Rais Anapoacha Kuhutubia Siku ya Uhuru......Inaashiria nini?

The Khoisan

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
13,486
2,000
Kwa mazoea tangu nikiwa mdogo kuna kawaida ya Rais kuhutubia siku ya uhuru. Wakati wa hotuba Rais pia alitumia mamlaka yake aliyopewa kuwasamehe wafungwa, n.k. Sasa imekuwaje mambo yamebadilika mpaka leo Rais anahudhuria gwaride tu na kuishia zake.

Je umuhimu wa sherehe ya Uhuru imekwisha??

Je kuna sherehe nyingine kubwa ya kitaifa zaidi ya uhuru??
 

Ibra Mo

JF-Expert Member
Oct 27, 2010
794
250
Apoteze muda wake kuwahutubia Wadanganyika afu achelewe kwenda kula Bata!!Hii ndo ccm Bhana watu wapo Ikulu wanakula Vyuku naku drink Mawine na Mawhisky saivi nyie Mtakomea kulialia nakunung'ung'unika tu hadi siku ambapo AKILI zenu zitakapokaa sawa.
 

hashycool

JF-Expert Member
Oct 2, 2010
6,574
2,000
Apoteze muda wake kuwahutubia Wadanganyika afu achelewe kwenda kula Bata!!Hii ndo ccm Bhana watu wapo Ikulu wanakula Vyuku naku drink Mawine na Mawhisky saivi nyie Mtakomea kulialia nakunung'ung'unika tu hadi siku ambapo AKILI zenu zitakapokaa sawa.

jioni bonge la party...kusheherekea uhuru....these crooks realy piss me off!
 

mapango

Member
Nov 3, 2010
88
95
Wadanganyika mumezoea kudanganywa danganywa, huyo amewasamehe kuwadanganya leo, si mufurahi!, sio lazima rais ahutubie katika sherehe ya uhuru, hasa ukizingatia hiyo Tanganyika yenyewe haipo, hicho alichokifanya ndio lazima, hayo mengine ni utamaduni tuliozoeshwa.
 

RedDevil

JF-Expert Member
Apr 30, 2009
2,373
2,000
Duh kama kweli hajahutubia basi kazi ipo, yaani jamaa anaona hakuna maana yeyote kuwa na uhuru. Yangu masikio!

Ila mimi napongezwa kutoka kila kona ya dunia huuku ughaibuni kwa kupata uhuru na najivunia uhuru wa nchi yangu, lakini nyumbani ndiyo hivyo tena. Tutafika tu, hakuna lisilowezekana wakuu.
 

ejogo

JF-Expert Member
Dec 19, 2009
990
225
Ahutubie nini wakati kwa miaka 49 bado tunapigana na umaskini, ujinga na malazi!! Ameiweka hotuba yake mpaka mwakani ambapo Tanganyika itakapotimiza miaka 50, labda mmojawapo wa hao maadui watatu atakuwa ameuwawa.
 

AmaniKatoshi

Senior Member
Mar 31, 2009
158
195
Kwa mazoea tangu nikiwa mdogo kuna kawaida ya Rais kuhutubia siku ya uhuru. Wakati wa hotuba Rais pia alitumia mamlaka yake aliyopewa kuwasamehe wafungwa, n.k. Sasa imekuwaje mambo yamebadilika mpaka leo Rais anahudhuria gwaride tu na kuishia zake.

Je umuhimu wa sherehe ya Uhuru imekwisha??

Je kuna sherehe nyingine kubwa ya kitaifa zaidi ya uhuru??


Yawezekana ni aibu ya kutokuwa na kitu cha maana cha kuwaambia watanganyika. Kumbukeni Dr Slaa alisema angeuweka mwenge makumbusho maana unasababisha matumizi yasionatija...JK na Mkapa wakamponda....leo wameogopa kuhutubia kwa sababu 49 years za uhuru ni kama vile jana ndio tumetoka kwa mkoloni....hakuna cha maana kilichofanyika...barabara zinaishia zile za mkoloni, viwanda vya mkoloni vimekufa, shule zile za mkoloni zimekuwa bora za kata, heshima utu na uwajibikaji wakatii wa mkoloni umegeukia kuwa UFISADI na kudanganya kwa hali ya juu...

Lakini, amefanya vyema maana amesoma alama za nyakati...watanganyika wanataka kusikia juu ya serekali tatu, juu ya katiba, juu ya udini ambao yeye na ccm yao waliuanzisha ambao haupo unawakost...etc....kwa nini aisiingie mitini?
 

Genekai

R I P
Feb 9, 2010
12,523
2,000
Amegundua hana jipya or si unajua mahotuba yake ni kuandikiwa inawezekana yamelowa maji hakuweza kuhutubia!
 

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,230
2,000
Kuana mambo mawili yanaweza kuwa chanzo:
1. watu walienda kuangalia gwaride akaona akianza kuhutubia watu watatoka akaabika kwa mara nyingine
2. khari ya mh. haikuwa nzuri si uliona ambulance
 

Consultant

JF-Expert Member
Jun 15, 2008
10,962
2,000
Shekhe Yahya atakuwa amemwambia yule ''shetani'' yupo mitaa ile na akiendelea kuhutubia ataanguka.

Sidhani kama alikuwa amekwenda pale kukagua gwaride tu then atimue. Kuna kitu kitakuwa kimetokea. Nani alihutubia ule umati wa watu instead?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom