Rais anayebeba watuhumiwa hafai | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais anayebeba watuhumiwa hafai

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by BAK, Oct 14, 2007.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 14, 2007
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,918
  Likes Received: 83,474
  Trophy Points: 280
  Sitaki Rais anayebeba wasiobebeka

  Ndimara Tegambwage
  Mwananchi

  SITAKI Rais Jakaya Kikwete apinde hoja. Sitaki rais awe moto na wakati huo huo awe baridi. Hii ni kwa kuwa sitaki wale rais anaotawala wamuone kuwa ni mwongo au mkosefu wa uadilifu.

  Hoja iliyoko mezani ni moja: Orodha ya watu wanaotuhumiwa kuhujumu uchumi wa nchi kwa kutenda, kutotenda au kunyamazia vitendo vya uhujumu.

  Kilio cha waliotoa orodha hiyo ni kwamba waliotajwa wachunguzwe na watakaobainika ionekane wazi kwamba wanachukuliwa hatua.

  Hicho ndicho kilio cha wananchi wengi; wale wanaoshuhudia fedha na utajiri mkubwa wa nchi vikifujwa na wachache na kwa njia ya ufisadi, huku viongozi wao wakiongeza tabasamu.

  Hayo ndiyo matakwa ya mabalozi wa nchi za nje, waliotoa maoni yao binafsi kuhusu madai ya ufisadi na kuhitimisha kuwa nao wangependa kuona serikali ikijibu tuhuma kwa njia mbili:

  Kwanza, ikijibu tuhuma zinazowakabili viongozi wake mmojammoja na serikali kwa ujumla; na pili, ikichunguza na kuchukua hatua.

  Hayo ndiyo matakwa ya Shirika la Fedha Duniani (IMF), kwamba pamoja na dalili za kile kinachoitwa kukua kwa uchumi, kuna haja ya kujibu tuhuma za ufisadi na kuchukua hatua za kuzuia mmomonyoko.

  Katika kauli zake wiki iliyopita mjini Arusha, badala ya kujibu hoja iliyoko mezani, Rais Kikwete alijipa kazi ya kuandama aliowaita “watu wengine.”

  Alitumia muda mwingi kukandia wale aliosema wanafanya kazi ya kutuhumu, kukamata, kushitaki na kuhukumu watuhumiwa. Alisema taifa litawekwa pabaya iwapo litadumu kwenye kutuhumiana.

  Kauli ya Rais Kikwete inaweza kutafsiriwa kama ifuatavyo: Kwamba hajaketi na kuelezwa yaliyotokea akiwa nje ya nchi. Hajasoma hata taarifa za magazeti na wataalam wake wa mawasiliano hawajapata muda wa kumpa taarifa.

  Kwamba rais hajaambiwa kuwa hata yeye ni miongoni mwa waliotuhumiwa; na kwa msingi huo alistahili kujibu sehemu inayomhusu.

  Kwamba rais hajakaa na watuhumiwa wengine kutafuta jinsi ya kujibu kwa pamoja au kutafuta msimamo wa pamoja, wa kina na unaoweza kutosheleza matakwa ya taarifa kamili ya serikali inayojali na adilifu.

  Kwa ufupi, rais hajajibu hoja kuu ambayo ni tuhuma za ufisadi. Kwa maana hiyo rais amepuuza tuhuma za ufisadi dhidi yake na mawaziri wake.

  Kinachoeleweka kutokana na kauli zake, ni kwamba ameamua kuzika hoja muhimu, na kwenye nafasi yake, kuingiza shutuma kwa vyama vya upinzani na viongozi wao ambao ni chanzo cha tuhuma za ufisadi.

  Lakini ni Kikwete yule yule aliyenukuliwa akiiambia Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama chake kuwa waziri yeyote atakayesaini mkataba wa madini nje ya makubaliano yaliyofikiwa kati ya serikali na kampuni za madini nchini, atakuwa amejifukuzisha kazi mwenyewe.

  Huko ndiko kuwa moto na baridi kwa wakati mmoja. Rais hajibu tuhuma dhidi yake. Rais hajibu tuhuma za wateule wake. Rais anakandia wapinzani kwa kuwa polisi na hakimu.

  Rais anasema waziri wake atakuwa amejifukuzisha kazi. Rais anasema atachunguza na yule ambaye tuhuma dhidi yake zitathibitika, atachukuliwa hatua.

  Rais anataka wananchi na “wapinzani” wapeleke ushahidi, kwake au polisi, wa tuhuma zao dhidi ya yeyote ili serikali itumie ushahidi huo kuchunguza!

  Hizi zote ni njia za kukimbia hoja kuu. Rais anapofikia hatua ya “kumbakumba;” kukusanya sababu dhaifu hapa na pale ili kulinda wateule wake na serikali yake, ujue kuna mkwamo.

  Wote waliokuwa wakifuatilia sakata la tuhuma za ufisadi tangu Dk. Willbrod Slaa asome orodha ya watuhumiwa hadharani, mwezi mmoja uliopita, walitarajia Rais Kikwete kuja na kauli tofauti na hii aliyotoa.

  Walisubiri aseme uhujumu wa uchumi ni kitu kibaya sana. Kwamba wananchi wamefanya vizuri kutoa hadharani majina ya wale wanaotuhumiwa. Kwamba tume huru ya wajumbe kutoka asasi za kijamii na watu wanaoaminika kuwa na rekodi safi katika jamii, inaundwa na kuanza mara moja kufanya uchunguzi.

  Nchi nzima walitarajia rais aseme anajua kuwa uchunguzi huanzia kwenye shaka. Shaka hutokana na tabia, mwenendo na hata mwonekano wa hali halisi wa mambo yanayopingana na kauli, ahadi, kanuni, taratibu na sheria zinazotawala.

  Kwa msingi huo, akitokea mtu au kundi la watu, wakawa na shaka; wakachimba na kuonyesha kiini cha shaka; hiyo inatosha kupiga kelele ili vyombo vilivyosomea kazi ya upelelezi viweze kufanya kazi.

  Wananchi na jumuia ya kimataifa walitarajia rais awe anajua hilo; na hasa awe anajua kwamba ushahidi hautoki kwa “wapiga filimbi,” bali hutokana na uchunguzi ambao ndio wote wanataka ufanyike.

  Kudai ushahidi kutoka kwa wananchi maana yake ni kukataa kuchunguza tuhuma za ufisadi; ni kuweka jembe la kukokotwa mbele ya maksai badala ya kuliweka nyuma ili alikokote na kulima.

  Na hii si kwa bahati mbaya. Ni makusudi. Ofisa mmoja alipotaka kuwanyima kazi vijana wanne waliokuwa na kasi ya kuchapa maneno 120 kwa dakika kwenye taipureta, alitoa zoezi lisilowezekana.

  Alisema: “Kwa kuwa nyote ni wataalam, sasa sharti tupate mshindi. Tutaweka taipureta nyuma yako; nawe utapinda mikono yako na kupiga taipureta huko nyuma ili kuonyesha umahiri wako. Nafasi iko wazi.”

  Waliona haiwezekani. Hawakujaribu. Walijua jambo moja, kwamba hizo zilikuwa njama za ofisa kuendelea kuajiri ndugu yake asiyekuwa mjuzi. Kumlinda. Ndivyo rais anavyotaka kufanya. Hapana. Ndivyo alivyofanya.

  Sitaki rais awe na fikra kwamba alionao katika baraza lake la mawaziri ndiyo pekee wenye akili na uwezo wa kutenda. Wako wengi nje ya baraza. Vilevile si Kikwete pekee awezaye kuwa rais katika nchi hii. Wamekuwapo. Wametoka na wengine wengi wapo.

  Kwa nini Rais Kikwete anashindwa kuelewa kuwa kwa nafasi aliyoko, anaweza kutenda maajabu na kuwa shujaa mwingine wa nchi hii kwa kuwatosa wasiobebeka na kusonga mbele?

  Sitaki rais asiyeona kuwa hata yeye anaweza kujikuta mmoja wa wasiobebeka na akatoswa na wale ambao angekuwa amewatosa mapema. Itakuwa habari kuu kwa gazeti letu.

  Mwandishi wa makala hii anapatikana kwa simu; 0713 614 872; baruapepe: ndimara@yahoo.com na www.ndimara.blogspot.com
   
 2. T

  Tasia I JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2010
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 1,226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Na Balibati Kangungu - Imechapwa 29 September 2010

  BABA wa Taifa, Mwalimu Nyerere aliwahi kusema: “Kwa kawaida watu makini wanaogopwa na wala rushwa; serikali ‘corrupt’ – ya wala rushwa – hutumwa na wenye fedha.”

  Alikuwa na maana kwamba, kawaida wahalifu huogopa sana mamlaka pamoja na vyombo vya kusimamia sheria na haki.

  Wakati huohuo, mamlaka na wote wanaosimamia haki, hutaka na hasa hupaswa, kukaa mbali na watuhumiwa wa uhalifu wowote; kwa maana ya kutokuwa maswahiba.

  Lakini sivyo ilivyo kwa mgombea urais wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, Amiri Jeshi Mkuu.
  Katika kampeni za kugombea urais zinazoendelea nchini kote, Kikwete
  ameonekana kwenye majukwaa ya siasa, akikumbatia na kukumbatiwa na watuhumiwa wa makosa makubwa ya jinai nchini.

  Hivi tatizo ni la mgombea au watuhumiwa wenyewe?
  Polisi mwadilifu, kama raia mwema na kiongozi safi, hapendi kuzoeana na wahalifu; na ndiyo sababu ifanyayo watuhumiwa wa uhalifu kudundwa na moyo kila waonapo walinzi wa sheria na haki.
  Sasa inakuwaje rais azoeleke kwa watuhumiwa kwa kiwango cha kuwakumbatia jukwaani na kuwaliwaza kwa lugha nyororo?

  Rais anapeleka ujumbe gani kwa wananchi ambao walikuwa wakidhani kuwa kweli kuna vita vya kupambana na wahalifu?

  Hivi karibuni jijini Mwanza, nilikutana na Alfred Tibaigana, aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

  Niliongea naye na kumpa pole kwa uchovu kutokana na kinyanganyiro cha kura za maoni katika jimbo la Muleba Kusini ambako aligombea kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

  Katika mazungumzo yale, na katika hali ya utani, akanieleza kuwa mpinzani wake mmoja alikuwa anawashawishi wapigakura wasimchague kwa kuwa yeye ni “polisi na hivyo akichaguliwa, “hamtakaa tena mnywe gongo.”

  Alisema haamini kuwa kushindwa katika kura za maoni kulitokana na yeye kuwa polisi, lakini hata hivyo anasema, “watu wengi vijijini bado wanaogopa polisi.”

  Si kawaida kuona watu wakimzoea polisi hata kama hawana makosa ya jinai. Polisi huitwa kwa majina mengi mabaya na hasa kama wanatimiza wajibu wao sawasawa.

  Mahali popote polisi walipo, wahalifu hawana raha. Mahali pengine mijini na vijijini, watu hawapendi kuishi mtaa mmoja na polisi kwa hofu tu kwamba, polisi hawana urafiki wa kudumu. Kimsingi hakuna polisi mwungwana linapokuja suala la uhalifu.

  Kama polisi anaweza kuogopwa kiasi hicho, mbona rais, amiri jeshi mkuu na kiongozi wa chama kizee na kikubwa haogopwi na watuhumiwa?

  Ingawa ni kweli kwamba vikao vya uteuzi vya chama vilipitisha baadhi ya watuhumiwa kuwa wagombea ubunge na udiwani, haina maana kuwa mgombea wa CCM, ambaye ni rais aliyeko marakani, awe na mazoea na watuhumiwa.

  Akiwa mkoani Iringa, Kikwete alimpandisha jukwaani Fredrick Mwakalebela, mwanachama wa CCM anayekabiliwa na kesi ya rushwa mahakamani kutokana na mchakato wa uchaguzi ndani ya chama cha mgombea urais.

  Vyombo vya habari vimeanika habari hiyo. Vikatoa hata picha ya wawili hao wakiwa wameshikana mikono.

  Hili ni pigo kubwa kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU); lakini limesababishwa na Kikwete ambaye kimsingi ndiye kamanda mkuu wa TAKUKURU.

  Tangu siku hiyo, inabidi taasisi hii ya kupambana na rushwa ijiulize mara mbili inaposhughulika na Mwakalebela.

  Wakati naandika makala hii, afisa mmoja wa TAKUKURU ameniambia, “Rais anatukatisha tamaa” na ndiyo maana hata baadhi ya maafisa wa TAKUKURU nao wameanza kushawishika kupokea rushwa kwani wanaona hawana kamanda aliyedhamiria kukomesha rushwa nchini.

  Hata ndani ya jeshi la polisi, askari wa vyeo vya chini wanalazimika “kumalizana na wahalifu” kwa sababu wakikomaa nao hadi vituoni, kuna hatari ya kuwaona wahalifu wakikumbatiana na makamanda wao na kutakiana heri na afya njema.

  Akiwa mkoani Kilimanjaro, Kikwete alimnadi Basil Mramba, mtuhumiwa anayekabiliwa na kesi mbaya ya matumizi mabaya ya madaraka na kesi hiyo inaendeshwa na TAKUKURU na mwendesha mashtaka wa serikali.

  Kikwete amenukuliwa akasema “anamwamini” Mramba na kuwa ni “mzee kijana” mwenye uwezo mkubwa na maono.

  Alipoingia mkoani Arusha akapanda jukwaani na Edward Lowassa, waziri mkuu aliyejiuzuru na kumnadi kuwa ni mtu safi na “anamwamini” na kuwaomba wananchi wampigie kura kwa sababu “yaliyopita si ndwele.”

  Lowassa alijiuzuru kutokana na kashfa ya Richmond iliyojaa matumizi mabaya ya madaraka na harufu ya rushwa.

  Bunge la Jamhuri lililomthibitisha alipoteuliwa kuwa waziri mkuu, ndilo lilimchunguza na kumwacha ajiuzulu kwa kashfa hiyo.

  Mpaka leo, wananchi wengi wanaamini kuna mengi yanafichwa kuhusu kashfa ya Richmond. Kumnadi Lowassa jukwaani, kama alivyonadi watuhumiwa wengine, kumethibitisha, kwa namna ya pekee, kuwepo kwa uswahiba kati ya Kikwete na ufisadi.

  Alipoingia madarakani na kuanzisha operesheni maalum ya kutokomeza ujambazi nchini, Kikwete alichekwa na majambazi wakubwa kwa kuambiwa “unataka kukata tawi ulilolikalia.”
  Haukupita muda mrefu, polisi wakiwa katika upekuzi ndani ya nyumba ya mtuhumiwa wa ujambazi, walikuta picha kubwa ya Rais Kikwete akiwa na mtuhumiwa huyo.

  Picha hiyo ilipigwa siku mtuhumiwa alipokabidhi hundi ya Sh. 40 milioni zilizotumika katika kampeni ya Kikwete mwaka 2005.

  Kilichofuata baada ya hapo ni mtuhumiwa kupewa onyo, kwamba awe mwangalifu na asijihusishe tena na ujambazi.

  Haijulikani mamilioni hayo ya shilingi yalitokana na “shughuli” ipi – damu za raia walionyang’anywa magari yao na kuuawa, wakiwemo polisi waliokuwa wanalinda raia hao?
  Kikwete ndiye anayejua. Lakini la muhimu ni kwamba urafiki kati ya jemedari Kikwete na watuhumiwa umewaponza wengi.

  Inapotokea kamanda anacheka na kukumbatiana na watuhumiwa, askari walio msitari wa mbele wanavunjika moyo na hata maisha yao kuwa hatarini.

  Taifa liko vitani dhidi ya rushwa, ubadhilifu wa mali ya umma na hata matumizi mabaya ya madaraka. Katika vita hivi, ni vema itikadi za vyama zikawekwa pembeni na kuweka utaifa mbele.
  Maafisa wa TAKUKURU wanapomtuhumu mtu au kumfikisha mtuhumiwa yeyote mahakamani, wanafanya hivyo kwa niaba ya rais.

  Sasa inakuwaje rais huyohuyo acheke na kukumbatiana na watuhumiwa jukwaani? Inakuwaje awainue mikono, aseme anawaamini na kuwaombea kura kwa wananchi?

  Mapema mwanzoni mwa utawala wake, Kikwete aliwateua kuwa mawaziri watu wa namna ya Andrew Chenge na Mramba hata kama kulikuwa na kelele na manung’uniko mengi kuhusu uadilifu wao.
  Ilioekana hilo lilitosha, lakini yaelekea sikio la kufa halisikii dawa. Baada ya hapo Kikwete aliendelea kuwateua, katika nafasi mbalimbali, maafisa waliohusika katika kashfa za ukwapuaji wa mabilioni ya shilingi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).

  Ifike mahali swali hili lijibiwe: Kwa nini mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete hachukii uhalifu na watuhumiwa wa uhalifu? Nani anayetamani rais wa namna hii?

  Gazeti toleo na. 208 mwanahalisi.
   
 3. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Hayo ndo maajabu ya karne hiiiii!!!!!!
   
 4. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  KATIKA UCHAGUZI MKUU WA WA MWAKA 1995 MWALIMU NYERERE NDIYE ALIYEKUWA MPIGA DEBE MKUU WA CCM DHIDI YA NGUVU KUBWA YA MHE AUGUSTINE LYATONGA MREMA WA NCCR MAGEUZI. LAKINI KWA SABABU ALIFAHAMU KUWA MGOMBEA UBUNGE ALIYESIMAMISHWA NA CCM DR EMMANUL MAGOTTI KATIKA JIMBO LA MUSOMA ALIKUWA NA TUHUMA ZA KUFILISI USHIRIKA WAKATI WA KWANADI WAGOMBEA WA CCM ALIMNADI MHE b mKAPA NA KWA NAFASI YA UBUNGE AKATANGAZA HADAHARANI KUWA KURA YAKE ITAKWENDA KWA MGOMBEA WA NCCR MAGEUZI BALOZI PAUL NDOBO NA UWANJA WOTE KULIPUKA KWA SHANGWE NA HOI HOI. nA HUYO NDIO ALIKUWA MWASISI WA CCM; SASA HAWA MAMABO YA KUKUMBATIANA NA MAFISADI WAMEYAPATA WAPI?.

  KAMA MWASISI WA CCM ALIWEZA KUKIPIGIA KURA CHAMA CHA UPINZANI, NI KWANINI WATANZANIA WENGINE WASHINDWE KUJIFUNZA KUTOKA KWAKE. NI VYEMA WANACCM WAKAVIPIGIA KURA VYAMA VYA UPINZANIA KAMA NJIA MOPJAWAPO YA KUTOA MAFUNZO KWA MAFISADI WOTE NDANI YA CCM, KWANI TANZANIA BILA CCM INAWEZEKANA KAMA ILIVYO KENYA BILA KANU YA KENYATTA NA MOI; ZAMBIA BILA UNIP YA KAUNDA N.K.

  LAKINI CCM BILA TANZANIA NA RASLIMALI ZAKE HAIWEZEKANI ASILANI. HERI VYAMA VIDOGO VIDOGO AMBAVYO VIMEZOEA KUWEPO BILA YA KUHUSISHA RASLI MALI ZA TANZANIA
   
 5. U

  Ujengelele JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2010
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 1,256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Rais anayebeba watuhumiwa hafai

  [​IMG]
  Na Balibati Kangungu - Imechapwa 29 September 2010

  [​IMG][​IMG] [​IMG]

  BABA wa Taifa, Mwalimu Nyerere aliwahi kusema: “Kwa kawaida watu makini wanaogopwa na wala rushwa; serikali ‘corrupt’ – ya wala rushwa – hutumwa na wenye fedha.”
  Alikuwa na maana kwamba, kawaida wahalifu huogopa sana mamlaka pamoja na vyombo vya kusimamia sheria na haki.
  Wakati huohuo, mamlaka na wote wanaosimamia haki, hutaka na hasa hupaswa, kukaa mbali na watuhumiwa wa uhalifu wowote; kwa maana ya kutokuwa maswahiba.
  Lakini sivyo ilivyo kwa mgombea urais wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, Amiri Jeshi Mkuu.
  Katika kampeni za kugombea urais zinazoendelea nchini kote, Kikwete
  ameonekana kwenye majukwaa ya siasa, akikumbatia na kukumbatiwa na watuhumiwa wa makosa makubwa ya jinai nchini.
  Hivi tatizo ni la mgombea au watuhumiwa wenyewe?
  Polisi mwadilifu, kama raia mwema na kiongozi safi, hapendi kuzoeana na wahalifu; na ndiyo sababu ifanyayo watuhumiwa wa uhalifu kudundwa na moyo kila waonapo walinzi wa sheria na haki.
  Sasa inakuwaje rais azoeleke kwa watuhumiwa kwa kiwango cha kuwakumbatia jukwaani na kuwaliwaza kwa lugha nyororo?
  Rais anapeleka ujumbe gani kwa wananchi ambao walikuwa wakidhani kuwa kweli kuna vita vya kupambana na wahalifu?
  Hivi karibuni jijini Mwanza, nilikutana na Alfred Tibaigana, aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam.
  Niliongea naye na kumpa pole kwa uchovu kutokana na kinyanganyiro cha kura za maoni katika jimbo la Muleba Kusini ambako aligombea kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
  Katika mazungumzo yale, na katika hali ya utani, akanieleza kuwa mpinzani wake mmoja alikuwa anawashawishi wapigakura wasimchague kwa kuwa yeye ni “polisi na hivyo akichaguliwa, “hamtakaa tena mnywe gongo.”
  Alisema haamini kuwa kushindwa katika kura za maoni kulitokana na yeye kuwa polisi, lakini hata hivyo anasema, “watu wengi vijijini bado wanaogopa polisi.”
  Si kawaida kuona watu wakimzoea polisi hata kama hawana makosa ya jinai. Polisi huitwa kwa majina mengi mabaya na hasa kama wanatimiza wajibu wao sawasawa.
  Mahali popote polisi walipo, wahalifu hawana raha. Mahali pengine mijini na vijijini, watu hawapendi kuishi mtaa mmoja na polisi kwa hofu tu kwamba, polisi hawana urafiki wa kudumu. Kimsingi hakuna polisi mwungwana linapokuja suala la uhalifu.
  Kama polisi anaweza kuogopwa kiasi hicho, mbona rais, amiri jeshi mkuu na kiongozi wa chama kizee na kikubwa haogopwi na watuhumiwa?
  Ingawa ni kweli kwamba vikao vya uteuzi vya chama vilipitisha baadhi ya watuhumiwa kuwa wagombea ubunge na udiwani, haina maana kuwa mgombea wa CCM, ambaye ni rais aliyeko marakani, awe na mazoea na watuhumiwa.
  Akiwa mkoani Iringa, Kikwete alimpandisha jukwaani Fredrick Mwakalebela, mwanachama wa CCM anayekabiliwa na kesi ya rushwa mahakamani kutokana na mchakato wa uchaguzi ndani ya chama cha mgombea urais.
  Vyombo vya habari vimeanika habari hiyo. Vikatoa hata picha ya wawili hao wakiwa wameshikana mikono.
  Hili ni pigo kubwa kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU); lakini limesababishwa na Kikwete ambaye kimsingi ndiye kamanda mkuu wa TAKUKURU.
  Tangu siku hiyo, inabidi taasisi hii ya kupambana na rushwa ijiulize mara mbili inaposhughulika na Mwakalebela.
  Wakati naandika makala hii, afisa mmoja wa TAKUKURU ameniambia, “Rais anatukatisha tamaa” na ndiyo maana hata baadhi ya maafisa wa TAKUKURU nao wameanza kushawishika kupokea rushwa kwani wanaona hawana kamanda aliyedhamiria kukomesha rushwa nchini.
  Hata ndani ya jeshi la polisi, askari wa vyeo vya chini wanalazimika “kumalizana na wahalifu” kwa sababu wakikomaa nao hadi vituoni, kuna hatari ya kuwaona wahalifu wakikumbatiana na makamanda wao na kutakiana heri na afya njema.
  Akiwa mkoani Kilimanjaro, Kikwete alimnadi Basil Mramba, mtuhumiwa anayekabiliwa na kesi mbaya ya matumizi mabaya ya madaraka na kesi hiyo inaendeshwa na TAKUKURU na mwendesha mashtaka wa serikali.
  Kikwete amenukuliwa akasema “anamwamini” Mramba na kuwa ni “mzee kijana” mwenye uwezo mkubwa na maono.
  Alipoingia mkoani Arusha akapanda jukwaani na Edward Lowassa, waziri mkuu aliyejiuzuru na kumnadi kuwa ni mtu safi na “anamwamini” na kuwaomba wananchi wampigie kura kwa sababu “yaliyopita si ndwele.”
  Lowassa alijiuzuru kutokana na kashfa ya Richmond iliyojaa matumizi mabaya ya madaraka na harufu ya rushwa.
  Bunge la Jamhuri lililomthibitisha alipoteuliwa kuwa waziri mkuu, ndilo lilimchunguza na kumwacha ajiuzulu kwa kashfa hiyo.
  Mpaka leo, wananchi wengi wanaamini kuna mengi yanafichwa kuhusu kashfa ya Richmond. Kumnadi Lowassa jukwaani, kama alivyonadi watuhumiwa wengine, kumethibitisha, kwa namna ya pekee, kuwepo kwa uswahiba kati ya Kikwete na ufisadi.
  Alipoingia madarakani na kuanzisha operesheni maalum ya kutokomeza ujambazi nchini, Kikwete alichekwa na majambazi wakubwa kwa kuambiwa “unataka kukata tawi ulilolikalia.”
  Haukupita muda mrefu, polisi wakiwa katika upekuzi ndani ya nyumba ya mtuhumiwa wa ujambazi, walikuta picha kubwa ya Rais Kikwete akiwa na mtuhumiwa huyo.
  Picha hiyo ilipigwa siku mtuhumiwa alipokabidhi hundi ya Sh. 40 milioni zilizotumika katika kampeni ya Kikwete mwaka 2005.
  Kilichofuata baada ya hapo ni mtuhumiwa kupewa onyo, kwamba awe mwangalifu na asijihusishe tena na ujambazi.
  Haijulikani mamilioni hayo ya shilingi yalitokana na “shughuli” ipi – damu za raia walionyang’anywa magari yao na kuuawa, wakiwemo polisi waliokuwa wanalinda raia hao?
  Kikwete ndiye anayejua. Lakini la muhimu ni kwamba urafiki kati ya jemedari Kikwete na watuhumiwa umewaponza wengi.
  Inapotokea kamanda anacheka na kukumbatiana na watuhumiwa, askari walio msitari wa mbele wanavunjika moyo na hata maisha yao kuwa hatarini.
  Taifa liko vitani dhidi ya rushwa, ubadhilifu wa mali ya umma na hata matumizi mabaya ya madaraka. Katika vita hivi, ni vema itikadi za vyama zikawekwa pembeni na kuweka utaifa mbele.
  Maafisa wa TAKUKURU wanapomtuhumu mtu au kumfikisha mtuhumiwa yeyote mahakamani, wanafanya hivyo kwa niaba ya rais.
  Sasa inakuwaje rais huyohuyo acheke na kukumbatiana na watuhumiwa jukwaani? Inakuwaje awainue mikono, aseme anawaamini na kuwaombea kura kwa wananchi?
  Mapema mwanzoni mwa utawala wake, Kikwete aliwateua kuwa mawaziri watu wa namna ya Andrew Chenge na Mramba hata kama kulikuwa na kelele na manung’uniko mengi kuhusu uadilifu wao.
  Ilioekana hilo lilitosha, lakini yaelekea sikio la kufa halisikii dawa. Baada ya hapo Kikwete aliendelea kuwateua, katika nafasi mbalimbali, maafisa waliohusika katika kashfa za ukwapuaji wa mabilioni ya shilingi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).
  Ifike mahali swali hili lijibiwe: Kwa nini mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete hachukii uhalifu na watuhumiwa wa uhalifu? Nani anayetamani rais wa namna hii?
   
 6. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #6
  Oct 6, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Mwogopeni sana Kikwete. Wazungu wanasema, 'Birds of the same feathers, flock together'!
   
 7. U

  Ujengelele JF-Expert Member

  #7
  Oct 6, 2010
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 1,256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  They always flock together
   
 8. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #8
  Oct 6, 2010
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  INDEED THEY DO...!

  VOTE FOR THE ONE-IN-A-GENERATION MAN....Dr SLAA, THANK U GOD FOR GIVING US ANOTHER NYERERE..!
   
 9. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #9
  Oct 6, 2010
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  BABA wa Taifa, Mwalimu Nyerere aliwahi kusema: "Kwa kawaida watu makini wanaogopwa na wala rushwa; serikali ‘corrupt' – ya wala rushwa – hutumwa na wenye fedha."

  WELL SAID..... HUITAJI KUHITIMU DARASA LA SABA ILI KUELEWA KUWA SERIKALI YA KIKWETE INATUMWA NA AKINA FISADI.
   
 10. C

  Chokona Member

  #10
  Oct 6, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 56
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wengine husema hivi "Show me your friend and I will tell you, who you are"
   
 11. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #11
  Oct 6, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,381
  Likes Received: 3,141
  Trophy Points: 280
  Tupige kura ya maoni kwanza kabla ya uchaguzi ili ccm waamini kuwa hatuwataki?..........rais na akili zake anawasamehe wezi na kuwanadi?....inaniumiza sana moyoni sijui wa kunipooza.........
   
 12. Mundali

  Mundali JF-Expert Member

  #12
  Oct 6, 2010
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Rais mkumbatia uhalifu naye pia anahusika. Tukumbushane ya akina Noriega. JK hana tofauti kubwa na Noriega, alipewa orodha ya wauza unga hajawafanya lolote. HAFAIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII
   
 13. Mazingira

  Mazingira JF-Expert Member

  #13
  Oct 7, 2010
  Joined: May 31, 2009
  Messages: 1,837
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  BABA wa Taifa, Mwalimu Nyerere aliwahi kusema: "Kwa kawaida watu makini wanaogopwa na wala rushwa; serikali ‘corrupt' – ya wala rushwa – hutumwa na wenye fedha."
  Alikuwa na maana kwamba, kawaida wahalifu huogopa sana mamlaka pamoja na vyombo vya kusimamia sheria na haki.

  Wakati huohuo, mamlaka na wote wanaosimamia haki, hutaka na hasa hupaswa, kukaa mbali na watuhumiwa wa uhalifu wowote; kwa maana ya kutokuwa maswahiba.

  Lakini sivyo ilivyo kwa mgombea urais wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, Amiri Jeshi Mkuu.
  Katika kampeni za kugombea urais zinazoendelea nchini kote, Kikwete
  ameonekana kwenye majukwaa ya siasa, akikumbatia na kukumbatiwa na watuhumiwa wa makosa makubwa ya jinai nchini.

  Hivi tatizo ni la mgombea au watuhumiwa wenyewe?
  Polisi mwadilifu, kama raia mwema na kiongozi safi, hapendi kuzoeana na wahalifu; na ndiyo sababu ifanyayo watuhumiwa wa uhalifu kudundwa na moyo kila waonapo walinzi wa sheria na haki.

  Sasa inakuwaje rais azoeleke kwa watuhumiwa kwa kiwango cha kuwakumbatia jukwaani na kuwaliwaza kwa lugha nyororo?
  Rais anapeleka ujumbe gani kwa wananchi ambao walikuwa wakidhani kuwa kweli kuna vita vya kupambana na wahalifu?

  Hivi karibuni jijini Mwanza, nilikutana na Alfred Tibaigana, aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam.
  Niliongea naye na kumpa pole kwa uchovu kutokana na kinyanganyiro cha kura za maoni katika jimbo la Muleba Kusini ambako aligombea kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
  Katika mazungumzo yale, na katika hali ya utani, akanieleza kuwa mpinzani wake mmoja alikuwa anawashawishi wapigakura wasimchague kwa kuwa yeye ni "polisi na hivyo akichaguliwa, "hamtakaa tena mnywe gongo."

  Alisema haamini kuwa kushindwa katika kura za maoni kulitokana na yeye kuwa polisi, lakini hata hivyo anasema, "watu wengi vijijini bado wanaogopa polisi."
  Si kawaida kuona watu wakimzoea polisi hata kama hawana makosa ya jinai. Polisi huitwa kwa majina mengi mabaya na hasa kama wanatimiza wajibu wao sawasawa.
  Mahali popote polisi walipo, wahalifu hawana raha. Mahali pengine mijini na vijijini, watu hawapendi kuishi mtaa mmoja na polisi kwa hofu tu kwamba, polisi hawana urafiki wa kudumu. Kimsingi hakuna polisi mwungwana linapokuja suala la uhalifu.
  Kama polisi anaweza kuogopwa kiasi hicho, mbona rais, amiri jeshi mkuu na kiongozi wa chama kizee na kikubwa haogopwi na watuhumiwa?

  Ingawa ni kweli kwamba vikao vya uteuzi vya chama vilipitisha baadhi ya watuhumiwa kuwa wagombea ubunge na udiwani, haina maana kuwa mgombea wa CCM, ambaye ni rais aliyeko marakani, awe na mazoea na watuhumiwa.

  Akiwa mkoani Iringa, Kikwete alimpandisha jukwaani Fredrick Mwakalebela, mwanachama wa CCM anayekabiliwa na kesi ya rushwa mahakamani kutokana na mchakato wa uchaguzi ndani ya chama cha mgombea urais.

  Vyombo vya habari vimeanika habari hiyo. Vikatoa hata picha ya wawili hao wakiwa wameshikana mikono.
  Hili ni pigo kubwa kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU); lakini limesababishwa na Kikwete ambaye kimsingi ndiye kamanda mkuu wa TAKUKURU.
  Tangu siku hiyo, inabidi taasisi hii ya kupambana na rushwa ijiulize mara mbili inaposhughulika na Mwakalebela.

