Rais anapofungua Chuo,Shule,Hospital ni lazima alipwe?

Kennedy

JF-Expert Member
Dec 28, 2011
35,853
2,000
Je kuna ukweli wowote maana kuna habari nimezisikia eti Rais anapofanya kazi binafsi za watu ambazo si za Serikali lazima alipwe kwanza.Mfano ikiwa kama umejenga chuo chako,shule,hospital na unataka aje afanye ufunguzi baada ya majengo hayo kukamilika. Tafadhali kama kuna anaejua vizuri suala hili atujuze maana kwa upande wangu najua Rais anapofanya kazi zote hizo ni utekelezaji wa majukumu ya kila siku .
 

PhD

JF-Expert Member
Jul 15, 2009
4,279
2,000
Ndio mkuu kutoka ndani kabisa nakuhakikishia katika hafla yeyote ile ambayo rais anafungua kama mwalikwa, tayari kunakuwa na bajeti ya malipo ambayo inakuwa imeandiliwa kwa wahusika, ikiwa ni rais basi wasaidizi wa rais watawasilisha bajeti hiyo ikiwa na watu muhimu kama walinzi, wapishi, madereva, wasaidizi binafsi nk ili walipwe posho zao, hii inafanyika hata rais akiwa ziara mikoani, kwa waziri mkuu ni hivyo hivyo na pia kwa spika wa bunge wote wasaidizi wao hupeleka bajeti na huwasainia pesa mabosi wao. Kumbuka sakata la jairo Mizengo Pinda na Mama Makinda wote walichukua laki mbili na nusu kila mmoja, hii ndio Bongo bana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom