Rais anaposhindwa kutolea maamuzi vikwazo wapatavyo watendaje wake humanisha nini??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais anaposhindwa kutolea maamuzi vikwazo wapatavyo watendaje wake humanisha nini???

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nsimba, Mar 24, 2011.

 1. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #1
  Mar 24, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hebu soma kipisi hiki cha habari wakati rais akitembelea wizara ya uchukuzi: (IPPMEDIA 23 machi 2011)

  "Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), Israel Sekirasa, amelichongea Jeshi la Polisi nchini kwa Rais Jakaya Kikwete kuwa ndiyo kikwazo cha udhibiti wa daladala korofi nchini kwa kuwa nyingi zinamilikiwa na maofisa wake. Sekirasa aliyasema hayo jana wakati wa ziara ya Rais Kikwete katika Wizara ya Uchukuzi baada ya kupewa nafasi na Rais Kikwete kuzungumzia utendaji wa mamlaka yake. Alisema suala la kudhibiti daladala korofi linakuwa gumu kwa kuwa kuna mgongano wa kimaslahi kwa wasimamizi wa Sheria ya Usalama Barabarani na ndiyo sababu suala la kuzikabili daladala korofi inaonekana kama limeshindikana. Sekirasa alianza kwa kusema kimafumbo bila kufafanua kauli yake, lakini baada ya kubanwa na Rais Kikwete afafanue ndipo akataja bayana kuwa daladala nyingi zinazoonekana barabarani zinamilikiwa na maofisa wa polisi, hivyo kazi hiyo inakuwa ngumu.

  “Mheshimiwa Rais, kazi ya kupambana na daladala barabarani inakuwa ngumu kwa sababu ya conflict of interest (mgongano wa kimaslahi) baina ya wasimamizi wa sheria, kazi inakuwa ngumu na ndo sababu wakati fulani tuliamua kuikodisha kampuni binafsi (Majembe Auction Mart) ifanye kazi hiyo,” alisema.
  Baada ya Sekirasa kuzungumza bila kueleza bayana mgongano huo wa maslahi na wasimamizi wa sheria, Rais Kikwete aliingilia kati na kumtaka afafanue inakuwaje wasimamizi wa sheria wanakuwa na mgongano wa kimaslahi na utekelezaji wa sheria za usalama barabarani.

  “Mgongano wa kimaslahi unatoka wapi, na ni kati ya Jeshi la Polisi na nini?” alihoji Rais Kikwete ndipo Sekirasa akaweka wazi kuwa daladala nyingi zinamilikiwa na askari na ndiyo sababu wakiambiwa wadhibiti daladala wanalegalega.
  Baada ya kauli hiyo, Rais Kikwete aliangua kicheko na kusema yaleo kali.
  “Ya leo kali tutarajie headline kesho,” alisema kwa kifupi Rais Kikwete bila kujibu hoja ya Sekirasa.

  Hiyo wakuu inakaaje-Rais anaishia 'kucheka' na kuhofia heading zitakavyokuwa magazetini kesho yake (leo)!!!!!????
   
 2. JOYCE PAUL

  JOYCE PAUL JF-Expert Member

  #2
  Mar 24, 2011
  Joined: Jan 8, 2010
  Messages: 1,007
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  nw wewe wasemaje juu ya taarifa hiyo isiyo na jibu?yaani hapo ni watendaji tu wanamwangusha rais
   
 3. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #3
  Mar 24, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kwani ungekuwa wewe ungefanyaje???? Stand on kikwete shoes . mimi mwenyewe ningecheka sana sana mtu kama huyo unamfukuza kazi hajui wajaibu wake

  jamaa naye hafai hiyo kazi aliyopewa .Hajui wajibu wake na nguvu zake.

  Ni aina ya watu amabao tatizo likitokea yeye anaaza kuangalia nje badala ya ndani . hafai kabisa anasubiri kikwete ndo aseme hayo

  • Amendika official barua ngapikulalamika.
  • kamuandia nani?
  Au ndo yale yale ya maboss kukutana breakpoint t kamandaXYZ akisema atashughulikia basi anadhani ni maelezo ya kiofisi.

  mambo hayaendi hivyo watu wengi tuko kwenye maofisi lakini hatujawi kuandika hata advice moja kwa maboss wetu . Ni aibu aibu.Wanajua kuandika perdiem tu na masurufu teh teh teh
   
Loading...