  Wakati naandika makala hii, afisa mmoja wa TAKUKURU ameniambia, "Rais anatukatisha tamaa" na ndiyo maana hata baadhi ya maafisa wa TAKUKURU nao wameanza kushawishika kupokea rushwa kwani wanaona hawana kamanda aliyedhamiria kukomesha rushwa nchini.

  Hata ndani ya jeshi la polisi, askari wa vyeo vya chini wanalazimika "kumalizana na wahalifu" kwa sababu wakikomaa nao hadi vituoni, kuna hatari ya kuwaona wahalifu wakikumbatiana na makamanda wao na kutakiana heri na afya njema.

  Akiwa mkoani Kilimanjaro, Kikwete alimnadi Basil Mramba, mtuhumiwa anayekabiliwa na kesi mbaya ya matumizi mabaya ya madaraka na kesi hiyo inaendeshwa na TAKUKURU na mwendesha mashtaka wa serikali.

  Kikwete amenukuliwa akasema "anamwamini" Mramba na kuwa ni "mzee kijana" mwenye uwezo mkubwa na maono.

  Alipoingia mkoani Arusha akapanda jukwaani na Edward Lowassa, waziri mkuu aliyejiuzuru na kumnadi kuwa ni mtu safi na "anamwamini" na kuwaomba wananchi wampigie kura kwa sababu "yaliyopita si ndwele."

  Lowassa alijiuzuru kutokana na kashfa ya Richmond iliyojaa matumizi mabaya ya madaraka na harufu ya rushwa.
  Bunge la Jamhuri lililomthibitisha alipoteuliwa kuwa waziri mkuu, ndilo lilimchunguza na kumwacha ajiuzulu kwa kashfa hiyo.

  Mpaka leo, wananchi wengi wanaamini kuna mengi yanafichwa kuhusu kashfa ya Richmond. Kumnadi Lowassa jukwaani, kama alivyonadi watuhumiwa wengine, kumethibitisha, kwa namna ya pekee, kuwepo kwa uswahiba kati ya Kikwete na ufisadi.

  Alipoingia madarakani na kuanzisha operesheni maalum ya kutokomeza ujambazi nchini, Kikwete alichekwa na majambazi wakubwa kwa kuambiwa "unataka kukata tawi ulilolikalia."

  Haukupita muda mrefu, polisi wakiwa katika upekuzi ndani ya nyumba ya mtuhumiwa wa ujambazi, walikuta picha kubwa ya Rais Kikwete akiwa na mtuhumiwa huyo.
  Picha hiyo ilipigwa siku mtuhumiwa alipokabidhi hundi ya Sh. 40 milioni zilizotumika katika kampeni ya Kikwete mwaka 2005.

  Kilichofuata baada ya hapo ni mtuhumiwa kupewa onyo, kwamba awe mwangalifu na asijihusishe tena na ujambazi.
  Haijulikani mamilioni hayo ya shilingi yalitokana na "shughuli" ipi – damu za raia walionyang'anywa magari yao na kuuawa, wakiwemo polisi waliokuwa wanalinda raia hao?

  Kikwete ndiye anayejua. Lakini la muhimu ni kwamba urafiki kati ya jemedari Kikwete na watuhumiwa umewaponza wengi.
  Inapotokea kamanda anacheka na kukumbatiana na watuhumiwa, askari walio msitari wa mbele wanavunjika moyo na hata maisha yao kuwa hatarini.
  Taifa liko vitani dhidi ya rushwa, ubadhilifu wa mali ya umma na hata matumizi mabaya ya madaraka. Katika vita hivi, ni vema itikadi za vyama zikawekwa pembeni na kuweka utaifa mbele.

  Maafisa wa TAKUKURU wanapomtuhumu mtu au kumfikisha mtuhumiwa yeyote mahakamani, wanafanya hivyo kwa niaba ya rais.
  Sasa inakuwaje rais huyohuyo acheke na kukumbatiana na watuhumiwa jukwaani? Inakuwaje awainue mikono, aseme anawaamini na kuwaombea kura kwa wananchi?
  Mapema mwanzoni mwa utawala wake, Kikwete aliwateua kuwa mawaziri watu wa namna ya Andrew Chenge na Mramba hata kama kulikuwa na kelele na manung'uniko mengi kuhusu uadilifu wao.

  Ilioekana hilo lilitosha, lakini yaelekea sikio la kufa halisikii dawa. Baada ya hapo Kikwete aliendelea kuwateua, katika nafasi mbalimbali, maafisa waliohusika katika kashfa za ukwapuaji wa mabilioni ya shilingi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).
  Ifike mahali swali hili lijibiwe: Kwa nini mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete hachukii uhalifu na watuhumiwa wa uhalifu? Nani anayetamani rais wa namna hii?

  Source: Mwanahalisi toleo no. 208
  =====================================

  My take: Watanzania tutakuwa tumerogwa tukimchagua tena Kikwete kuwa raisi wa nchi hii. Sema hapana kwa Kikwete rafiki wa majambazi na mafisadi.
   
Loading...