Rais aonana na Rais mpya wa Ghana, atembelea mashamba ya mananasi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais aonana na Rais mpya wa Ghana, atembelea mashamba ya mananasi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by armanisankara, Aug 16, 2012.

 1. a

  armanisankara JF-Expert Member

  #1
  Aug 16, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption"]Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Rais John Dramani Mahama wa Ghana nyumbani kwake jijini Accra leo Agosti 11, 2012 baada ya kumtembelea na kumpa pole ya msiba wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Marehemu John Evans Atta Mills aliyezikwa jana.


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption"]Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais John Dramani Mahama wa Ghana nyumbani kwake jijini Accra leo Agosti 11, 2012 wakati alipomtembelea kiongozi huyo mpya wa Ghana na kumpa pole ya msiba wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Marehemu John Evans Atta Mills[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption"]Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitazama manasi yakitayarishwa kwa ajili ya kusafirishwa na kuuzwa nje ya nchi katika kiwanda cha Bomarts Farms Ltd. katika kitongoji cha Dobro nje kidogo ya jiji la Accra leo Agosti 11, 2012


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption"]Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitazama ukulima wa kisasa wa manasi yanayolimwa kwa ajili ya kuuzwa nje ya nchi katika shmaba la Bomarts Farms Ltd. katika kijiji cha Dobrokatika eneo la Nsawam nje kidogo ya jiji la Accra leo Agosti 11, 2012. Kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa shamba hilo Bw. Anthony Botchway na mwenye suti ya buluu ni Waziri wa Chakula na Kilimo Mhe Kwesi Ahwol


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption"]Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia upandaji wa miche ya mananasi katika shamba la Koranco kijiji cha Obotweri nje kidogo ya jiji la Accra. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Koranco Farms Ltd. Bw Emmanuel B. Koranteng ambaye amekuwa akilima shamba la matunda kwa miaka 27. Mwalimu Nyerere aliwahi kumtembelea shambani hapo katikati ya miaka ya 1980 kujionea ukulima huo wa matunda.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #2
  Aug 16, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  Hiyo ni kazi ya taifa la Israel katika kuijenga africa ktk maswala ya kilimo. waisraeli wamefanikisha sana ghana ktk kilimo na kuwatafutia masoko ya mazao yao ndani ya Israel na marekani. serikali yetu bado haitaki hata kuweka ofisi pale tel aviv eti kwa sababu mpalestina ni ndugu yetu na hana nchi!Raisi wa ivory Cost mwezi uliopita litembelea israel kukuza export na import ya bidhaa kati ya Iraeli na nchi yake. tena yeye ni muislamu lakini kaweka mbele maslahi ya kiuchumi kuliko ya kisiasa. leo hii hapa petu ndio kwanza viongozi wetu wanakimbilia Iran na Uturuki ambako hakuna lolote la maana kutuletea maendeleo. kweli aliyetuloga kweli kafa.
   
Loading...