Rais Anapokubali Awakilishwe na Wahuni na Watekaji Havunji Maadili ya Taasisi ya Urais?

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,707
71,018
Ukisikiliza mazungumzo ya mabishano kwa simu kati ya Mbunge wa Arusha Godbless Lema na mkuu wa wilaya ya Hai Ole Sabaya utagundua kuwa mheshimiwa Rais anawakilishwa katika ngazi mbalimbali na vijana wahuni na wanao jihusisha na jinai kwa kutumia madaraka waliyopewa na Rais.

Hili la Ole Sabaya la kuteka watu, kujaribu kuua na kudai hongo kwa nguvu limeanza kusemwa siku nyingi kabla ya kunaswa Leo kwa majibishano hayo. Jee taasisi zifanyazo kazi ya uchunguzi hazimwambii Rais matendo ya aibu yatendwayo na mwakilishi wake?

Au anaambiwa anapuuza kama anavyo puuza matendo ya aibu ya mteule wake mwingine Makonda?

Katiba inaruhusu bunge kujadili kumuondoa Rais madarakani kwa kufedhehesha mamlaka ya kiti chake jee kuruhusu wahuni kama Ole Sabaya kutumia jina la Rais kutenda uhuni na kupanga mauaji sio kufedhehesha kiti?

Maana wananchi wameelewa hivyo kuwa wahuni hawa wana go ahead ya Rais kufanya hayo.

Sasa hapo anahusika vipi hizo hulka za wakina Sabaya msimuhusishe Mh. Magufuli
alafu Lema mbunge wa Chuga Hai alikwenda kufanya nini
huyo katibu mwenezi ni mahaba yake tu
 
sasa hapo anahusika vipi hizo hulka za wakina Sabaya msimuhusishe Mh. Magufuli
alafu Lema mbunge wa Chuga Hai alikwenda kufanya nini
huyo katibu mwenezi ni mahaba yake tu
Rais ana organs zote za kupata tabia za viongozi wote, ndio maana mpaka katika level ya wilaya tunao DSO's kwa ajili ya kuripoti yote yanayo endelea. Kwa hiyo eitha haambiwi kwa hiyo hao watu hawafai au anaambiwa anadharau kuwa Watanzania ni wajinga watafanya nini. Jee tumefikia kuwa na rais wa hivyo mwenye kutudharau?
 
‘...community ya Wachagga...’

Mkiitwa Wakabila mnabisha
Mbona tunasema "usicheze na wakurya" tukiwa Tarime? Ukienda Singida unaambiwa usifanye mchezo na watoto wa kinyalu wewe!
Kule kwa Majaliwa Ruangwa niliwahi kuambiwa "ogopa community ya wamwera! Utapigwa mauno urudi Dar unachechemea"
Jee huo ulikuwa ubaguzi?
 
Rais ana organs zote za kupata tabia za viongozi wote, ndio maana mpaka katika level ya wilaya tunao DSO's kwa ajili ya kuripoti yote yanayo endelea. Kwa hiyo eitha haambiwi kwa hiyo hao watu hawafai au anaambiwa anadharau kuwa Watanzania ni wajinga watafanya nini. Jee tumefikia kuwa na rais wa hivyo mwenye kutudharau?

wakati mwingine mh.Rais anaona kama mnawajaribu wateule wake mfano wewe mbunge wa Mtama - Lindi unatoka jimboni kwako unakwenda jimbo la Masasi - Mtwara kwa sababu tu kuna kiji- online tv imeripoti utumbo anaona hamtoshi kabisa
 
sasa hapo anahusika vipi hizo hulka za wakina Sabaya msimuhusishe Mh. Magufuli
alafu Lema mbunge wa Chuga Hai alikwenda kufanya nini
huyo katibu mwenezi ni mahaba yake tu

Mada Imeanza ukisikiliza mazungumzo ya Lema na sabaya we unajadili lema alienda hai kufanya nini bila Shaka hujui ulichokiandika
 
OCD kakwaa kisiki Leo, na Mimi nasema hizo sifa zinamstahiki huo OCD
IMG-20191114-WA0151.jpeg
 
Kuna mahali nimeona watu wanasema hiyo si sauti ya Sabaya ila ni ya vijana wa Arusha.
 
21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom