Rais anapoteua Mawaziri wenye uwezo mdogo, Ukisema Waziri fulani ana uwezo mdogo, Je ni kumwingilia Rais katika uteuzi?

Wanabodi,

Huu ni uzi wa swali tuu,
Rais Anapoteua Mawaziri wenye uwezo mdogo, Ukisema Waziri Fulani ana uwezo mdogo , Jee ni Kumwingilia Rais Katika Uteuzi?.

Tanzania ni nchi yetu sote, watu wenye mamlaka kuu kuhusu nchi hii ni "we the people" kupitia katiba ya JMT, tumechagua viongozi wetu akiwemo rais wa JMT, ambaye tumemuajiri kwa kura zetu na kumlipa mshahara kwa kodi zetu, hivyo we are the boss!.

Ili rais wetu atimize majukumu yake vizuri, tumempa mamlaka ya kuteua wasaidizi wake kwa uhuru bila kuingiliwa. Miongoni mwa wasaidizi hawa ni mawaziri na manaibu mawaziri.

Inapotokea baadhi ya mawaziri hawa ni hawana uwezo kabisa, japo wana ma cheti ya kuhitimu, lakini vichwani ni watupu kabisa, ni weupe, hawawezi kumsaidia kitu rais, jee kuna ubaya kumwambia rais waziri fulani anauwezo mdogo na hakusaidii?.

Inapotokea mtu baki kama mimi, nikamuona waziri fulani ana uwezo mdogo, jee kumtaja kwa jina waziri fulani kuwa ana uwezo mdogo, jee huku kutakuwa ni kumwingilia rais katika powers zake za uteuzi, au ni kumsaidia kujua kuwa kwenye line-up yake, licha ya kuwa na majembe yanayomsaidia lakini pia kuna viazi ambavyo haviwezi kumsaidia chochote.

Juzi kati nilipata fursa ya kuangalia kwenye TV, mahojiano ya naibu waziri fulani, kiukweli kabisa, ni hajui kitu mpaka basi!. Jee tukimtajia rais Magufuli kuwa mteule huyu hajui kitu, huku ni kumwingilia au ni kumsaidia?.

NB. Naombeni kwa heshima ya mamlaka ya uteuzi, tusichangie kwa kutaja majina yoyote ya mawaziri hawa wasio na uwezo , kuwataja majina ni kuwadhalilisha, ukiwadhalilisha wateule wa rais, ni kumdhalilisha rais!, ila kiukweli sisi watu wa kujiuliza, ukimuona mtu ni hana uwezo hata kabla hajateuliwa, halafu anakuja kuteuliwa, unajiuliza hivi mteule alikuwa anatumia vigezo gani kuwateua mawaziri hawa?!.

Nawatakia Jumapili Njema.
Paskali.
Hili swali bado liko valid.
P
 
Back
Top Bottom