Rais amtumbua Vita Kawawa na bodi yake, aagiza viongozi wa WETCU wakamatwe

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa ujumbe huo jana jioni, Alhamisi Machi 16, 2017 katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Isike Mwanakiyungi mkoani Tabora, ambapo amesema Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa TTB, Vita Kawawa pamoja na Mtendaji Mkuu wa Bodi hiyo Wilfred Mushi.

Waziri Mkuu pia amevunja Bodi ya WETCU pamoja na Bodi ya Tumbaku Tanzania – TTB kwa sababu ya kushindwa kusimamia zao hilo pamoja na matumizi mabaya ya fedha za umma.

Majaliwa amemuagiza pia Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora kuwakamata viongozi wanne wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Tumbaku (WETCU) pamoja na kufunga ofisi za chama hicho hadi uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za chama hicho utakapokamilika.

Viongozi wa WETCU ambao Waziri Mkuu ameagiza wakamatwe ni Mwenyekiti Bw. Mkandara Mkandara, Makamu Mwenyekiti Bw. Msafiri Kassim, Mkaguzi wa Ndani na Mhasibu Mkuu. Pia amewasimamisha kazi watumishi wa kitengo cha uhasibu wa chama hicho hadi uchunguzi utakapokamilika.

“Kuanzia sasa watumishi wote wa kitengo cha uhasibu pamoja menejimenti nimewasimamisha kazi pamoja na Mrajisi wa mkoa wa Tabora Deogratius Rugangila. Kamanda hakikisha ofisi hazifunguliwi kuanzia sasa hadi hapo timu ya ukaguzi itakapokamilisha kazi yake,” amesisitiza.

Waziri Mkuu amesema kwa muda mrefu wakulima wameteseka na zao hilo kukosa tija kwa sababu ya usimamizi mbovu wa viongozi wa ushirika na Bodi ya Tumbaku Tanzania jambo ambalo Serikali haiwezi kulivumilia.

Amesema “Hatuwezi kuwa na ushirika ambao hauwasaidii wanachama. WETCU walipokea sh. bilioni 15 ambazo walizikatia risiti na hazijaonekana. Pia waliwalipa wazabuni sh, bilioni 10 ambazo hawajazikatia risiti,”.

“Wakati wanachama ambao ni wakulima wakiendelea kuteseka WETCU walinunua gari la sh. milioni 269 kinyume na na maelekezo ya Mkutano Mkuu wa wadau ambao ulipitisha zitumike Shilingi milioni 40 tu,” amesema.

Waziri Mkuu ameongeza kuwa chama hicho kimesababisha kupungua kwa uzalishaji kwa kiasi kikubwa kutokana na kuwa na menejimemti mbovu jambo ambalo limechangia wakulima wa tumbaku kukosa tija.

Amesema WETCU kimekithiri kwa matumizi mabaya ya fedha ambapo alitolea mfano suala la ukarabati wa ofisi tatu ikiwemo ya makao makuu ambayo ilipangwa ikarabatiwe kwa sh. milioni 33 wakatumia sh. milioni 170 na ofisi za Tabora na Urambo zilipangiwa sh. milioni tano kila moja na hazikukarabatiwa.

Pia Waziri Mkuu amepiga marufuku ununuzi wa mbolea kutoka nje ya nchi wakati ikiwa inazalishwa hap nchini. Aidha, alimepiga marufuku matumizi ya dola katika sekta ya tumbaku na badala yake zitumike fedha ya Kitanzania kwa sababu kitendo hicho kimekuwa kinawanyonya wakulima.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mheshimiwa Aggrey Mwamri, wakuu wa wilaya zote za mkoa huo pamoja na Maofisa Kilimo na Ushirika kuhakikisha wanasimamia vizuri zao hili ili liweze kuwa na tija kwa wakulima na Taifa kwa ujumla.

