Rais anatumia kodi zetu vibaya, Royal Tour yake haina faida ni Ufujaji wa pesa za Maskini

Akikaa mkoa mmoja kwa muda mwingi tunamsemaaaaa, akitembelea wananchi tunamseeemaaa hatuishiwi manenoo

kikubwa tunatumaini tutapata mrejesho (short run and long term effect) za royal tour
 
Rais alipaswa afikirie mambo makubwa ya msingi na kuachana na uigizaji anaoufanya kwa kutumia pesa zetu vibaya. Toka ameteuliwa kuwa Rais anazunguka tu.

Hatulii kufanya kazi. Nchi hii watu wanaiba ye hana hata habari ana talii tu. Haya mambo ni ufujaji wa pesa za umma. Badala yake ndo mnapandisha bei ya bidhaa na pia kodi mkiongeza na tozo.

Huu ni wizi wa mchana kweupe
1. Ni bora wazawa wangetumika kuchukua filamu hiyo na kandarasi ya kimkataba kuwekwa kwa ajili ya kutangaza duniani kuliko kukodi wazungu ambapo hati miliki bila shaka itakuwa kwao halafu maka ya mbeleni wajukuu wataidai irejeshwe
2. Ni bora utalii wa ndani ungehamasishwa kwa wingi kwa taratibu zisizo ngumu kufuatwa kabla ya kupewa nafasi ya kutembelea kupunguza muda wa kupoteza na gharama nafuu
3. Kuna hatari ya hili suala huko mbeleni kuibuliwa kama uhjumu uchumi wa nchi licha ya kuwepo kinga ya kushitakiwa maana hapatakuwa na matokeo yoyote ya maana kwa manufaa ya wananchi
4. Mpaka sasa ilitakiwa waziri wa utalii na waziri wa mambo ya nje wangekuwa tayari wamejiuzulu kwa kushindwa kufanya ubunifu wa kutosha kutangaza na kuvutia utalii wa rasirilimali za nchi
5. Katika mradi huu kuna baadhi watatumia isivyo wakijificha nyuma ya kivuli cha mkuu wa nchi
 
Rais alipaswa afikirie mambo makubwa ya msingi na kuachana na uigizaji anaoufanya kwa kutumia pesa zetu vibaya. Toka ameteuliwa kuwa Rais anazunguka tu.

Hatulii kufanya kazi. Nchi hii watu wanaiba ye hana hata habari ana talii tu. Haya mambo ni ufujaji wa pesa za umma. Badala yake ndo mnapandisha bei ya bidhaa na pia kodi mkiongeza na tozo.

Huu ni wizi wa mchana kweupe
Tungeambiwa bei gani kurekodi hiyo filamu na kama procurement ya hiyo kampuni ilifanyikaje. Pia tuambiwe kama tunatarajia kuvuna kiasi gani. Hiyo biashara huenda ikaishia patupu huku wenye kushauru venture kama hizo wakijipatia mamilioni. Nina shaka na katibu mkuu kiongozi wa sasa. Hapendi show ila huenda ni mpigaji.
 
Ponda mali kufa kwaja...

Wanasiasa wote ni wale wale, hata mie nikiingia kwenye siasa na nikapata kitengo... Lazima keki ya taifa niitafune vilivyo.
 
Kwani waziri anayehusika na utalii hayupo, mabalozi hawapo? kama mnataka kusikika duniani tumieni watu maarufu mfano wanamziki, wacheza mpira nk. yaleyale ya kule msoga yanaanza kurudi kidizaini.......bora mzee wa msoga alikuwa hatubambikii tozo.
 
Hata tozo mlibeza...baada ya kusikia fedha zimepelekwa kujenga vituo vya afya,mkaombwa muandikwe kwenye vibao.

Mwacheni Mama Samia afanye kazi zake.
Kazi gani? Ya kuzurura? Tozo ni wizi mwingine wa Serikali kwa watu wake
 
Rais alipaswa afikirie mambo makubwa ya msingi na kuachana na uigizaji anaoufanya kwa kutumia pesa zetu vibaya. Toka ameteuliwa kuwa Rais anazunguka tu.

Hatulii kufanya kazi. Nchi hii watu wanaiba ye hana hata habari ana talii tu. Haya mambo ni ufujaji wa pesa za umma. Badala yake ndo mnapandisha bei ya bidhaa na pia kodi mkiongeza na tozo.

Huu ni wizi wa mchana kweupe
Mkuu umesema..

"Nchi hii watu wanaiba na hana habari"

mimi sikatai wala sikubali..ninachokuomba tuwekee hapa mifano hata mi 3 tu ya watu wanaoiba/walioiba na kiasi walichoiba.

Asante mkuu

Sent from my Infinix X572 using JamiiForums mobile app
 
Bora hata ya huyo kuliko yule anayetumia mabilioni kujenga uwanja wa kuanikia mpunga kijijini kwao, badala ya kuhamasisha utalii yeye anauwa hao wanyama wenyewe kwa kuwahamasisha kutoka walipozoea na kuwapeleka sehemu nyingine matokeo yake wanashindwa kuhimili hali ya hewa wanakufa,kusema kweli kuna mijitu mijinga sana mpaka unajiuliza jitu kama hilo Mungu aliliumbia nini? Bora angelifanya kuwa jiwe tu.
 
Rais alipaswa afikirie mambo makubwa ya msingi na kuachana na uigizaji anaoufanya kwa kutumia pesa zetu vibaya. Toka ameteuliwa kuwa Rais anazunguka tu.

Hatulii kufanya kazi. Nchi hii watu wanaiba ye hana hata habari ana talii tu. Haya mambo ni ufujaji wa pesa za umma. Badala yake ndo mnapandisha bei ya bidhaa na pia kodi mkiongeza na tozo.

Huu ni wizi wa mchana kweupe
mmekataa kulipa toto hapa halafu mnasema kuna pesa yenu- pesa yenu ipi? acheni dharau
 
Rais alipaswa afikirie mambo makubwa ya msingi na kuachana na uigizaji anaoufanya kwa kutumia pesa zetu vibaya. Toka ameteuliwa kuwa Rais anazunguka tu.

Hatulii kufanya kazi. Nchi hii watu wanaiba ye hana hata habari ana talii tu. Haya mambo ni ufujaji wa pesa za umma. Badala yake ndo mnapandisha bei ya bidhaa na pia kodi mkiongeza na tozo.

Huu ni wizi wa mchana kweupe
tusipofanyanwatasema tukifanya wanasema bora tufanye ili wakiuliza tuwaonyeshe tulichofanya

ni busara za hali ya juu sana mama mwacheni afanye tu
 
Back
Top Bottom