Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 24,463
- 34,485
Kimsingi nilikuwahi mapeema wakati umeanza kutekeleza majukumu yako ya Urais hasa baada ya Kuapa rasmi.
Nilikushauri uenende kwa hekima na uwe muangalifu sana kwa wasaidizi wako.
Kuna mambo ambayo kanuni za kibinaadam zinaweza kupata ufumbuzi ama kiini chake. lakini kuna mambo pia ambayo hata utumie telescope ya kuangalia angaza mbali huwezi kung'amua. mimi ni kiongozi in minority cascade lakini najifunza mengi mno kupitia haiba na tabia za ninaowaongoza.
Angalia hili jambo sasa.
Naamini utakuwa muangalifu sana na ndege aitwaye kasuku ambaye yeye ubunifu wake ni ulimi wake unaoweza kukariri pekee
Nimesema Ukweli.

- Wasichokuambia waliokuzunguka ni kwamba wananchi waliowengi wanaaminishwa kwamba wewe ndo chanzo cha madhila yote na ugumu wa maisha unaowakabili. Naamini umewahi kusikia huu wimbo usemao MAGUFULI KABANA. Yaani umefunga kila mwanya wa wananchi kupata maisha. watu wako hawasemi ukweli huku mitaani. hawasemi kuwa pesa za bure na za michongo zimedhibitiwa.
- Wasichokuambia ni kwamba kila kauli unayoitoa huwa inadakwa na kiwanda maalumu cha kuongezea hamira maneno yako na kuweka chembe za chuki ionekane haujali wala huoni madhila ya wananchi.
- wanachokuficha ni kwamba wananchi wanakupenda kwa sababu wamejawa hofu kuwa wanaweza na wao wakatumbuliwa.
- WALAMI wamejipanga kuokota mitaa na vijiji kwa wingi hapo 2019 ili wajipange 2020
- Watanzania waliotoroka nyumbani na kuzamia Msumbiji kisha wakarudishwa huku wengine wakiwa majina matupu walipaswa kupewa neno la faraja. maana hata yule mwana mpotevu aliyetapanya mali ya urithi alilakiwa na baba yake aliporejea nyumbani...
- Usipoona umuhimu wa viongozi wa ngazi ya chini kabisa (wenyeviti wa Mitaa) na ukawaacha wanyanyasike na kutengwa na watendaji wa serikali, basi kimya chao kitaweza kuleta jibu lisilotarajiwa 2019.
- MSEMA KWELI NI MPENZI WA MUNGU..... Je unaukubali ukweli kiasi gani mzee wangu? Hali ya uchumi kwenye kada ya chini si nzuri. Mfumuko wa bei hauzuiliki kwa huu mwendo wa EWURA kupandisha bei ya mafuta kila mwezi
Naamini utakuwa muangalifu sana na ndege aitwaye kasuku ambaye yeye ubunifu wake ni ulimi wake unaoweza kukariri pekee
Nimesema Ukweli.