Rais amteua Dkt. Mussa Assad kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu

Mtoto wa Mkulima

JF-Expert Member
Apr 12, 2007
681
126
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dkt. Mussa Asaad kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania.

Dkt. Asaad ni Mhadhiri Mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na atashikilia nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu. Rais amemteua Dkt. Asaad kwa mujibu wa kifungu Na. 31(1) cha sheria ya Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (The National Board of Accountants and Auditors Act) ya mwaka 1995,na uteuzi huo wa Dkt. Asaad umeanza rasmi tarehe 29 Agosti, 2007. Gray S. Mgonja KATIBU MKUU-HAZINA
 
Ninamfahamu Assad kwa juujuu, nadhani kila aliyepitia pale Mlimani alikuwa anazungumza kuogopa kukamatwa na Assad. Jamaa yuko fiti sana. sio kama amepunguza unene wake.
 
Ninamfahamu Assad kwa juujuu, nadhani kila aliyepitia pale Mlimani alikuwa anazungumza kuogopa kukamatwa na Assad. Jamaa yuko fiti sana. sio kama amepunguza unene wake.

Yeah Jamaa yuko fit sana. nakumbuka kitabu chake pale mlimani watu wanakiogopa na huwa wanakesha chini ya Mdigirii (mti. Ila jamaa yuko fit sana najua pia anacosultance firm yake pale maeneo ya posta. Ukimuona jamaa utafkiria ni Dr Dre maana mshikaji kama mmarekani hata ongea yake.
 
Dr. Mussa J Assad ni mtu makini sana,na watu wa type kama yeye ndio wanatakiwa wakamate sehemu kama NBAA ili uhuni wa watu kuuziwa mitihani ukome kabisa bongo(waliosoma AC 100 na AC 101 pale Mlimani wanaweza kusema zaidi),ninamfahamu kwa muda na nimeshafanya kazi naye,ni mtu anayependa kuchukua mawazo ya kila mtu na kuyapima,watu wa NBAA mpeni ushirikiano wa kutosha!


rejea article yake kuhusu makala yake ya degree za wahadhiri vihiyo wa Mzumbe University.teh teh
Hongera Dr. Assad
 
rejea article yake kuhusu makala yake ya degree za wahadhiri vihiyo wa Mzumbe University.teh teh
Hongera Dr. Assad

Samahani wadau,,, naomba link ya hiyo makala!!! huenda mmejadili hapa kabla sijazaliwa na kubatizwa kwa jina la kilitime bini JF!
 
Nilijua tu kwamba hiyo ya dini itaibuka!!!!.
Kaka jamaa ana credentials zinazo mruhusu kuchukua hiyo job....mambo mengine ni coincedences tu, hiyo "highway" ya udini itawapeleka pabaya.
 
Mimi Nampongeza Kikwete kwa issue ya kuchagua viongozi wazuri especially kwenye taasisi nzito,,, zile zisizokuwa za kisiasa...

1. Mdhibiti/Mkaguzi Mkuu wa Hesabu Za Serikali
2. Jaji Mkuu
3. Accountant General
etc...

Ila sina uhakika na uwezo wa Mwanasheria Mkuu!!!


Kwenye viongozi wa siasa, siko naye kabisa,,,, kwa mfano uchaguzi wa mtangazaji mmoja wa kituo kikubwa cha media, kuwa mkuu wa wilaya moja ya mikoa ya pwani... hapo hapana!!!
 
kilitime;83124]Mimi Nampongeza Kikwete kwa issue ya kuchagua viongozi wazuri especially kwenye taasisi nzito,,, zile zisizokuwa za kisiasa...

1. Mdhibiti/Mkaguzi Mkuu wa Hesabu Za Serikali
2. Jaji Mkuu
3. Accountant General
etc...

Ila sina uhakika na uwezo wa Mwanasheria Mkuu!!!
Kidogo na Mwema pia namkubali kiaina
 
Mimi nasikitika simjui mtu huyu ila nampongeza kwa uteuzi.
Leo watanzania hatutaki sifa tunataka kazi maana we have been blocked to develop for more than thirty years...
 
Hivi amechukua nafasi ya nani? Na je Mzee Reginald Mengi hakuwa Chairman wa Board hii? au Makongoro Mahanga?

Hata hivyo nampongeza Dr Assad ni miongoni mwa wasomi vijana wenye potential kubwa kwa taifa hili. I just wish him to be given executive role in the near future
 
..jamaa anafaa!
..ac100!akikuambia ukasome kile kitabu chake alichoandika na yule sista we kasome,usitake mengine!utakunywa supu!
..ila,mashavu ndo yatazidi kuongezeka!ingawa sijamkutana muda kidogo!
..ameacha kuvaa suruali za kubana?
..nilijua ipo siku atafika mbali!nimefurahi!

..hayo mambo ya dini,mbona kila mmoja anayo!kwani ben enzi zake ilikuwaje?
..hapo mi namwona assad,sio mwislam!
 
Hongera zake Dr Assad,Ni mtu mchapa kazi na anayejua kwa dhati ufuatiliaji,Naamini kuwa NBAA imepata kiongozi makini,kwani pia ni msikivu na mpenda maoni.Hongera Mkuu!!
 
Sasa nimeanza kumfahamu baada ya kuwasoma wanafunzi wake wengi hapa. ninampongeza kwa kuteuliwa.
Nawaasa watanzania kuacha siasa za dini maana hatutafika popote. uwe mwislam, mkristo, mpagani haikuongezei sifa za ubora. Cha msingi uchapa kazi na ubunifu. Mimi si mwislam lakini bado nawaona waislam kama ndugu zangu wa dam. Bila wao mimi sina thamani
 
Congrats Dr. Assad.

Where is Nungwi?, I'm eagerly waiting for his comments :(
 
Congrats Dr. Assad.

Where is Nungwi?, I'm eagerly waiting for his comments :(

Nipo nipo nimejaa tele! nimeacha maksudi kusema chochote kuacha haki na demokrasia ya JF ichukue mkondo wake.

Finally justice not only has been done but also has seen to be done!

CV ya Dr Assad ni unquestionable, amebobea ktk taaluma ya uhasibu na ni mtu asie na maskhara ktk mambo ya taaluma. NBAA wameramba dume, of recent appointments by JK this will go down as best of all.

Im running out of words to explain his credentials Im just wishing him all the best.

Congratulations to Dr Assad
 
Nipo nipo nimejaa tele! nimeacha maksudi kusema chochote kuacha haki na demokrasia ya JF ichukue mkondo wake.

Finally justice not only has been done but also has seen to be done!

CV ya Dr Assad ni unquestionable, amebobea ktk taaluma ya uhasibu na ni mtu asie na maskhara ktk mambo ya taaluma. NBAA wameramba dume, of recent appointments by JK this will go down as best of all.

Im running out of words to explain his credentials Im just wishing him all the best.

Congratulations to Dr Assad

Mkuu Nungwi naona falsafa ya demokrasia JF imekujaa mkuu. Msikaji mimi namfahamu sana ni mchapakazi ni kijana wa kileo. Ukimwangalia kwa mbali nakumbuka na benzi lake jekundu jamaa ni simple sana na anajichanganya na watu na zaidi nasema jamaa yuko exposed kiana.
 
Hivi amechukua nafasi ya nani?
na mimi nauliza vivyo hivyo au nafasi ilikuwa wazi?

Watu wengi wanateliwa na muungwana sijasikia wanaositishwa kazi!

Hongera Assad, hope hautajiunga nao utakaposhindwa kupambana nao.
 
Back
Top Bottom