Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inatoa ulinzi dhidi ya mashtaka kwa rais aliyepo madarakani na aliyestaafu katika Ibara ya 46(3) ya katiba.
Ibara hiyo inasema; "Isipokuwa kama hataacha kushika madaraka ya rais kutokana na masharti ya ibara ya 46A (10), itakuwa ni marufuku kumshtaki au kufungua mahakamani shauri lolote la jinai au kumdai mtu aliyekuwa anashika madaraka ya rais baada ya kuacha madaraka hayo kutokana na jambo lolote alilofanya yeye kama rais wakati alipokuwa bado anashika madaraka ya rais kwa mujibu wa Katiba hii".
Ufafanuzi unaopatikana katika kifungu cha 46A (10), unasema kuwa rais mstaafu anayeweza kushtakiwa kwa kosa la jinai au madai ni yule aliyeondolewa madarakani kwa azimio la bunge baada ya mashtaka dhidi yake (bungeni) kuthibitika.
Kifungu hicho kinasema, "Endapo Bunge litapitisha azimio kuwa mashtaka dhidi ya rais yamethibitika na kwamba hastahili kuendelea kushika kiti cha rais, spika atawafahamisha rais na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi juu ya azimio la bunge, na hapo rais atawajibika kujiuzulu kabla ya siku ya tatu tangu bunge lilipopitisha azimio hilo