Acha uongo hakuna mladi wa balabala kutoka Isaka kwenda Ushirombo
 
Back
Top Bottom