Pia amewaagiza Maofisa Kilimo waende vijijini na kuwatambua wakulima wa tumbaku katika kila kijiji na kuwasajili. “ Kuanzia leo Maofisa Ushirika wabadilishe mienendo ya kazi nataka wasimamie zao la tumbaku kwa umakini zaidi.” Alisema.

VIDEO:

7-16.jpg

6-28.jpg

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wadau wa zao la tumbaku kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Machi, 16, 2017. Kulia ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba na katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Aggrey Mwanri.
3-57.jpg

Mwenyekiti wa WETCU, Gabriel Mukandara na Makamu wake, Msafiri Ngassa (kushoto) wakiwa kwenye gari la polisi baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuagiza kuwa wakamatwe na kuwekwa ndani hadi uchunguzi kuhusu utendaji wao utakapokamilika. Majaliwa alikuwa akizungumza na Wadau wa zao la tumbaku kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Machi 16, 2017.
 
Hizo hela zilienda kwa watu wa chama cha magamba na hapo ulikuwa ni uchochoro wa kupitia tu jamaa wamekuwa victims sababu hiyo tu, pia bado tunaendelea kuondoa masalia ya mkwere.
 
Pole Vita Kawawa mtoto wa Simba wa vita, hii ni Tanzania ya Magufuli sio ile tuliyoizoea

Hawa walibebwa sana enzi ya mkweree ingawa walikuwa na tuhuma nzito za ujangili wa kuua TEMBO huko Selous national park!!! Sasa hivi habebwi mtu pengine Bashite peke yake kwani wanasema wao hapani kazi tu!!!
 
Hii serikali yenyewe mpaka sasa imefanya makosa mengi na inastahili kura ya kutokuwa na imani kama alivyo-suggest Zitto siku za nyuma na hivyo imepoteza uhalali wa kutumbua wengine.

Maamuzi ya kutoa asilimia 230 ya fedha za bajeti kwa baadhi ya wizara huku zingine zikiambulia asilimia 16 tena bila kuzingatia utaratibu ni ufisadi mkubwa huku serikali hiyo hiyo ikijicha kwenye kwapa la kutumbua wengine huku yenyewe imejaa madudu kibao na mengine yakiwa ni ya kuvunja katiba,hakika hii sio sswa na haikubaliki.

Inashsngaza serikali hii inayojidai kujali fedha za umma lakini CAG analalamika kupewa bajeti ndogo kiasi kwamba anashindwa kufanya kazi zake.

Mnatafuta sifa kwa kutumbua wengine huku madhambi yenu mkiyakalia kimya mkidhani mtatuhadaa.

Ni serikali hii hii mpaka sasa imeamua kukaa kimya juu ya swala la Bashite na wabunge wa CCM kutuhumiwa kuhongwa milioni kumi kumi.

Ni serikali hii imeamua kukaa kimya juu ya kashifa ya Lugumi lakini iko mstari wa mbele kutumbua wengine.

Setikali hii hii iliyo mstari wa mbele kutumbua wengine imeshindwa kukunasusha habari ya gazeti la Mwananchi kuwa Raisi ametisha wabunge wa CCM kumuwajibisha waziri mkuu alafu inajisifu yenyewe iko safi.

Ni serikali hii hii iliyo mstari wa mbele kutumbua wengine lakini iko kimya kuhusu Bashite!!


Nawambieni tumewshawajua tabia yenu na kwa doublestandard yenu hii umma hautawaamini kwa lolote hata mkifanya mazuri na tutawakataa tu kwenye sanduku la kura kama walivyofanya majuzi wananchi wa Manispaa ya Lindi katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Hauwezi kunyoosha nchi kwa doublestandard ya kiwango hiki sana sana utaharibu tu maana huwezi kusafisha huku na wakati huo huo wewe mwenyewe unaharibu kwingine.Huku ni kujidanganya tu.

Sheria ni msumeno.
 
Back
Top Bottom