Rais anapounga mkono 'Mgomo' katika nchi anayoiongoza inatupa picha gani

Mleta mada umeandika meengi, kumbe manyoya tu. Sasa kwako mgomo wa wewe kutouza mazao uliyolima mwenyewe na Daktari kugoma kumtibu mgonjwa ni sawa??
 
Hahahahahahah mkuu ukiwa mzoefu na siasa za kitanzania hupati shida.Leo Rais aseme bei ni hii,yaani hadi wewe utakua Miongoni mwa watakao sema one man show, ooh ttz katengeneza mwenyewe na kalitatua mwenyewe mara anatafuta kiki nk.Mwache Jpm apige kazi

Rais akifanya lenye tija tutamuunga mkono na kuambiwa one man show ndio vionjo vyenyewe vya demokrasia. Mbona nilimuunga mkono kwenye kuondoa service charge ya umeme? Hili la bei ya korosho rais hawezi kukwepa ni udhaifu wa maamuzi yake na serekali anayoiongoza.
 
Mleta mada umeandika meengi, kumbe manyoya tu. Sasa kwako mgomo wa wewe kutouza mazao uliyolima mwenyewe na Daktari kugoma kumtibu mgonjwa ni sawa??
Mgomo ni mgomo tu maana yake ni kupinga au kutokubaliana na jambo fulani, hoja yangu ni pale rais wa nchi anapounga mkono mgomo anapeleka ujumbe gani kwa kada zingine, je wakiamua kuandamana ataungana nao.
 
Kama mnachukia kukosolewa, kwa generation hii mtapata taabu sana.

Bad timing for this presidency.
Hakuna anayechukia kukosolewa sema wengi wa bavicha hamjui KUKOSOA na KUPINGA au kutukana Matusi. Nilikua sina ttz na uwezo wa ELIMU yaani FIKRA juu ya bavicha, lkn baada ya 2015 napata shida sana kujua bavicha wanauelewa wwt au lah.
 
Hakuna anayechukia kukosolewa sema wengi wa bavicha hamjui KUKOSOA na KUPINGA au kutukana Matusi. Nilikua sina ttz na uwezo wa ELIMU yaani FIKRA juu ya bavicha, lkn baada ya 2015 napata shida sana kujua bavicha wanauelewa wwt au lah.
Una akili ndogo sana.
 
Inatupa picha kuwa anajali kero za wananchi wake na yupo tayari kuunga mkono mgomo au madai yenye msingi.
wakati tatizo wamelileta wao?!!utengeneze tatizo kisha ujifanye unalitatua halafu upewe sifa!!!tena msimu uliopita watu waliyaona hayo na kusema waliishia kubezwa na vitisho tu!!!
 
Jana Rais Magufuli alinukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari kuwa anaunga mkono mgomo wa wakulima wa korosho kutopeleka mazao yao kwenye mnada, pamoja na lengo zuri la Rais haoni kuwa anayajengea uhalali na makundi mengine kufanya migomo yakitegemea Rais atakuwa nyuma yao. Na je, kukitokea uvunjifu wa amani au uharibifu wa mali (mazao) kipindi cha mgomo huo rais atakwepaje lawama.

Kama rais ameamua kuwaunga mkono wanaogoma basi asiishie kwa wakulima wa korosho peke yake kwa sababu wenye matatizo kama hayo wapo wengi, tunaomba awahimize pia wakulima wa pamba, kahawa, alzeti nao wagome.

Siku Madaktari au Walimu wakigoma wakihitaji nyongeza ya mishahara, je rais atakuwa nyuma yao na kuwapongeza kama alivyofanya kwa wakulima wa korosho au atawapelekea FFU au atawaambia kama wanaona mshahara hautoshi waache kazi.

Binafsi naona motive behind ya sakata la korosho liko kisiasa zaidi ya kumsaidia mkulima. Kama bei elekezi ya serikali ni sh.1,550 kwa kilo na mfanyabiashara ananunua korosho kwa sh. 2,700/kilo, hapo nani anamnyanyasa mkulima serikali au mfanyabiashara.

Rais anapopinga maamuzi ya serikali (bodi ya korosho) iliyopanga bei elekezi ina maana yuko kinyume na serikali yake?
We are still in verge of knowing no.....sorry for us all....
 
Inatupa picha kuwa ni Rais aliyekosa msimamo,leo awatishie kuwafukuza wabunge 11 wa CCM wanaowapigania wananchi wanaozurumiwa kwenye korosho kesho aungane na wananchi kwenye mgomo kwa jambo lilelile alilotaka kuwafukuza wabunge 11 na waziri mkuu wao.
 
Wakati serikali inapanga bei elekezi yeye alikuwa likizo? au ni mwendo wa kutengeneza tatizo ili baadaye uonekane unalitatua.

Tuseme anapinga maamuzi ya serikali yake.
Ndio tabia yao sasa hivi kutengeneza tatizo halafu wanalitafutia ufumbuzi. Wanajua kuna wajinga wa kutosha kuwaamini kuwamwagia sifa. Kipindi kile alisema atapiga shangazi za watu na leo shangazi hao hao wanaungwa mkono ili kuwasahaulisha. Anajua jinsi walivyo wasahaulifu. Na kuna mashangazi wa kike na wa kiume humu wamefunga vibwebwe kumwaga sifa.
 
Kumbukumbu zinaniambia aliwahi toa kauli ya kupiga hadi shangazi zao,leo anawaunga mkono!
"Maisha bila Unafiki hayaendi"
 
Back
Top Bottom