Rais amteua katibu wa CCM kuwa mkurugenzi wa halmashauri (DED) na msimamizi wa uchaguzi kinyume cha sheria na taratibu cha cheo husika

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,571
2,000
Unaweza kushangaa lakini hii ndio hali Taifa lilikofika, tukisema tu watu hawatuelewi, lakini kazi yetu ni kusema, tutaendelea kusema iko siku watu watatuelewa.

Huyu Jimson Mhagama aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi anakwenda kuwa msimamizi wa Uchaguzi katika majimbo ndani ya wilaya hiyo, (Returning officer) wakati sasa hivi anavyoteuliwa alikuwa ni Katibu wa CCM Mkoa wa Ruvuma, akitokea Singida na alikuwa Katibu wa ccm wilaya ya Mufindi.

Sheria za Tamisemi zinaainisha sifa za Wakurugenzi na moja ya sifa kuu ya kwanza ni lazima wawe watumishi wa serikali na wawe wameongoza idara katika serikali kwa angalau miaka kadhaa.

Leo UVCC na makada wao wengine ndio wanakwenda kuwa wasimamizi wa uchaguzi, je unataraji huyu amtangaze mshindi wa upinzani 2020????

FB_IMG_1554815582406.jpg

Na Yericko Nyerere
 
Cheko Lamhenga

Senior Member
Aug 1, 2018
166
225
Wivu na chuki ni mbaya zinatuchelewesha katika maendeleo, Mi sioni shida kuteuliwa mtu wa namna hiyo cha msingi achape kazi.
 
Bonny

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
13,329
2,000
Upinzani mnalalamika sana ki ukwel kusema huku mitanadaoni haitoshi inabd ifike hatua mtafute njia mbadala maana hii mpka sasa haijawa na utatuzi, Kama Rais amekosea kufanya uteuzi kutokana na sheria inavyosema pelekeni shaur mahakaman ikapatikanae tafsir sahihi ya hilo jambo. Ikishindikana Mahakaman sasa mje niwape mbinu nzur zaid ya hyo
 
Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
10,348
2,000
Hizi mambo zingefikia kikomo pale tu Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba ingepita kama ilivyo na kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Subira the princess

JF-Expert Member
Mar 3, 2018
1,997
2,000
Unaweza kushangaa lakini hii ndio hali Taifa lilikofika, tukisema tu watu hawatuelewi, lakini kazi yetu ni kusema, tutaendelea kusema iko siku watu watatuelewa.

Huyu Jimson Mhagama aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi anakwenda kuwa msimamizi wa Uchaguzi katika majimbo ndani ya wilaya hiyo, (Returning officer) wakati sasa hivi anavyoteuliwa alikuwa ni Katibu wa CCM Mkoa wa Ruvuma, akitokea Singida na alikuwa Katibu wa ccm wilaya ya Mufindi.

Sheria za Tamisemi zinaainisha sifa za Wakurugenzi na moja ya sifa kuu ya kwanza ni lazima wawe watumishi wa serikali na wawe wameongoza idara katika serikali kwa angalau miaka kadhaa.

Leo UVCC na makada wao wengine ndio wanakwenda kuwa wasimamizi wa uchaguzi, je unataraji huyu amtangaze mshindi wa upinzani 2020????

View attachment 1066922
Na Yericko Nyerere
Solution ni kwa vyama vya siasa kutoshiriki chaguzi bila tume huru ya uchaguzi
 
Subira the princess

JF-Expert Member
Mar 3, 2018
1,997
2,000
Upinzani mnalalamika sana ki ukwel kusema huku mitanadaoni haitoshi inabd ifike hatua mtafute njia mbadala maana hii mpka sasa haijawa na utatuzi, Kama Rais amekosea kufanya uteuzi kutokana na sheria inavyosema pelekeni shaur mahakaman ikapatikanae tafsir sahihi ya hilo jambo. Ikishindikana Mahakaman sasa mje niwape mbinu nzur zaid ya hyo
Unaongelea mahakama IPI? Mahakama zimebakwa na dola au unaishi nchi gani?
 
Kilangila

JF-Expert Member
Jul 22, 2013
1,819
2,000
unaweza kujiua ukafa ukatuacha wengine tukiendelea kufurahia matunda ya nchi yetu
Huyu tulie naye sidhani kama anajali hata ikibidi kuua mamilioni ya watu kulinda cheo na chama chake. Mimi naogopa hata kusogea karibu naye. Hata si binadamu wa kawaida. Ikibidi acha tu nife kuliko kushuhudia udhalimu unaoendelea. Kilangila.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom