Rais ni kiongozi Mkuu wa nchi. Chini yake kuna vyombo mbalimbali vya kumsaidiakuongozi nchi. Vyombo hivi vimeundwa na watanzania wenzake ikiwemo taasisi ya haki za binadamu inayoongozwa Bi Kijo Bisimba.
Juzi Kijo Bisimba amemtahadhalisha Mhesimiwa Rais Dr. John Pombe Magufuli kuwa anapotumbua majipu, afuate sheria zilizowekwa.
Rais, jana amejibu hoja hiyo na kusema ataendelea kutumbua majipu kwa staili ileile. Akaenda mbali kwa kusema hata yeye ni jipu atamtumbua.
Hapa ndipo ninapopata shida.
Rais angeweza kumuita Mkurugenzi wa Taasisi ya haki za binadamu. Akamsikiliza maoni yake na sababu za msingi za kusema alivyosema. Staili ya kulumbana na mtu wa chini yako tena mbele ya vyombo vya habari siyo afya njema kwa utawala uwao wote ule. Ukiona baba analumbana na wanawe hadharani, ujue kuna tatizo. Ukikuta baba hayuko tayari kukosolewa kwa lolote lile ujue ustawi wa familia unakuwa shida.
Wilson Kabwe si kama na mtetea, la hasha! Ila alipaswa kusikilizwa, kama kuna tuhuma dhidi yake alipaswa kupelekwa mahakamani, maakama ingeamua kama ana makosa au hana. Utaratibu huu siyo wangu wala wa Wilson Kabwe ni wa kisheria ambayo Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli aliapa kufanykazi kwayo. Mwenye mamlaka ya kusema huyu ana makosa au la ni mahakama. Kumuita mtu mwizi, kawaibia sana watanzania bila uthibitisho wa kimahakama ni kuvunja sheria maana unaingilia mamlaka ya mahakama, jambo ambalo ni kuvunja sheria pia.
Hakuna tofauti na jamii inayochoma moto kwa matairi mtuhumiwa wa wizi wa kuku mitaani.
Alichokifanya Bisimba ni kama kibao cha njia panda kinachoonesha njia ya kwenda Hombolo ni hii ili anayetaka kwenda huko aifuate. Kukishambulia kibao ni ajizi, ni sawa na mtu anayekutaka kwenda njia ambayo haiendi Hombolo. Hombolo kutabaki kuwa Hombolo hata pasipo kuwa na kibao. Sheria itabaki kuwa sheria hata kama hakuna wa kuisemea.