Kiti cha Rais hakipaswi kuwa wazi kwa namna yoyote ile. Hivyo kwa kujibu wa sheria na kanuni makamu wa rais anapaswa kuapishwa mapema sana ili kuziba pengo lililoachwa
 
Kwa mujibu wa katiba, Mama Samia (Rais) atashauriana na chama chake (CCM) ili kupata jina la Makamu wa Raisi.

Baada ya jina kupatikana, litapelekwa Bungeni kwa ajili ya kuidhinishwa kwa kura zaidi ya 50%.

Chanzo. Azamtv

Swali: Bunge hili lenye wabunge wa CCM zaidi ya 80%, wanaweza KUTOPITISHA jina la Makamu wa Rais endapo wataona hatoshi kushika nafasi hiyo?
 
Hakuna bunge kuna genge la CCM tu pale Wala jina halitapelekwa watatajiwa tu Kama kuteua na kupandisha majaji kulivokuwa kunafanywa na mpenzi zaidi wa Mungu.
 
Hakuna bunge kuna genge la cccm tu pale Wala jina halitapelekwa watatajiwa tu Kama kuteua na kupandisha majaji kulivokuwa kunafanywa na mpenzi zaidi wa Mungu
Ndugu, Mwenye enzi Mungu ana yake aliyo yapanga kwa taifa na watu wake , wakati wake na taifa lake... Tuishi kwa kulitukuza jina la muumba wetu awaye yote, mengineyo ni vyeo tu ambavo havina maana , humu duniani sote hatuna zaidi ya miaka 100 toka sasa...
 
Mosi, Rais wa JMT mama Samia baada ya kuapishwa atapendekeza jina la makamu wa Rais wa JMT ambaye atatoka kwenye chama chake cha CCM

Pili, makamu wa Rais mteule ataidhinishwa na bunge kwa kupigiwa kura ambako atatakiwa kupata 50% au zaidi kukalia kiti hicho.

Kwa sababu bunge lina wabunge wengi wa CCM yaani zaidi ya 95% inategemewa mchakato wa kura utakuwa mwepesi sana.

Maendeleo hayana vyama!
 
Apo kwenye"Lazima atoke kwenye chama chake cha CCM"ndo pamewakata maini wazee wakunyapianyapia wa Ufipa.
 
Mosi, Rais wa JMT mama Samia baada ya kuapishwa atapendekeza jina la makamu wa Rais wa JMT ambaye atatoka kwenye chama chake cha CCM

Pili, makamu wa Rais mteule ataidhinishwa na bunge kwa kupigiwa kura ambako atatakiwa kupata 50% au zaidi kukalia kiti hicho.

Kwa sababu bunge lina wabunge wengi wa CCM yaani zaidi ya 95% inategemewa mchakato wa kura utakuwa mwepesi sana.

Maendeleo hayana vyama!
Bora huu msiba ungetokea mwezi kama huu mwaka 2019/20! Nimewaza tu lakini. 🤔
 
Back
Top Bottom