Rais anapovunja Katiba kwa kauli ya kibaguzi

Zakaria Lang'o

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
2,593
2,767
Watanzania wenzangu jana huko Rufiji kwa Mbunge Bwege, Rais Magufuli ametoa Kauli yenye ukakasi mkubwa. Baada ya wananchi kueleza shida yao ya kupata Stendi, Rais alisikika akiwaambia kuwa kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 aliwaomba wamchagulie mtu kutoka CCM, wao wakamchagua Bwege. Hivyo aliwataka wamwambie huyo Bwege awajengee Stendi.

Hii ni Kauli ya kibaguzi na ambayo imetolewa na mtu ambaye aidha hafahamu kuwa kuna Ibara ya Katiba inakataza matamshi ya kibaguzi ya aina hii au anaelewa isipokuwa anaamini kwamba kwa kuwa ni Rais basi hawajibiki kufuata kilichomo kwenye Katiba ya Nchi.

Hebu tuangalie Katiba ya Nchi inasemaje kuhusu maana ya neno "ubaguzi:'

Ibata ya 9: (g) kwamba serikali na vyombo vyake vyote vya umma vinatoa nafasi zilizo sawa kwa raia wote, wake kwa waume, bila kujali Rangi, kabila, dini au Hali ya mtu.
(k) kwamba nchi inatawaliwa kidemokrasia na ujamaa."
Ibara ya 8 (1) "Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi inayofuata misingi ya demokrasia na haki za kijamii..."
Ibara ya 13(4) "Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu au mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria yoyote au utekelezaji wa kazi au shughuli yoyote ya mamlaka ya nchi."

(5) "kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya ibara hii neno " kubagua" maana yake ni kutimiza haja, haki, au mahitaji mengineyo kwa watu mbalimbali kwa kuzingatia utaifa wao, kabila, pahala wanapotokea, maoni ya kisiasa, rangi, dini, jinsia au hali yao ya maisha kwa namna ambayo watu wa aina fulani wanafanywa au kuhesabiwa kuwa dhaifu au duni na kuwekewa vikwazo au masharti ya vipingamizi ambapo watu wa aina nyingine wanatendewa tofauti, au wanapewa fursa au faida iliyoko nje ya masharti au sifa za lazima..."

Hiyo ndiyo Katiba ya Jamhuri. Inakataza ubaguzi wa kupeleka maendeleo kwa Wana CCM tu kwa sababu kwamba yeye Rais anataka kufanya kazi na Wana CCM tu.

Kuna mtu atasema rais alikuwa anafanya siasa, kama ni hivyo basi hizo zitakuwa ni siasa za maji taka (gutter politics) ambazo ndizo hasa zinakatazwa na ibara za Katiba nilizoanisha hapo juu.

Ni rai yangu kwa wananchi wa Tanzania kuwa kwa kuwa tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu mwezi Oktoba, basi wasimrejeshe madarakani mtawala anayedharau katazo la Katiba ya Nchi na kuamua kuwabagua kwa dhahiri.

Baba wa Taifa hili Mwalimu Nyerere aliwahi kusema: "Ubaguzi ni sawa na kula nyama ya mtu,..." Mtu huyo ataendelea kula nyama zaidi na zaidi.

Tumeona Waislamu wanalalamika kuwa wanabaguliwa katika utawala wa nchi, tumeona wananchi wakilalamika kuwa Chato inapendelewa ki maendeleo, tumesikia watu wakidai Wasukuma wanapewa madaraka kwa wingi japokuwa inajulikana kuwa usomi wao ni hafifu. Yote hayo husababishwa na roho ya ubaguzi iliyozama ndani mtawala.

Tusijidanganye kuwa ataishia kwenye ubaguzi wa kiitikadi za kisiasa pekee. Atazama zaidi.

Ndiyo maana leo Makabila yanaonekana ni watu wasiohitajika katika nafasi za juu katika taasisi za Ujenzi wa nchi wakati ukweli i kwa Kuna wasomi mahiri wengi huko katika makabila hayo kuliko katika makabila mengine nchini. Yote haya ni mazao ya ubaguzi. Tusikubali.
Come Octoba, piga chini mbaguzi na mdharau Katiba.

Asanteni.
 
Hakuna rais , mtu mishipa imemtoka kama kama nini kila kitu nguvu,mwambieni wilaya ya kongwa na mpwapwa hali mbaya kuna mbunge wa upinzani?

Siku ya Leo Nawakumbuka Wote Ambao Wapo Magereza Kwa Kesi Ambazo Dhamana Zipo Wazi Ila Kwa Makusudi ya Serikali Wamenyimwa, na Wale Ambao Kesi Zao Zinapigwa Kalenda Kila Zinapotajwa. Tito, Theo, Mwaipaya Pamoja na Masheikh Niwatakie EidMubarak. Mwenyenzi Mungu Awalinde.
 
Kauli zake ndo wateule wake wa chini wanazotumia...bongo bht mby jaman.
Hatujapata kiongozi wa kitaifa....Hovyo hovyo hovyo
 
Halafu Msajili wa Vyama vya Siasa atkuambia hajasikia hiyo kauli...
 
Hakuna rais , mtu mishipa imemtoka kama kama nini kila kitu nguvu,mwambieni wilaya ya kongwa na mpwapwa hali mbaya kuna mbunge wa upinzani?

Siku ya Leo Nawakumbuka Wote Ambao Wapo Magereza Kwa Kesi Ambazo Dhamana Zipo Wazi Ila Kwa Makusudi ya Serikali Wamenyimwa, na Wale Ambao Kesi Zao Zinapigwa Kalenda Kila Zinapotajwa. Tito, Theo, Mwaipaya Pamoja na Masheikh Niwatakie EidMubarak. Mwenyenzi Mungu Awalinde.
Asante mkuu. Hivi karibuni Mbunge wa Kishapu Selemani Nchambi kakamatwa na mabunduki 16 ya kuulia wanyama Serengeti akiyamiliki kinyume cha sheria, akapewa adhabu ndogo na mahakama tena harakaharaka utadhani hakimu ni shemeji yake; huku Jaji wa Kanda ya Kati Dodoma akijifanya kuugua kila vijana wa Chadema wakipelekwa mahakamani kupata haki yao. Yaani hata Majaji wamesahau msemo wao maarufu wa: "justice delayed is justice denied!!!"
Tukisema eti tunaingilia Uhuru wa Mahakama.
Hivi kama huyu Jaji angeenda hospitali kutibiwa, akaambiwa daktari ni mgonjwa hivyo arudi siku nyingine ndipo atibiwe je, angeona ametendewa haki na waganga!!?
 
Kwa kweli kuna saa nabaki tu kumuombea Mh. sana Mwenyekiti wangu.

Nafikiri kuna saa mambo yanakuwa mengi sana na kumlemea.

Pia, kuna haja kujali nafasi ya za juu za nchi kwa kupima afya za viongozi mara kwa mara.

Vilevile, kitengo kwa uhalisia kinapaswa kuwa na watalaam wa kila nyanja. Hawa walipaswa kuwa na uelewa wa mood ya kiongozi na vitu gani vinavyosababisha kuharibu mood ili wakwepe pale inapobidi.

Haikuwepo sababu yeyote ya Mh. Rais kuhutubia baada ya kutoka kwenye msiba wa mtu aliyehusika kwa karibu sana na maisha yake ya siasa.

Idara ya usalama wa taifa ni taasisi ndani ya taasisi ya Urais, hivyo ina mamlaka na uwezo wa kumcontrol Rais kwa maslahi ya nchi na afya yake.
 
Back
Top Bottom