Rais anapounga mkono 'Mgomo' katika nchi anayoiongoza inatupa picha gani

Rais asijue bei elekezi ya korosho hadi inaanza kutumika, ila hoja yangu kuu ninahoji tangu lini rais aunge mkono mgomo wowote ule hakuwa na lugha nyingine zaidi ya kusema anaunga mkono mgomo.
Kwaiyo wewe ulitaka atumie lugha gani?
 
wakati tatizo wamelileta wao?!!utengeneze tatizo kisha ujifanye unalitatua halafu upewe sifa!!!tena msimu uliopita watu waliyaona hayo na kusema waliishia kubezwa na vitisho tu!!!
Hebu twambie hilo tatizo amelitengeneza vipi?
 
Hiki kichwa changu sometime hata mimi huwa sikielewi vizuri maana kinajiuliza hivi kwani beiza mazao yetu zinapangwa na serkali zetu au soko la dunia? Mfano serkali iseme bei iwe kilo ya korosho 4500 soko la dunia liwe 1750. Je hapa nani atatunisha msuli serkali. Vs soko la dunia. Kichwa changu mbona kina ni let down?
 
Rais kwanza angewawajibisha waliopanga bei elekezi ya chini .kama korosho zipaswa kuuzwa kwa tsh 5,000/=+ sababu gani bei elekezi iwe 1550/=.pengene angetumbua hawa ujumbe ungekua imara zaidi.
 
Wakati serikali inapanga bei elekezi yeye alikuwa likizo? au ni mwendo wa kutengeneza tatizo ili baadaye uonekane unalitatua.

Tuseme anapinga maamuzi ya serikali yake.
ndiyo maana hata kaimu wa bodi ya korosho katumbuliwa kwa maamuzi hayo ya bei elekezi....
 
MANENO mengi pumba tupu walahi
Chromosome retard walahi

karibu ustadhi
1540704504590.png
 
Jana Rais Magufuli alinukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari kuwa anaunga mkono mgomo wa wakulima wa korosho kutopeleka mazao yao kwenye mnada, pamoja na lengo zuri la Rais haoni kuwa anayajengea uhalali na makundi mengine kufanya migomo yakitegemea Rais atakuwa nyuma yao. Na je, kukitokea uvunjifu wa amani au uharibifu wa mali (mazao) kipindi cha mgomo huo rais atakwepaje lawama.

Kama rais ameamua kuwaunga mkono wanaogoma basi asiishie kwa wakulima wa korosho peke yake kwa sababu wenye matatizo kama hayo wapo wengi, tunaomba awahimize pia wakulima wa pamba, kahawa, alzeti nao wagome.

Siku Madaktari au Walimu wakigoma wakihitaji nyongeza ya mishahara, je rais atakuwa nyuma yao na kuwapongeza kama alivyofanya kwa wakulima wa korosho au atawapelekea FFU au atawaambia kama wanaona mshahara hautoshi waache kazi.

Binafsi naona motive behind ya sakata la korosho liko kisiasa zaidi ya kumsaidia mkulima. Kama bei elekezi ya serikali ni sh.1,550 kwa kilo na mfanyabiashara ananunua korosho kwa sh. 2,700/kilo, hapo nani anamnyanyasa mkulima serikali au mfanyabiashara.

Rais anapopinga maamuzi ya serikali (bodi ya korosho) iliyopanga bei elekezi ina maana yuko kinyume na serikali yake?
Mkuu hili suala hata Mimi nimejaribu kulifikiria sana.

Tuanzie kwa Kaimu wa Bodi ya Korosho ambaye inasemekana alikuwa anatembea na askari kwenda kwa watu wa vyama vya msingi, Hivi ni kweli anaweza kuamua mwenyewe bila ya kuwa na MTU nyuma yake? Na je, mbona karudishwa wizarani badala ya kuchukuliwa hatua?

Suala LA BEI dira ya Korosho; Wataalam walio panga BEI hiyo wamesema kuwa inaleta faida ya 20% baada ya kutoa gharama, iweje BEI ya 2700 ionekane ndogo?

Tukirudi kwenye suala la Serikali kuingia kati, mbona watu wa kusini hao hao waliuza mbaazi kwa Tzs 150-200/= kutoka Tzs 1800 - 2000/= ya mwaka Jana na serikali kupitia naibu waziri Eng. Manyanya alisema wasifikirie kuuza tu wanaweza kuzila wenyewe?

Ninachokiona hapa, kutokana maamuzi ya serikali kunyakua fedha za ushuru wa mauzo ya nje zaidi ya bil 200 naona kuna mchezo wanacheza ili ikitokea BEI imeongezeka ionekane serikali ipo Pamoja na Wakulima, labda kama WAHINDI watatishwa waongeze BEI kutoka ya sasa.

Upande wa pili kama BEI itabakia kama ilivyo, Serikali itafanya nini? Kwa sababu kwenye hili naona wanatumia nguvu nyingi kuliko diplomasia.

Mwaka Jana Korosho iliweza kuiingizia serikali fedha ya kuhudumia wizara moja, achilia mbali ziada ya fedha za Wakulima za "Export Levy"
 
Back
Top Bottom