Rais anapoteua Mawaziri wenye uwezo mdogo, Ukisema Waziri fulani ana uwezo mdogo, Je ni kumwingilia Rais katika uteuzi?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,468
113,583
Wanabodi,

Huu ni uzi wa swali tuu,
Rais Anapoteua Mawaziri wenye uwezo mdogo, Ukisema Waziri Fulani ana uwezo mdogo , Jee ni Kumwingilia Rais Katika Uteuzi?.

Tanzania ni nchi yetu sote, watu wenye mamlaka kuu kuhusu nchi hii ni "we the people" kupitia katiba ya JMT, tumechagua viongozi wetu akiwemo rais wa JMT, ambaye tumemuajiri kwa kura zetu na kumlipa mshahara kwa kodi zetu, hivyo we are the boss!.

Ili rais wetu atimize majukumu yake vizuri, tumempa mamlaka ya kuteua wasaidizi wake kwa uhuru bila kuingiliwa. Miongoni mwa wasaidizi hawa ni mawaziri na manaibu mawaziri.

Inapotokea baadhi ya mawaziri hawa ni hawana uwezo kabisa, japo wana ma cheti ya kuhitimu, lakini vichwani ni watupu kabisa, ni weupe, hawawezi kumsaidia kitu rais, jee kuna ubaya kumwambia rais waziri fulani anauwezo mdogo na hakusaidii?.

Inapotokea mtu baki kama mimi, nikamuona waziri fulani ana uwezo mdogo, jee kumtaja kwa jina waziri fulani kuwa ana uwezo mdogo, jee huku kutakuwa ni kumwingilia rais katika powers zake za uteuzi, au ni kumsaidia kujua kuwa kwenye line-up yake, licha ya kuwa na majembe yanayomsaidia lakini pia kuna viazi ambavyo haviwezi kumsaidia chochote.

Juzi kati nilipata fursa ya kuangalia kwenye TV, mahojiano ya naibu waziri fulani, kiukweli kabisa, ni hajui kitu mpaka basi!. Jee tukimtajia rais Magufuli kuwa mteule huyu hajui kitu, huku ni kumwingilia au ni kumsaidia?.

NB. Naombeni kwa heshima ya mamlaka ya uteuzi, tusichangie kwa kutaja majina yoyote ya mawaziri hawa wasio na uwezo , kuwataja majina ni kuwadhalilisha, ukiwadhalilisha wateule wa rais, ni kumdhalilisha rais!, ila kiukweli sisi watu wa kujiuliza, ukimuona mtu ni hana uwezo hata kabla hajateuliwa, halafu anakuja kuteuliwa, unajiuliza hivi mteule alikuwa anatumia vigezo gani kuwateua mawaziri hawa?!.

Nawatakia Jumapili Njema.
Paskali.
 
Mkuu Pascal, kwanza terminology uliyotumia "kiazi' ni relative term nikimaanisha kuwa mtu anaweza kuwa kiazi katika jambo fulani na akawa genius/dhahabu katika jambo jingine. Kwa maana hiyo NW huyo huenda ni kiazi kweli kweli katika masuala alokuwa anayazungumzia ila kuna sehemu naye ni mtabe kweli kweli.

Swali lako la msingi kuwa ni kosa kumsema mteule kama ni kiazi .... kwa maoni yangu kama mtu anaweza kuthibitisha kwamba Mhe. rais, fulani bin fulani ni kiazi haswa na ushahidi ni huu hapa nadhani hatakuwa amekosea bali atakuwa amelisaidia taifa!! Anyway, I'm just thinking louder from this acute angle.
 
Ukiwaangalia usoni Mawaziri wengi huwa naishia kucheka sana sana

Waziri anacheka Kama analia, Waziri anafoka huku haelewi anafoka kwa sababu gani?

Nilichogundua mawaziri wengi uwezo wa kufikiri na kuamua ni mdogo sana sana, Wengi hawaelewi kazi ya waziri ni ipi?

Pascal wewe unafahamu ukiwa mwandishi wa habari lazima ujue upo kwenye tukio au mkutano kwa kazi ipi? Usipojua kazi yako Ndio wale waandishi tunaowadharau .

Waziri wa Mifugo au kilimo hata mbuzi hana kwanza alisomea degree ya American war, Sasa American war na Kilimo kweli?

Waziri wa afya alisomea Sheria tena sheria za kipuuzi, Hivi huyu waziri ana uelewa na Journal za afya, Utamkuta anaongelea afya huku anatetemeka na sauti ya kuimbia kwaya kanisani,

Yule wa utalii kutwa na Fimbo kama Babu sasa utalii na fimbo wapi na wapi, Badala ya kujikita kuvutia wawekezaji yeye kutwa na fimbo maporini
 
Mkuu leo nimekukubali!
 
Hahaaa! Imebidi nicheke tu!
 
Wanabodi,

Huu ni uzi wa swali tuu,
Rais Anapoteua Mawaziri Viazi, Ukisema Waziri Fulani ni Kiazi, Jee ni Kumwingilia Rais Katika Uteuzi?.

Tanzania ni nchi yetu sote, watu wenye mamlaka kuu kuhusu nchi hii ni "we the people" kupitia katiba ya JMT, tumechagua viongozi wetu akiwemo rais wa JMT, ambaye tumemuajiri kwa kura zetu na kumlipa mshahara kwa kodi zetu, hivyo we are the boss!.

Ili rais wetu atimize majukumu yake vizuri, tumempa mamlaka ya kuteua wasaidizi wake kwa uhuru bila kuingiliwa. Miongoni mwa wasaidizi hawa ni mawaziri na manaibu mawaziri.

Inapotokea baadhi ya mawaziri hawa ni viazi kabisa, japo wana ma cheti ya kuhitimu, lakini vichwani ni watupu kabisa, ni weupe, hawawezi kumsaidia kitu rais, jee kuna ubaya kumwambia rais waziri fulani ni kiazi na hakusaidii?.

Inapotokea mtu baki kama mimi, nikamuona waziri fulani ni kiazi, jee kumtaja kwa jina waziri fulani kuwa ni kiazi, jee huku kutakuwa ni kumwingilia rais katika powers zake za uteuzi, au ni kumsaidia kujua kuwa kwenye line-up yake, licha ya kuwa na majembe yanayomsaidia lakini pia kuna viazi ambavyo haviwezi kumsaidia chochote.

Juzi kati nilipata fursa ya kuangalia kwenye TV, mahojiano ya naibu waziri fulani, kiukweli kabisa, ni kiazi mpaka basi!. Jee tukimtajia rais Magufuli kuwa mteule huyu ni kiazi, huku ni kumwingilia au ni kumsaidia?.

NB. Naombeni kwa heshima ya mamlaka ya uteuzi, tusichangie kwa kutaja majina yoyote ya viazi hawa, kuwataja majina ni kuwadhalilisha, ukiwadhalilisha wateule wa rais, ni kumdhalilisha rais!, ila kiukweli sisi watu wa kujiuliza, ukimuona mtu ni kiazi hata kabla hajateuliwa, halafu anakuja kuteuliwa, unajiuliza hivi mteule alikuwa anatumia vigezo gani kuwateua viazi hawa?!.

Nawatakia Jumapili Njema.
Paskali.
PASCO ,Rais ni mchaguliwa wa wananchi.
Mteule wake akibronga, sawa na Rais kuboronga.
Wananchi wana kila haki kusema mtu uliyetuletea hatuhudumi kwa viwango tunavyotaka wananchi.
Na hilo laweza mpunguzia kura Rais huko mbeleni.

Rais si malaika, akikosea hata yeye lazima anyooshewe kidole, unless tunaanza kuingiza mentality ya utawala wa kifalme.
 
Back
Top Bottom